(¯`·._.In Loving Memory Of My Mother._.·´¯)

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
(¯`·._.•In Loving Memory of My Mother™•._.·´¯)


Assalamu Alaikum
Amani iwe nanyi.


Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu kwa wote ambao walithubutu kuniandikia email na PM kutaka kujua wapi na mahala gani msiba utakuwepo, kwa bahati ghafi, nilipotoa taarifa ya msiba, sikujaaliwa tena kuingia Jf na kuwafahamisha wale ambao kwa mapenzi yao juu yangu walitaka kwenda kuzika na kuna ambao wamediriki kutaka kutoa mkono wa rambirambi. Kwa kweli mmenionyesha jambo kubwa sana katika maisha, hakika nimejifunza mengi mno katika msiba huu.

Kwa taarifa tu mazishi ya Mama mpendwa yalifanyika siku ile ile aliyofariki, jioni mida ya saa kumi. Na kufuatiliwa na Dua kwa siku tatu za msiba tangia alipo fariki...!

Nawashukuru nyote kwa kutumia wakati wenu na kuonyesha kujali, sina neno ambalo linaweza kuwakilisha shukrani zangu kwenu zaidi ya kusema Ahsanteni sana na nimefarijika sana sana, bila kifani.

Hakika Mwenyezi Mungu amesema kweli kuwa ...ameumba mauti na uhai ili kutujaribu ni yupi miongoni mwetu atakayefanya mambo mema.

"Inna-Kula-Shay-In Khalqnahu-Biqadar"
Kwa Hakika Sisi Tumekiumba Kila Kitu Kwa Kipimo.
Verily, All Things Have We Created In Proportion And Measure.
Qur'an 54:49

Du'aa
"Amani ishuke juu yenu watu waliotutangulia walio waumini, nasi apendapo Mwenyezi Mungu tutakutana nanyi, tunamuomba Mwenyezi Mungu atusamehe, sisi na nyinyi.

Na Mwenyezi Mungu awarehemu wa mwanzo na wa mwisho wetu namuomba Mwenyezi Mungu atupe sisi afya njema na siha njema."

Amin Summa Amin

Dua hii iwaendee wote walio ondokewa na wazazi wao, ndugu na jamaa wote waliotutangualia Insha'Allah Mwenyezi Mungu atuwafikishe dua hii iwanufaishe maiti wetu.

Hakika Mtu mwema ni hai hata kama atahamishwa katika makazi ya wafu.
 
Mkuu pole sana kwa kufikwa na mtihani, kifo ni chetu sote ila hakizoeleki, nakuombea mwenyezi mungu akupa subira ktk kipindi hiki kigumu, na azidi kujaza imani kwa kila mtihani ukupatao, kwa mama tunamuomba m'mungu amsamehe madhabi yake yote aliyoyatenda wakati wa uhai wake, amuondoshee adhabu za kaburi na siku ya kiyama, aje kumjaalia awe miongoni Mwa waja wake watakaoingia ktk pepo yake takatifu...."INNA LILAH WAINNA ILAHIN RAJ'UUN"
 
Umpe ee bwana raha ya milele na mwanga wa milele umwangazie apumzile kwa amani. Roho ya mama yake X-Paster ipate rehema kwa Mungu na ipumzike kwa amani. Amen.
 
:angel:Aliye mpenda zaidi kamchukua tumuombee afikie paradiso ya huko tuendako na sisi kwani ndiyo njia yetu!!Mungu aiweke roho ya mama maalipema peponi,Amen wote tuseme amen!.:rip::amen:
 
MKUBWA X-PASTER,
Nilipoona tangazo lako nilikata tamaa sana, maana ilinikumbusha yaliyonipata miaka kadha iliyopita.
Pole sana kiongozi, Mwenyezi Mungu amrehemu Mama yako, na ampumzishe katika pepo mwanana!
 
ewe Allah, msamehe makosa yake mama yetu, na umpatie rehema zako, na uyafanye mepesi makazi yake mapya ya barzakh (maisha ya kaburini) na umpanulie kaburi lake na umtilie nuru! hakika wewe Allah ni mwenye kupokea tauba, mwenye huruma!
 
Alleluya!! ...ipo siku tutaonana,amrehemu Mungu mwenyezi.

Kwa pamoja tuseme Amen.
 
Nawausia muwe na subira na kuridhika wakati wa msiba mara ya kwanza na museme:

إنا لله وإنا إ ليه راجعون اللهم أجرنا فى مصيبتنا واخلف لنا خيرا منها
"Bila shaka tunatoka kwa Allaah سبحانه وتعالى na Kwake ndio marudio. Ee Allaah Tupe ujira katika msiba wetu huu na Utubadilishiye lililo bora zaidi kuliko huo msiba."



((استغفروا لأخيكم وسلوا له التثبيت فإنه الآن يسأل))
((Muombeeni maghfirah ndugu yenu na mumtakiye uimara (kutoyumba) kwani sasa anaulizwa)) [Abu Daawuud]

Jueni kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema:((ينقطع عمل ابن آدم من الدنيا إلا من ثلاث : صدقة جارية أو علم ينتفع به أو ولد صالح يدعو له))

((Amali ya binadamu hukatika baada ya kufa ila kwa mambo matatu: Swadaqah yenye kuendelea, elimu yenye manufaa au mtoto mwema anayemuombea)) [Muslim na Ibn Maajah].


Ee Mola Msamehe… na Umrehemu…Muinue daraja yake awe wa karibu walioongoka… Wabadilishie kizazi chake kwa yaliyopita…Na Utusamehe sisi na yeye. Ee Mola wa Ulimwengu…Mpanulie kaburi lake…na Umtilie mwangaza




 
Back
Top Bottom