775 Billions deni la barabara, serikali inadaiwa

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Mwaka Jana TANROADS walikuwa wanadaiwa billion 300. Hazijalipwa.

Mwaka huu TANROADS wanadaiwa 475 billion za Barabara.

Sasa kwa nini Serikali ina kiherehere cha kulipa DOwans
 
CCM na Mrema wake , nahisi deni litakuwa sana mpaka bajeti ijayo waanze kutukanana bungeni. Unafiki wa Magufuli utaonekana wazi
 
Magufuri kakuta deni.Load fund zilishaliwa na wajanja.Kama mnakumbuka magufuri alisema aliporudishwa miundo mbinu kuwa: mwaka 2005 kujenga kilomita moja ya lami ilikuwa shs.350milion baada ya miaka mitatu gharama zilifika shs.1.2 bill hapo unategemea nini???? madeni yale siyo realistic yamekuwa inflated ili kuweka mgawao wa mafisadi.
 
Vipi Mishahara ya wafanyakazi imelipwa mwezi wa kumi?

Je zile za Polisi zimerudishwa?
 
Wanajisifu kila siku kwamba serikali imejenga barabara za lami kumbe ni mikopo! Kuna tofauti gani na sharobaro anayejisifu kupendeza kwa nguo za kuazima au za kukopa huko hana akili ya kujiingizia kipato. Au kujisifu kuwa unakula vzur huku unamadeni kibao dukani kwa jirani! Kwa kifupi serikali imefilisika na hawana namna tena!
 
Lazma tukubali hakuna serikali isiyodaiwa. Cha msingi ni kuwapo na plan za kukagua uhalali wa hayo madeni na kuyalipa bila penalties ili kutowaumiza wananchi. Custodians wa kodi zetu shurti waone uchungu kidogo wajameni!
 
Mwaka Jana TANROADS walikuwa wanadaiwa billion 300. Hazijalipwa.

Mwaka huu TANROADS wanadaiwa 475 billion za Barabara.

Sasa kwa nini Serikali ina kiherehere cha kulipa DOwans

Nashagaa! Halafu Igunga wanadanganyika kirahisi eti Magufuli atajenga barabara na daraja!
 
Lazma tukubali hakuna serikali isiyodaiwa. Cha msingi ni kuwapo na plan za kukagua uhalali wa hayo madeni na kuyalipa bila penalties ili kutowaumiza wananchi. Custodians wa kodi zetu shurti waone uchungu kidogo wajameni!

Sawa, lakini mbona madeni ya serikali yetu mengi sana? Ukiacha hayo ya nje, waalimu, polisi, etc etc etc na bado tunaambiwa ya barabara!
 
Wakati Mkapa anaondoka Magogoni Tanzania ilikuwa inafanya vizuri sana kwenye hii sekta ya barabara. Kenya walikuwa wanapata somo hapa na gharama za ujenzi zilikuwa zinaeleweka.

Then wakaja wanamtandao na kupachika watu wao, gharama zikapanda, viwango vikashuka! Lakini kubwa zaidi kukawa na miradi ya barabara ambayo haikuwa kwenye bajeti. Wafadhili wamepiga kelele sana huu mtindo wa kutekeleza 'miradi ya wakubwa' maana unavuruga bajeti kuu. Na mtu aliyevurunda kabisa alikuwa Shukuru Kawambwa. Sijui kwa nini bado wanampa wizara huyu baba maana uwezo wake ni mdogo kuliko maelezo.

Sasa hivi Magufuli kajitahidi sana kurekebisha mambo (kushusha bei) lakini karithi miradi mingi mibovu na hela zilishaliwa!
 
Mwaka Jana TANROADS walikuwa wanadaiwa billion 300. Hazijalipwa.

Mwaka huu TANROADS wanadaiwa 475 billion za Barabara.

Sasa kwa nini Serikali ina kiherehere cha kulipa DOwans

Madeni karibia Trilioni moja? Hii si ni budget ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa takriban miaka 8!!

Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele.
 
Haya ndiyo matunda ya ufisadi na kukosekana kwa utawala bora na uwajibikaji. Athari mojawapo wa deni kubwa kama hilo ni kudhoofisha kwa makarandasi wazawa. Makarandasi mbalimbali wanaoidai TANROADS wanalazimika kutumia muda mwingi kusubiri malipo yao ambapo mikopo yao kutoka kwenye mabenki ikiendelea kuongezeka kutokana na riba. Matokeo yake ni kudumaza kwa uchumi na kuua moyo wa ujasiria mali.
 
Na hii wizara(TANROADS) muda mrefu hawajaajiri....mainjinia kibao mtaani wapowapo tu
 
Wote mnalalamika. Toeni solution.

Nini kifanyike?

Sitaki majibu mepesi ya wawajibike, CCM iondoke etc kwa maana experience na history zinaonyesha hata wakija NCCR au CUF watu ni wale wale watanzania watakaofanya kazi na kuiba hizo hela.
 
Lazma tukubali hakuna serikali isiyodaiwa. Cha msingi ni kuwapo na plan za kukagua uhalali wa hayo madeni na kuyalipa bila penalties ili kutowaumiza wananchi. Custodians wa kodi zetu shurti waone uchungu kidogo wajameni!

Udaiwaji wa aina hii wa serikali haukubaliki! waliingia mikataba ya ujenzi, kwamba watalipa kadiri wakarandasi watavyokua wanaendelea na kazi.

Kushindwa kutekeleza sehemu yake ya mikataba, serikali inajenga taswira ya ubabaishaji na kutoaminika,
hao wakandarasi hawakuja kuikopesha serikali, wamekuja kufanya biashara!
 
Wote mnalalamika. Toeni solution.

Nini kifanyike?

Sitaki majibu mepesi ya wawajibike, CCM iondoke etc kwa maana experience na history zinaonyesha hata wakija NCCR au CUF watu ni wale wale watanzania watakaofanya kazi na kuiba hizo hela.

Hiyo experience na historia zinazokuonyesha nI za wapi. Tanzania hatujawahi kuwa na chama kingine madarakani na tofauti na CCM.
Vunja mtandao wa mafisadi na wahujumu uchumi kwa kuiua CCM kwani ndio njia yao ya kupitia. Hakuna Fisadi au mhujumu wa uchumi asiye kuwa na kadi ya CCM.
 
Back
Top Bottom