75 ya wahojiwa wasema Kikwete sawa

Lukwangule

Senior Member
May 25, 2009
157
2

Asilimia 75 ya watanzania waliohojiwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali linajihusisha na utafiti wa masuala ya siasa, uchumi na kijamii wameonyesha kuwa wangependa Rais Jakaya Mrisho Kikwete andelelee kuongoza Tanzania mara baada ya uchaguzi Mkuu mwisho mwa mwaka huu.
Hatua hiyo inafuatia watanzania 2000 waliohojiwa kutoka sehemu mbalimbali kumkubali kuwa Rais Kikwete anastahili kuchaguliwa tena kuwa Kiongozi Mkuu wa Tanzania.
Takwimu hizo zilitolewa jana jijini Dar es salaam na Meneja wa Utafiti wa Vyombo vya Habari na Umma kutoka Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Synovate Tanzania Abdallah Gunda alipokuwa anatoa matokeo ya utafiti wa hali ya demokrasia hapa nchini.
Alisema kuwa asilimia hizo ni zaidi ya theluthi mbili ya Watanzania ambao walihojiwa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Katika utafiti huo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipata asilimia 10 wakati Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi alipata asilimia 9.
Gunda aliongeza kuwa Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) , Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na Dkt Salim Ahmed Salim walipa asilimia moja kwa kila mmoja wao ya Watanzania wenye uwezo kupiga kura wakipenda kuwa wanafaa kuwa Rais.
Meneja huyo alisema kuwa katika utafiti wao asilimia mbili ya wahoojiwa wote walisema kuwa wasingependa kueleza nani wangependa awe Rais wakati asilimia mbili nyingine hawajui wa kumchagua.
Aidha katika utafiti huo Chama cha Mapinduzi kilioneka kuwa watu wengi walio karibu nacho kwa kuapa asilimia 70, CHADEMA asilimia 17, CUF asilimia 9, NCCR-Mageuzi kuwa na asilimia 2 huku TLP na UDP zikiwa na asilimia moja kila kimoja​
 
Hivi huwa wanahoji wakina nani? Mimi sijawahi kuhojiwa na hizi tafiti kabisa halafu huwa zinazuka sana karibia ya uchaguzi je ni njia ya kampeni nayo?
 
Hahaha Makamba alishasema Jakaya ni mtaji wa CCM, kwahiyo hii ni janja ya CCM kujustfy kauli ile. Eti asilimia sabini....
Hivi kwa nini asitokee mtu yeyote humu akafanya tafiti ya ukweli (atengeneze fomu dodoso) tuweze kujua ipi mbivu na ipi mbichi? Halafu sisi wana jamii tushiriki kupitia forum hii. Pia hata wale guests wanaotembelea mtandao waruhusiwe kushiriki. Tuanze kupendekeza na maswali tunayo taka yawepo kwenye fomu dodoso hizo.
Ni pendekezo tu wajameni.
 
Back
Top Bottom