80% ya watanzania wameajiriwa sekta ya kilimo, huku serikali bado inategemea mvua kwa kilimo

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
kutokana na ta kwimu za serikali, 80% ya "waajiriwa" wapo kwenye sekta ya kilimo, serikali hajiweka mikakati thabiti yakuhakikisha "ajira" kubwa kuliko zote nchini zinapewa kipaumbele. Bado mpaka leo serikali inategemea kilimo cha mvua kusaidia sekta hii nyeti nchini. Mvua zenye zimedhiirisha kwa minaga mingi tu sio zakutegemea , hapa Tanzania na duniani pote. Kilimo cha umwagiliaji bado hakijapewa kipaumbele na umuhimu unaostahili.

Kwa hali hii wananchi wengi kwenye hii sekta muhimu inayotoa ajira kubwa kuliko zote wataendelea kuteseka na matatizo kama njaa yataendelea kuisumbua nchi hii kwa miaka mingi sana mbeleni.

Juhudi zinazowekwa na serikali mpaka sasa hazijazaa matunda, ingawa zinaonekana ni nzuri.

Serikali imetoa mbolea nyingi kusaidia wakulima nchini Tanzania. Lakini kila siku kwenye vyombo vya habiri utasikia wahusika wa kusambaza "vocha" wamewapatia watu wasio husika na mashirika yasio kuwemo kwenye list ya kupatiwa vocha hizo.

Tatizo jingine ni matreka ya kilimo kwanza. Stori ni zile zile. Serikali imeingia gharama kubwa mno kuagizia matrekta haya lakini matunda yake ni madogo sana. Kila kukicha unasikia viongozi wa maeneo mbali mbali nchini wanatumia matrekta haya kwa mambo yao binafsi. Matreka ya kilimo yanatumika kubebea mizigo. Hii inaonyesha wazi kabisa serikali ilikua haijawaandaa kwa kuelimisha wakulima na jamii juu ya mpango wake wakuboresha kilimo nchini. Pia ufatiliaji wa maendeleo ya mipango ya serikali kuboresha kilimo ni wachini sana kama haupo kabisa..

Tuweke siasa pembeni, ni wakati serikali iongeze bidii kwenye kufatilia mambo yenye umuhimu kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom