2030: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki

Mi naona Roma alicho imba ni ukweli mtupu ila magamba lazima yatasema ni uchochezi!...
Big up Roma tunapenda kuwasikia wanamuziki kama nyie haya uliyo imba yote ni mambo yaliyotokea kwenye jamii sasa huo uchochezi uko wapi???...
 
Zito akiroga na kubeba tunguri kasulu cc tunaroga Pangani (My take Roma katumiwa na kundi linalompinga Zitto)
 
Kwangu wasanii wa mziki halisi Tanzania ni
1) Afande Sele
2) Sugu
3) Roma
4) Jeydee

Wengine wote ni wabana pua tu

Hivi wapi naweza kupata hizi nyimbo za Sugu:

  1. Tukikubali au Tukikataa, Ni Hali Halisi
  2. Niko Mikononi mwa Polisi
  3. Mchakamchaka

Na pia nauhitaji wimbo wa Soggy Doggy Hunter unaoitwa “Nimchague Nani ……..Awe Kiongozi wa Jamii”
 
Inauzwa elfu tatu tu za kitanzania. Huu ni mfumo aliyokuja nayo msanii R.O.M.A. Kwa maelezo ya kununua ingia hapa www.bongoflavortz.com/2012/12/nyimbo-mpya-ya-roma-yauzwa-buku-3.html?m=1
nimetafuta link nimekutana na intro full track nitaipata vipi?
 
Hii ni vita ya Msambaa, Mbondei usitie maguu
Ona kipindi cha bunge Dodoma inanuka ngono
Spika akiahirisha bunge, wengi watausapoti mgomo
Wabunge mnadai posho ili mhonge dada zetu

Leo Ridhiwani hafanani na Makongoro
Nchi imejaa misitu, tuna uhaba wa madawati
RPC usitume kikosi ili uishushe CHADEMA
Muhimbili naumwa goti, eti dokta kapasua kichwa
Uchafu wa Mrisho unamfanya msafi aonekane Benja
Watanzania tuna uoga, sio amani mnadanganywa

Sikiliza track yake hii hapa:

https://soundcloud.com/millard-ayo/www-millardayo-com-roma
 
mtoto wa kitanga he has done it again! mistari imesimama aiseee!!! ...

Amegusa pande zoteee aiseee! nita download wapi hii...?
 
Wasanii wote wangeimba facts kama hizi, sanaa ingekua silaha tosha sana katika harakati za ukombozi. Salute kwako Roma
 
Big up Roma .naomba ukagombee ubunge kule bumbuli kwa februari marope,

ili iweje sasa?jamaa ameamua kuitumikia jamii kwa muziki,hivi unadhan kwenda bungen ndo kuwatumikia wananchi?msanii ana nafas kubwa ya kuwasaidia wanajamii kuliko MP anaweza akawa na foundation n.k,we umekazania bunge tu lol
 
Yaani mistari yote hujaona ila iliyomgusa Zitto ndo ukakurupuka.Mimi nakwambia na anayekojolea msahafu hajui kanisa
 
Roma ajawai kutoa ngoma mpya,sijaona kipya kabisa hapo,ukisikiliza tangia anatoka hadi sasa anaimba kitu kilekile na flow ni ileile ya makelele..zaidi ni muendelezo wa kutumia majina ya watu maharufu kuyataja negatively ili apate atenshen...labda kipya ni kawachana waislam which is so bad.
 
Huu wimbo si unauzwa Buku 3? Mbona kauachia watu wasikilize free? Huu wimbo hauna tofauti na mathematics..
 
roma asichelewe kutoa video ya huu wimbo,bonge la ideas hasa yule mtoto analivyoimba chorus
 
Back
Top Bottom