50 People Who Are Screwing Up Tanzania

Status
Not open for further replies.
Please mjumuishe mwanamama anaitwa Maria Kejo. Huyu inabidi awepo kwenye top 10 ya hii list of shame. she has been involved in almost all controversial goverment contracts from IPTL to the pre-colonial type (africans take beads and whitemen take diamond) mining cotracts. She is whorishly corrupt and will sell this country to any white man with money. Please include this b-tch.
 
kama hao ndo wanainyonya au walioiweka bongo kwenye hali mbaya kwanini wasichukuliwe hatua kali.kama tunawajua na serikali ina jua lazima ifanye uchunguzi au hao ndo serikali??

Kesi ya nyani utaipeleka kwa ngedere? Umesahau ripoti ya mwakyembe na wenzake? kiko wapi? ni kiini kwenye macho! au sijui kiini macho! mi ndo sijui !!!! Hawa watu wanajuana !
Ukitaka kujua hilo angalia ya JK na BEN ? Unawezaje kumshitaki Waziri ukamwacha Bosi wake? eti kwa matumizi mabaya ya madaraka ?
 
Last edited:
Kwa haraka haraka unaweza kuwataja watu wote uliopata kuwasikia, hii inatokana misingi mibovu tuliyojiwekea wenyewe na ile tuliyorithi kutoka kwa wakoloni. Hii ina maana ni ndoto kumpata kiongozi msafi katika system iliyochafuka.

Nadhani baadhi yetu tumeanza kuona hili ndio maana kuna msukumo mkubwa wa kubadili mjadala kutoka kwa watu binafsi (zitto, rostam, lowassa n.k) kuelekea kwa maadili ya uongozi. Nimeweka jina la Zitto kwa makusudi kwani linaweza kutupatia ufumbuzi wa kitendawili hiki, tujiulize mara 100 je iwapo Zitto asingekuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge leo kuna mtu angethubutu kulitaja jina lake kwenye orodha hii? Jibu rahisi ni hapana. Sasa unaweza kupata picha tatizo sio Zitto ila ni mifumo anayoitumikia.

Iwapo tunalengo la kuleta mabadiliko ya kweli ni vyema orodha ilenge kuibua mijadala juu ya mifumo mibovu au taasisi mbovu kuliko watu binafsi ambao ni zao la mifumo hiyo.Na kwa kusema hivyo sihalalishi matendo ya watu binafsi ila najaribu kuwa makini ilikuepuka kutwanga maji kwenye kinu. Kwa kuanza kuwoki mai toki naanza ni orodha mifumo mibovu.

1. Katiba ya Jamhuri Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977(mwanakijiji alipata kueleza vizuri hii kwenye tundiko lake juu ya Iwapo Tanzania ina hitaji Stimulus package)
2. Elimu kuanzia ngazi ya chekechea hadi chuo kikuu
3. ...
4. ...
 
nimekusoma mkuu, ni kukurupuka kuandika "watanzania wote" wakati tumeanzisha mada kwa kichwa cha "watu 50". Nawaondoa watanzania kwa ujumla wao ili kuweza kuwaweka 50 wa ukweli.

Kasheshe, nia si kuchafuana, hapana. Ni vyema tukawajua maadui wa maendeleo ya taifa letu

Pia nashauri Mkuu baada ya kupata watu hao 50 tuanze elezea kila mmoja anahusika vipi kuifisadi Tz.
 
Sawa, nimekubali, na update list yangu

Mtumishi hii list ikishakamilika tutachanga fedha na kuinunulia page kwenye gazeti moja maarufu mfano mwanahalisi na kuichapa huko chini ya kichwa cha habari"kwa mtizamo wa Jamii Forum........" Hii ndahani ndiyo kitu ambayo mwanakijiji kila siku anasema tunazitumiaje habari tunazozipata humu?
 
Mkuu mbona unawaacha wakina:- Ferdinand Ruhinda, Joseph Mungai na William Lukuvi katika list yako? Hawa wanastahili kuwemo kwa kigezo chochote kile cha ufisadi!!
 
Muongeze kwenye list Lauwo wa TRA - Customs jina la pili silikumbuki...mianya yote ya kuvujisha mapato pale bandarini huyu ndiye architect wake. Hatofautiani na akina Mgonja! Nimeelezwa amestaafishwa siku za karibuni,mtaona tofauti ya kukua kwa makusanyo ya customs ( excluse effects za economic crisis na jinamizi la TICS)
 
Huyo no. 15 mbona haonekani? Nashauri ubadilishe rangi yake ifanane na wengine au kama ni kinara basi weka nyekundu
 
Ni muda mrefu sasa Tanzania imeshuhudia misukosuko mingi ya kisiasa na maadili katka uongozi wa ngazi za juu. Hii imesababishwa na watanzania kung'amua kuwa kuna watu wanatafuta uongozi katika nchi hii kwa njia yoyote ile.

Watu hawa wana fedha nyingi walizopata isivyo halali na wanatumia kujisafisha kwa njia mbalimbali. Watu hawa ni Rostam Aziz,Edward Lowassa na Hendry Chenge.

Ninavyoona mimi watu hawa wasipodhibitiwa wasababisha machafuko katika nchi hii kwani wana fedha nyingi haramu wanazoweza hata kuanzishia jeshi.

Watu hawa ndio walionyuma ya kuchafuana na hujuma mbalimbali hapa nchi, sijafanya utafiti wa kina lakini kabla ya kunipinga ifanya utafiti kuhusu watu hawa.

Na kama JK anataka nchi hii iwe salama awadhibiti watu hawa kwa kutaifisha fedha walizonazo zisizohalali.

Nawasilisha.
 
Mkuu Chenge's first name ni Andrew, unaweza ukajikuta umemaanisha mtu mwingine ni taarifa tuu Ndugu.
 
Nakuunga mkono ndugu yangu. Watu hawa ni hatari kupita kiasi. Ni matumainin yangu kuwa JK analitambua hili. Lakini mtu hatari zaidi ni Rostam Aziz, Mburushi huyu anayetamba kuwa ndiye aliyemuweka JK madarakani. Sasa anapigana kufa na kupona ili ampachike Mkuu wa Mafisadi, Edward Lowassa eti ili awe rais baada ya JK. Huku ni kuwatukana Watanzania!
 
Hao hawamuwezi Kikwete hata dakika moja, Kikwete ni mtu mkimya sana sana ,na hatari ya mtu mkimya ni kubwa kuliko yule anaepiga makelele,maana mtu mkimya anakuwa alert kwa kila step anayochukua,japo ataonekana hajui au mtamuona zezeta lakini hesabu zake haziendi upande, anapanga ,anayajua, na kuelewa ni wakati gani anahitaji kuchukua hatua ili kuidhibiti hali.

Hivyo hao akina Rostam na wengine inakuwa kama wadudu waliokuwemo ndani ya sufuria kubwa ,hivyo Kikwete aliepo juu anawaona na kuwatazama movement zao na nani anataka kutoka kwenye sufuria atamuona tena kwa urahisi zaidi ,natumai umepata picha halisi ,hivyo Kikwete anayatazama haya yanayofanywa kwa upole kabisa akiamini watu watajirekebisha intime kabla hajaamua kuwarudisha ndani ya sufuria kwa yule anaekuja juu akiamua kutaka kutoka ndani ya sufuria ,kwa ufupi hawa watu wamewekwa ndani ya kona au uangalizi na kila hatua wanayofanya inadhibitiwa na kupimwa kwa kina na malengo yake,kiasi kwa walipo wanaonekana wamo katika kugombea ukubwa wao kwa wao,hivyo Kikwete analielewa hilo ,na wao kama ndugu lazima mkubwa amuheshimu mdogo ,sasa wanapotokea ndugu kupigana inabidi uwawache ili mmoja aweze kumuheshimu mwenziwe.

Kikwete ni Raisi ambae amekuwa mvumilivu sana kiasi kuwa uvumilivu wake unaonekana kuwa umepita mipaka ,lakini anaamini kuwa kila mtu atauona ukweli wa anayoyafanya na atajirekebisha hivyo tunaweza kumuweka katika kundi la watu wenye subira.Na ndivyo nimuonavyo mimi kwa upande wangu ,ni mtu ambae anaweza kukasirika mpaka akabadilika rangi lakini mwisho wake hurudisha hasira zake na kuwa katika uvumilivu na ndio tunavyokwenda nae he is a man of GOD & we can do nothing to force him to take action by our makelele.

Hata Mtume wetu Muhammad alikuwa mpole sana kuna sehemu alipigwa mawe na yakamtoa ngeu na damu,malaika alimshukia na kumwambia sema tuwafanye nini wale watu ,Mtume akawaombea dua tu na hakuwatakia waadhibiwe.

Hivyo wavumilivu ni watu wa aina hawawezi kabisa kufuata matakwa ya mtu mwengine katika kuchukua hatua.
 
Mnajua huyu lowassa alikuwa anataka urais 2015,ila mungu mkubwa maana nchi ingeuzwa,c mchezo jamaa ni mtu wa mabisness na anapata desa kutoka kwa professional aliyetunyonya toka ukoloni.
Hawa jamaa ndo wanatuletea matatizo nchini,wana mitandao yao ya kuichafua serikali na kujisafisha wenyewe.
Naamini kikwete analitambua hili hata zaidi yetu.Hivyo atawadhibiti vya kutosha tu.Mimi ningefurahi kama hizi sura zicngerudi 2010,Walau tuwe na sura mpya za wabunge na hapo ndo tutaacha kufanya kazi kwa mazoea.
 
Most of the time watu wenye hela tend to do anything...kama Cheney si huyo saa hizi anaanza kuleta mtafaruki kwa kuanza kuongea kuwa marekani itavamiwa soon....inamaana anatumia pesa yake kuvuruga watu akili....na kuna wengine wana pesa lakini utakuta wapo mstari wa mbele kusadia nchi kama warren buffet,bill gate just to name few....Ila kwa afrika mmh!...na ukizingatia tanzania hatujawahi kupatwa na misukosuko once ikitokea basi itakuwa kasheshe sijui tutakimbilia wapi...

inabidi tuu watu tusali ili mambo yaliyotokea kwenye nchizetu xa jirani yasitokee Tanzania......
 
Ni muda mrefu sasa Tanzania imeshuhudia misukosuko mingi ya kisiasa na maadili katka uongozi wa ngazi za juu.Hii imesababishwa na watanzania kung'amua kuwa kuna watu wanatafuta uongozi katika nchi hii kwa njia yoyote ile.Watu hawa wana fedha nyingi walizopata isivyo halali na wanatumia kujisafisha kwa njia mbalimbali.Watu hawa ni Rostam Aziz,Edward Lowassa na Hendry Chenge.Ninavyoona mimi watu hawa wasipodhibitiwa wasababisha machafuko katika nchi hii kwani wana fedha nyingi haramu wanazoweza hata kuanzishia jeshi.Watu hawa ndio walionyuma ya kuchafuana na hujuma mbalimbali hapa nchi,sijafanya utafiti wa kina lakini kabla ya kunipinga ifanya utafiti kuhusu watu hawa.Na kama JK anataka nchi hii iwe salama awadhibiti watu hawa kwa kutaifisha fedha walizonazo zisizohalali.Nawasilisha.

Usiwe na jazba unaushahidi wowote wa kubainisha hilo au ni chuki tu hao watu sioni kama wanamakosa hadi sasa. hivi tuseme iwe ni wewe ndio umeona hilo vyombo vya dola halioni hicho kitu na kama ingekuwa hali ipo hivyo ulivyo isema basi sidhani kama serekali ingewachia watu hao wa 3 wafanye hayo wakati serekali inauwezo wa kuwashuhulikia na sifikiri serekali ingekubali nchi kuchafuliwa lakini kwa hali inavyokwenda nahisi hata serekali inajuwa kuwa hao watu wanazuliwa tu
 
Mkuu mbona unawaacha wakina:- Ferdinand Ruhinda, Joseph Mungai na William Lukuvi katika list yako? Hawa wanastahili kuwemo kwa kigezo chochote kile cha ufisadi!!

ufisadi wa ngono ???je
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom