50 Greatest Tanzanians (minus politicians)

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Kusherekea 50 years naomba mtuletee list ya 50 greatest Tanzanians (tukimtoa Nyerere na wanasiasa ambao tushawajadili sana)

Itakuwa si vibaya mkatuletea na sababu why these unsung heroes are great

Si lazma mje na list ya majina 50 lakini muhimu ni kutuambia kwa nini hawa watu japo hawaenziwi na watawala wetu lakini muhimu kuwajaua na michango yao kwenye historia ya Tanzania.

Personally nitaanza na Mashado Plantan ambaye nilikuwa simjui mpaka member mmoja humu alipoingia na jina lake na nikatafuta wasifu wake. Mashado was the original INVISIBLE wa enzi zake kwani alikuwa ni Mwafrika Mtanzania wa kwanza kuanzisha Gazeti lake lilikuwa linaitwa ZUHURA in the 1950's !

Muhimu wawe wanatoka from all walks of life kasoro wanasiasa.

we might learn a thing or two
 
mbona Mashado Plantan alikuwa ni mwanasiasa? nilidhani umesema wasio wanasiasa.
 
Mzee Mwanakijiji

Kwa uzalendo wake, kwa uanaharakati wake, kwa uhamasishaji wake, na kwa kujitolea kwake kwa taifa lake katika kuongoza mapambano ya kifikra. Mzee Mwanakijiji hana lazima au haja ya kufanya yote hayo ayafanyayo. Anaweza kabisa kujikalia kimya na tuli kama maji mtungini na akala mbatata na bata wa kila aina.

Huyu mzee ana msukumo wa ajabu. Hajui kuchoka wala kukata tamaa. Neno kuogopa (uoga) halipo katika msamiati wake. Hakika Mzee Mwanakijiji anastahili kuwemo katika orodha ya Watanzania 50 walio mashuhuri.

Mzee Mwanakijiji is a great Tanzanian!
 
ndugu yangu hunipendi.. duh!

Ila hili zoezi gumu kwa kweli. Labda mtoa mada angetupa japo vigezo vya kuangalia siyo vya kutoangalia.
 
Maxence Melo and co, for starting this great blog ambayo inatambulika na kuogopwa pia na serikali iliyojo madakani.

JF imekuea kisima cha habari na chachu ya mabadiliko katika nchi nzima. I'm almost sure waanzilishi na wamiliki wa JF wanapata vitisho na technical subbotage za hapa na pale for standing up for what they believed in, big up!
 
Mzee Mwanakijiji

Kwa uzalendo wake, kwa uanaharakati wake, kwa uhamasishaji wake, na kwa kujitolea kwake kwa taifa lake katika kuongoza mapambano ya kifikra. Mzee Mwanakijiji hana lazima au haja ya kufanya yote hayo ayafanyayo. Anaweza kabisa kujikalia kimya na tuli kama maji mtungini na akala mbatata na bata wa kila aina.

Huyu mzee ana msukumo wa ajabu. Hajui kuchoka wala kukata tamaa. Neno kuogopa (uoga) halipo katika msamiati wake. Hakika Mzee Mwanakijiji anastahili kuwemo katika orodha ya Watanzania 50 walio mashuhuri.

Mzee Mwanakijiji is a great Tanzanian!

A brilliant!!! Mwanakijiji!!
 
1. Brigedia Bayeke aliyekwenda kuwashikisha adabu washenzi waliokuwa wanabaka dada zetu mikoa ya magharibi. KUna watu wana madaraka ya juu na vyeo vya juu hawajali, tena wanashiriki kufanya kama yale aliyopingana nayo Bayeke.
2. Jenerali Ulimwengu, aliyekwenda kwenye mission ya hatari Msumbiji akiwa kijana mdogo, kutokana na moyo wa uazalendo kwa nchi yake, na moyo wa kupigania uhuru wa mwafrika...malipo yake aliambiwa kuwa si mtanzania
3. Issa Shivji
4. kuna dada mmoja mwanasayansi amepata tuzo pale muhimbili hivi karibuni
 
Mods naomba comment za kipuuzi puuzi mzifute (hata ikibidi yangu)
Ili zibaki zile tu zinazo elezea watu maarufu walio shiriki katika kupigania na
kuiendeleza nchi yetu.

Am very young,nahitaji kuwafahamu na naamini sio mimi peke yangu
maana wengi wanataka kujifunza,....
Kuna watu wana tafuta umaarufu humu kwa kupost uchafu uchafu tu kila sehemu.
 
Marehemu Stan Katabalo,mwandishi wa gazeti la Mfanyakazi alikufa katika mazingira kiutata mara tu alipofichua kashfa ya Loliondo..

Mzee Sabodo kwa kuvunja kongwa la uoga katika kusupport demokrasia ya nchi hii. Kitendo chake cha kuchangia CDM ilhali yeye ni CCM. Hii imenipa kuamini kuwa hata biashara anazofanya ni safi, zingekuwa zimepinda kama za wenzake kina Subhash Patel & asingethubutu.
 
1. Kardinali Rugambwa (kardinali wa kwanza mwafrika).
2. Rashid Matumla (bingwa wa dunia ngumi WBO).
3. David Msuguri (kiongozi wa vita vya kagera na kufanya Tz kuwa nchi pekee Afrika kupigana na nchi nyingine na kushinda).
3. MM Mwanakijiji (mwanaharakati wa demokrasia na maendeleo asiyeogopa wala kuchoka).
4. Mbaraka Mwishehe,Marijani Rajabu,Tx Moshi na Banza stone (hawa walileta mapinduzi makubwa ya muziki nyakati zao).
 
Tundu Antipas Mugwai Lissu-shujaa na mtetezi mkuu wa watu wanaoishi maeneo ya mgodi aliyeanika uovu wa fukiafukia ya Bulyanhulu. Amekamatwa na kufungwa na kuwekwa korokoroni mara kadhaa kutetea wanyonge hao.

Ametumia taaluma yake ya sheria kutetea waathirika wa migodini huko mahakamani ingawa kwa sasa ni mwanasiasa lakini kwa makubwa aliyofanya kutetea wanyonge anastahili kuwa shujaa wa wanyonge Tanzania.
 
Mwingine ni General Kombe kama sijakosea alikuwa ni mtu wa usalama wa taifa na mwanajeshi mstaafu walimuua kimazabe wkt akienda Arusha japo alishuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kuwa amejisalimisha. Kisa alikuwa na siri nyingi za nchi na wakahofia anawapa wapinzani huku akiwa ktk mpango wa kuingia ktk siasa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom