29 watimuliwa TANESCO

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Wanajamvi taarifa nilizozipata hivi punde toka kwa kiongozi mmoja wa juu wa Tanesko nikuwa wafanyakazi 29 wa shirika la umeme Tanesko wamefukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani hi leo,hawa ni wale waliotengeneza mgao feki wa umeme na kulihujumu shirika hilo.

UPDATE:

Imedhibitishwa kuwa ni kweli,na nimpango mahususi wa kuwazaba midomo wapinzani kufuatia operetion mbalimbali zinazoendelea nchini. Mtoa taarifa pia anasema hi inatokana na hali kuwa mbaya katika chaguzi zinazoendelea ndani ya chama Tawala.kwani hali imendelea kuwa mbaya kwa baadhi ya makundi ya wanaotaka UKIRANJA MKUU kwani baadhi ya makudi yanahusika mojakwamoja na hujumahii hivyo wanapata wakati mgumu wa kutetea nafasi zao ndani ya chama na hivyo kuamua kuwatoa kafara walio chini yao kwa maslahi ya wakubwa ili kuuhadaa uma wa Watanzania kuwa hawahusiki na wizi huo. ( nakuhakikishia hali ni mbaya sana huko juu,mambo hayaendi kabisa wakubwa wanakimbizana kutetea nafasi zao si mchezo kila kambi inajiimarisha inavyoweza na kila mbunu itatmika nakuhakikishia.)mwisho wa kumnukuu.
 
kesi zinaenda mahakamani lakini jibu halipatikani wamefanywa nini, ni sawa na tume, ikiundwa tunatangaziwa mwisho wa tume jibu kapuni
 
Kweli hizi kesi hazina manufaa. Bora wangetimuliwa waende home tu wakapumzike.

Lakini wengine humu wangelalamika why hawajapelekewa mahakamani!
 
Watimuliwe kazi tuu kesi kwa Tz ya sasa ni useless mnawafanya mahakimu wawe busy unneccessarily
 
Kwanini mtuhumiwa namba moja asiwe waziri wa nishati wa kipindi hicho cha mgao.Wafanyakazi hao walipata wapi mamlaka ya kuanzisha mgao.
 
Sikumbuki serikali ama mashirika ya umma kushinda hizi kesi za kuwatimua kazi wafanyakazi wake.
 
Kuwatimua bila ya kuwafungulia mashtaka bado hakuwazuii hao wafanyakazi kufungua kesi za kupingwa kufukuzwa kazi.
 
Ninawasiwasi tena hili nitaweza changa la macho Katika kuwatoa baadhi kafara ili kumaliza tuhuma za wakuu wetu.
 
Hivi wakuu mnaamini hizi tambo kwamba mgawo umeisha? Kwa mitambo ipi ya umeme? Haya majenereta ya emergency yanayotukamua watumiaji?
 
Je kweli hiyo list kuna dada yetu Badra Masoud? maana kuna Kaka siki hizi ana kaimu nafasi yake
 
Sikumbuki serikali ama mashirika ya umma kushinda hizi kesi za kuwatimua kazi wafanyakazi wake.

After 3/4 years, kesi hizi hugeuka kuwa dili kubwa kwa mahakimu!! Jamaa hushinda na kulipwa kimya kimya Nchi ikabaki na maumivu makubwa.
 
list hiyo iko wapi mkuu tunahitaji kujua watu waliomo ili tuweze kupata habari kamli
 
Inawezekana kabisa hao wakawa walikuwa wanatumiwa na chadema, kweli siasa za nchi hii ni za kipumbavu.



Note;we all know, hata JK angefanya zuri gani sio tu kwamba msingelisifia lakini msingelipenda kabasi hata kutokea kwake
 
Wanajamvi taarifa nilizozipata hivi punde toka kwa kiongozi mmoja wa juu wa Tanesko nikuwa wafanyakazi 29 wa shirika la umeme Tanesko wamefukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani hi leo,hawa ni wale waliotengeneza mgao feki wa umeme na kulihujumu shirika hilo.

UPDATE:

Imedhibitishwa kuwa ni kweli,na nimpango mahususi wa kuwazaba midomo wapinzani kufuatia operetion mbalimbali zinazoendelea nchini. Mtoa taarifa pia anasema hi inatokana na hali kuwa mbaya katika chaguzi zinazoendelea ndani ya chama Tawala.kwani hali imendelea kuwa mbaya kwa baadhi ya makundi ya wanaotaka UKIRANJA MKUU kwani baadhi ya makudi yanahusika mojakwamoja na hujumahii hivyo wanapata wakati mgumu wa kutetea nafasi zao ndani ya chama na hivyo kuamua kuwatoa kafara walio chini yao kwa maslahi ya wakubwa ili kuuhadaa uma wa Watanzania kuwa hawahusiki na wizi huo. ( nakuhakikishia hali ni mbaya sana huko juu,mambo hayaendi kabisa wakubwa wanakimbizana kutetea nafasi zao si mchezo kila kambi inajiimarisha inavyoweza na kila mbunu itatmika nakuhakikishia.)mwisho wa kumnukuu
.
hiyo update ni ya habari hii hii au?
 
Back
Top Bottom