29 watinga Kizimba cha Kisutu kwa tuhuma za kuchoma Makanisa Mbagala

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Watuhumiwawa vurugu za Mbagala wiki iliyopita, wakiwa chini ya ulinziwa polisi,
walipofikishwa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa
mara ya kwanza jana. Watuhumiwa 29, wawili kati yao wanawake, walisomewa
mashtaka mbalimbali kuhusiana na vurugu zilizopelekea makanisa kadhaa
kuchomwa moto wiki iliyopita, chanzo ikiwa ni baadhi ya watu wanaodaiwa
kuwa waislamu, kuandamana wakipinga mtoto mmoja kukojolea Quraan tukufu.
Dhamana ya watu hao itaamuliwa Oktoba 30.
btwelve.jpg

Baadhi ya watuhumiwa wa vurugu zilizotokea Mbagala jijini Dar es Salaam wiki iliyoipita, wakiwa ndani ya gari la polisi walipofikishwa mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Oktoba 16, 2012 kwa mara ya kwanza. Watuhumiwa 29, wawili kati yao wanawake, walisomewa mashtaka mbalimbali kuhusiana na vurugu zilizopelekea makanisa kadhaa kuchomwa moto wiki iliyopita, chanzo ikiwa ni baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waislamu, kuandamana wakipinga mtoto mmoja kukojolea Quraan tukufu. Dhamana ya watu hao itaamuliwa Oktoba 30.
waw.jpg
Akina mama wanaotuhumiwa kuhusika na vurugu zilizotokea huko Mbagala,
wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita, wakishuka kutoka
ndani ya gari la polisi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam jana. Akina mama hao ni miongoni mwa watuhumiwa 29
waliofikishwa kwenye mahakama hiyo kujibu mashtaka ya kuhusika na vurugu za kuvamia makanisa, kuchoma, kuharibu mali na kuiba.

Polisi aliyejihami kwa bunduki na radio ya mawasiliano, akishika doria kwenye lango la kuingilia chumba cha mahakama ambako watu 29 walifikishwa mahakamani hapo Jumanne Oktoba 16, 2012, wakikabiliwa na mashtaka kadhaa ya kuvamia makanisa, kuharibu, kuiba na kuchoma mali za makanisa hayo wiki iliyopita huko Mbagala jijini Dar es Salaam. Wote wamerejeshwa mahabusu hadi Oktoba 30 ambapo mahakimu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo, wameahidi kutoa uamuzi juu ya hatma ya dhamana.

Source: K-VIS BLOG
 

Hawa Wananchi wengine hata walikuwa hawajua wafanyacho; Walikuwa Wanafuata Mkumbo
 
Madhara ya kusikiliza radio imaan na kina ponda wenzao saaafi wapo tu wanaendelea kubwabwaja
 
Duu polisi ya TZ deal mbona naona polisi wote hao wameshiba au wamewachagua walioshibashiba wote?
 
Mbona sioni hata Sheikh mmoja? au hawa ndio wenye uchungu sana na kitabu hadi kimewapa ukichaa wa kuchukua Generator za kanisa, power window za magari yaliyokuwepo kanisani Sadaka na nguo za wachungaji...

Hii kesi sijaelewa ni ya fujo,dini au wizi? ,wishowe tutakuja sikia jamaa wote waligeuka vichaa kwa wakati ule wa tukio tu ndipo wakafanya hayo matukio...

Makanisa kumi hawa jamaa ni wa kulipiziwa kisasi na wao wasali kwenye mavumbi kama wenzao...

Kisasi kisasi ndio msemo mpya...
 
mbona yule mama aliyekuwa analia lia siku ile kwenye ITV hakukamatwa? Wamtafute yule inawezekana ndiye aliyeiba sadaka
 

Hawa Wananchi wengine hata walikuwa hawajua wafanyacho; Walikuwa Wanafuata

Mkumbo

Ndiyo wajue faida za bendera hufuata upepo! Labda walikuwa na lingine zaidi ya hilo!

Wahamasishaji wa shughuli nzima wapo wapi? Walitokea msikiti upi? Yote hii ni uwezo duni wa kutafakari na kutatua matatizo, utafikiri wendawazimu!
 
mbona yule mama aliyekuwa analia lia siku ile kwenye ITV hakukamatwa? Wamtafute yule inawezekana ndiye aliyeiba sadaka
..... yule wamsamehe tu, kama si huyo nayeona ndani ya baibui! pale tu, alionekana kuwa mwehu! kuna haja gani ya kumshtaki mwehu?
 
hawa ni wahuni tu si waislam ngoja tuone majina yao utakuta mchanganyiko. They just took advantage of the circumstance to loot. They are looters
 

Hawa Wananchi wengine hata walikuwa hawajua wafanyacho; Walikuwa Wanafuata Mkumbo


Kila siku huwa nasema sikubali kutumika hata kama mimi ni muislam!!
Waliopanga wamelipwa sasa waliotumika kukiona cha moto! ujinga mtupu
 
Back
Top Bottom