segwanga
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 2,789
- 729
Nimekuwepo pale nafanya kazi pale kama mwalimu.Kuwepo kwangu pale kwa miezi mitatu lilikuwa darasa ambalo sikutegemea kulipata.Sifanyi umbeya wala simhalibii bepari anayemilki shule wala siwahalibii walimu na wafanyakazi waliopo pale,wala siwaharibii wanafunzi na wazazi wao.Nimejifunza yafuatayo:1 sababu zilizotolewa na haki elimu na Ndarichako kuwa wanafunzi walifeli kwa sababu hawako makini,ni za ukweli wanafunzi hawasomi mpaka walazimishwe kwa kusimamiwa 2.Nimetambua kwa nini walimu wana badilisha shule kila uchao.Kwa bepari yule,walimu wanaoweza kufanya naye kazi ni wale ambao wamekosa sehemu nyingine,wamestaafu,wanaegesha au wanafki ambao wanajipendekeza kwa bepari.Kuwa mwl pale hauna tofauti na mbwa hauthaminiwi, unatumiwa tu kama box na wakati wowote waweza kutupwa kama takataka.3 Kazi ya ualimu inadharauliwa kuliko nilivyokuwa nafahamu.Bepari ambaye hata hajasomea ualimu anajifanya ndo anafahamu kuliko walimu waliosomea eti anawafundisha walimu.Usitarajie kiwango cha elimu kipande.4.Hakuna mkataba kwa kazi ya ualimu kwenye shule za private.Wakati wowote bepari akijisikia kukutimua anakutimua na wewe ukijisikia kusepa unasepa tu.5 Usipate na tatizo litakalokuchukua wiki mbilg hvi,utaambiwa uchague moja kati ya kazi au matatizo yako (ndicho kilichonitoa pale).6 Hakuna kodi ya serikali inayochukuliwa kwa sababu wafanyakazi wanachukulia mishahara dirishani.7 Hakuna hela inayopelekwa nssf.HAYO NDIO NILIYOJIFUNZA KWA SIKU 90 NILIPOKUWA PALE GREEN ACRES MABEZI