Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Naunga mkono,
Hususan kwa sababu hao wanaosemwa wanashindwa kuongoza kwa sababu hawajui kiingereza, hata Kiswahili chenyewe pia hawakijui!
Ni muhimu tukapanuka zaidi na kuangalia umuhimu wa lugha katika international relations and international development community, hasa kwa nchi kama yetu ambayo traditionally imekuwa inategemea wahisani in terms of loans, aid, trade negotiations etc; tumeshindwa kuendeleza kiswahili kufikia hatua kama kiren kwa brazil; na kati ya sababu kubwa zinazotuingiza kwenye mikataba mibovu ni ufisadi lakini pia lugha; suala la ufisadi hapa kulijadili haina haja sana kwani wengi tupo ukurasa mmoja ju ya hilo, lakini hili la lugha, kuna case studies nyingi sana ambazo zinaelezea jinsi gani viongozi wetu wanashindwa kufanikisha mambo mengi wakikutana na wenzao wa nje kwa sababu ya kutojua lugha ya kiingereza; hii haina maana kwamba lugha ya kiswahili haifai, suala la msingi hapa ni kwamba hatuitumii ipasavyo hence kutukoseshwa potential leaders in the context of the above....