89.5 FM wananikumbusha mbali sasa hivi

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,617
37,815
Wakumbwa,

Sasa hivi nipo online na 89.5, Jamaa wananikumbusha mbali sana enzi za Dar Jazz - tumemaliza ngoma inayoibwa " Bwana mashaka....... acha kulalamika....kama amekushinda mrudishe kwao...."

Jamani wenye viredio maofisini wekeni tujikumbushe enzi zetu, wakati huo hakuna mgawao wa umeme, hakuna ukimwi, hakuna foleni, hakuna matapeli, yaani maisha yalikuwa swafiii......

tuendelee kujikumbusha..... Sasa hivi inapigwa Makiwa.....

Nimekubalii........yanayosemwa na watu.....wanaopendwa na wengi siku zote hufa wangali vijana........chiku wangu weeee....chiku wangu daima nitakukumbuka......chiku wangu eeee kalale pema peponi...... tararaaaaaaa taraaaa.....
 
daa mkuu wewe km mimi hizi nyimbo nna historia nazo saaana, dede naye kwenda msondo dah katuangusha saaaana wana sikinde. kuna wakati mtangazaji kaitangaza safu ya ddc mlimani park kwa kweli machozi yalitaka kunitoka. akina chidumule mwanyiro abel mulenga gama gurumo bichuka wakati ule sauti yake haina mfano. kuna kibao km unanionyesha njia ya kwetu haujapigwa hapo lkn sauti ya bichuka pale ilikuwa imefikia kilele. sasa wanamuongelea TABIA MWANJELWA.
 
Sikiamidomo ya bata inavyotembea hapo,... wacha kabisa mkuu!! hairudi tena enzi hii.
sasa hivi ni makelele na majina tuu kwenye nyimbo mwanzo mwisho!!!
 
Wakumbwa,

Sasa hivi nipo online na 89.5, Jamaa wananikumbusha mbali sana enzi za Dar Jazz - tumemaliza ngoma inayoibwa " Bwana mashaka....... acha kulalamika....kama amekushinda mrudishe kwao...."

Jamani wenye viredio maofisini wekeni tujikumbushe enzi zetu, wakati huo hakuna mgawao wa umeme, hakuna ukimwi, hakuna foleni, hakuna matapeli, yaani maisha yalikuwa swafiii......

tuendelee kujikumbusha..... Sasa hivi inapigwa Makiwa.....

Nimekubalii........yanayosemwa na watu.....wanaopendwa na wengi siku zote hufa wangali vijana........chiku wangu weeee....chiku wangu daima nitakukumbuka......chiku wangu eeee kalale pema peponi...... tararaaaaaaa taraaaa.....

Mkuu usisahau kuisikiliza hii kitu kwenye RFA kila alhamisi saa nne usiku mpaka saa saba ni balaaaaaaaa!!
 
sikiliza OSS sasa MARA YA MWANZO ULIANZA KUNIOMBA NICHEZE MUZIKI WA KWETU SIWEZI KUKATAA aaaaah mungu wangu hii ndo ikikuwa miziki baaaana
 
uliza kwanza siyo uaanza kufanya upuuzi wako hapa,... dukuduku ni wasi wasi wao bwana eeeee,.... dili dnyu ndiili ,....
 
kulikuwa na safu ya zilipendwa jf baada ya mabadiliko wakaitoa MODS ilikuwaje tena? rudisheni ile kitu bana!!!!
 
Halafu kuna "Nikusimulie hadithi Mpenzi Kristina, kuhusu ule ugomvi wetu uliotokea baina yangu na Wewe unafanya vibaya unafanya vibaya" Kimulimuli hao jamani
 
Umeshakuwa mtu mzima Somboko Amba eeee na mambo ya starehe hukuyaanza leo - tara tra tra tra traaaaaaaaa...........

Heshima mbele Fuso...
Pale Kamanda anasema
''umeshakuwa mtu wa makamo
Somboko amba eeh
Na mambo ya starehe hukuyaanza leo''

Hasemi umeshakuwa mtu mzima...
 
Back
Top Bottom