2030: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki

huyo waziri wa utamaduni hana mamlaka ya kuifungia ngoma ya Roma msanii msomi anyejua ni nini maana ya sanaa' Safi sana Roma mtoto wa mkulima zidi kuandika vitu vya maana kama hivyo. Wimbo nimeusikia na niimeununua kwa buku tatu tu. Fanyeni hivy dogs kwani ndivyo tunavyotambulika na hao walioimbwa na roma.

Onyo________kwa yoyote atakaye sababisha ngoma ya Roma kusambaa kwenye internet atachukuliwa hatua za kinizamu. Na si vizuri kununua na kuanza kugawa hiyo itasababisha The Great Educated hip pop mc kutopata mahela mengi kama zilivyo ndoto zake kwenye hiyo truck ya ROMA2030.

Ni hayo tu SINA MENGI SANA'
 
Roma ajawai kutoa ngoma mpya,sijaona kipya kabisa hapo,ukisikiliza tangia anatoka hadi sasa anaimba kitu kilekile na flow ni ileile ya makelele..zaidi ni muendelezo wa kutumia majina ya watu maharufu kuyataja negatively ili apate atenshen...labda kipya ni kawachana waislam which is so bad.

Mkuu unless masikio yangu yanadanganya au redio yangu inachuja ni wapi kawachana waislamu ? au wewe ndio unataka kubadilisha maana
 
SERIOUS NOTE: Nimesikiliza, loooh, kuna maneno mazito!!! Ila mambo ya imani / dini yasingekuwemo, mbona ni wimbo mzuri.
Inalaani ufisadi, ubadhirifu, wizi, uzinzi etc. Kama mengine yanayosemwa humo yanasitua!!!

WITH A LIGHT TOUCH: Wimbo huu unatafaa kuutumia katika jitihada za kugombea ubunge/uraisi mwaka 2015, unakuwa unaupiga pale mwanzo, unahutubia, halafu unaupiga pale katikati, unahutubia, na unahitimisha tena kwa wimbo huu!!!
 
Heshima Mbele.

Happy New Year Kwenu Nyote.

Nasema Wenye vichwa vyepesi wataichukulia nyimbo kiuwepesi, watajadili Beat, Rhyme na Length. Watajadili wasifu binafsi wa alieimba (Roma), wataingiza Siasa pia.

Tutasahau lengo haswa la Msanii, mistari iliopo kwa hii nyimbo ndio lengo na ni msaada sana kwetu.

Naomba kuzungumzia mistari michache tu mingine mtaijadili binafsi.


1. "Tenda wanapeana kindugu, mwanangu kua uyaone"

Wengi wetu sisi ni watu wazima, tumeshakuwa lakini bado baadhi yetu hatujayaona. Hatujayaona labda kwa kuwa tumelelewa kitajiri sana na kwa connections au labda tumelelewa kimaskini sana na kiuoga hatuthubutu kuhoji. Hatujui thamani ya maisha yetu endapo Gold na Tanzanite zisingetoka kinyemela. Au Wanyama wetu wangeuzwa kihalali, Kodi zingelipwa on time na kwa halali etc. Kama hatujui haya wala hatujui tofauti ya Mtanzania na Msomali kirasilimali.

2. "Tazama Gongolamboto mtoto kamzaa mtoto na atalelewa na nani baba ake mmefunga keko"

Katika hali ya kawaida huwa serikali inakimbilia kumfunga mwanaume kama amejamiana na under age, ni kosa kweli na alistahili adhabu. Lakini je mmeshawahi jiuliza, yule mtoto atalelewa na nani?? Atamfahamu Baba? Je Baba akiwa Hai mpaka siku ya kutoka atakuaje?? Ataendeshaje maisha yake binafsi na ya mtoto au family?? Si ni majukumu million lazima a-opt shortcut (mbaya zaidi ya kuzaa na underage).
Kwanini tusingejiuliza na role ya mtoto wa kike hapo??
Kwanini tusingedisegn more fruitful penalty?? Community service inayozalisha both ways, kwa mtuhumiwa na serikali.
Kwanini elimu isitolewe (ya kweli sio hii wanayohubiri) kwa vijana wajue nini madhara ya kuzaa utotoni.. Msiseme haiwezekani angalieni mataifa mengine.

Hizi ni Punch mbili tu ziko miiingi zenye ujumbe mkubwa zaidi kila angle.


Hip Hop ni tamaduni, usiangalie flow kwenye hili angalia ujumbe na wakati tuliomo.

Asante Roma, 2030 ni Bonge la Nyimbo. Tunashukuru kukubali iweke Hulkshare.


Udini Wa Ma-Presenter, Sisi Wapagani Unatuumiza.
 
Ni ya kawaida sana nimeisikiliza mara nyingi, nadhan karopoka and is so direct sanaa haiko ivyo..hakuna jipya hapo.
 
Alieleta uzi huu nahisi ni Roma mwenyewe,anataka kupima upepo humu ndani tumeipokeaje ngoma yake.kifupi ni hivi, mistari mepesi saaanaaa,ukimya wake muda mrefu sikutegemea kama angerudi hivi.JIPaNgE TeNa
 
watumwa wa wakoloni utawajua tu. wimbo mzuri. je wimbo wa msanii gani wa bongo unao uona bora kuliko wimbo wa toma unao itwa 2030?. mia

Kasikilize Miss Tanzania na Homa ya dunia za Solo Thang ndo utaelewa mkuu sixgates alikuwa anamaanisha kitu gani.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
dah nimeisikiliza zaidi ya mara mbili nnachoweza kusema kwa sasa kwanza kimistari bado hajapoteza kuna lyrics kali ndani yake zenye ujumbe wa kutosha ila beats kama vile imepooza sana tofauti na mathematics na baadhi ya ngoma zake zilizotangulia kingine jamaa anibidi abadilike kidogo mbona flow ile ile
 
Back
Top Bottom