2030: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki

Kwangu wasanii wa mziki halisi Tanzania ni
1) Afande Sele
2) Sugu
3) Roma
4) Jeydee

Wengine wote ni wabana pua tu
 
baadhi tu ya mistari iliyomo
kipindi cha bungeni dodoma inanuka ngono,
spika akiairisha bunge wabunge wanashabikia mgomo
wanadai nyongeza ya posho ili wahonge dada zetu
kuna watoto wa mama salma chuoni usicheze peku
RPC usitume kikosi chadema wakiandamana
utalipa damu ya mwangosi iringa semeni amina
leo ridhiwani hafanani na makongoro....

ngoma ni kali balaa
 
Wimbo mpya wa HIP POP Kutoka kwa Msanii Roma Mkatoliki unaotamba kwa sasa katika anga la muziki Tanzania ukiwa una siku tatu tu tangu uachiwe hewani. wimbo huo unaonekana unaleta hisia kali za uasi na mapinduzi kwa vijana kutokana na mashairi yake yanayogusa mambo mazito yaliyolikumba taifa kama.

1. Kipigo cha Ulimboka ( kuna mstari unasema Damu ya Ulimboka iwe chachu ya Ukombozi kwa TZ)

2. Mauaji ya Mwandishi wa Habari Mwangosi kule iringa

3. Zitto na .......... Kasulu na Roma na Watanga kuwanga Pangani

4. Ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya Umma

5. Uamsho na vurugu za kidini

6. Ukabila na Ukanda

7. Kiitikio chake sasa yaani ( Chorus) inaizalilisha kabisa Serikali iliyopo madarakani kwani inasauti ya mtoto akilalamika kuhusu Tanzania yake inavyoharibika

8. Mnyukuano wa kisiasa unaondelea hivi sasa nchini nao ndani ya mistari

9. Na mambo yote unayoyafahamu yanayochochea uasi na vurugu kwa Rika la vijana yamezungumziwa katika wimbo huo wenye takribani dk 8 mnaweza ongezea hapo chini....

Kutokana na maudhui ya wimbo huo kuwa kisiasa zaidi inawezekana kabisa serikali sikivu na inayopenda amani kupitia waziri wa Habari na utamaduni kuufungia(Kuupiga BAN) wimbo huo kuendelea kusikika katika masikio ya watanzania kuepusha uasi, vurugu na uvunjifu wa amani unaoweza kutokea kutokana na mashairi ya wimbo huo unaitwa 2030.
 
Unajua maana ya sanaa? kazi kubwa ya sanaa ni kuelimisha na kuburudisha, Rose Mhando aliimba ACHIA haukupigwa ban tumesikia nyimbo nyingi za Mpoto hazikupigwa ban. inatakiwa twende na wakati mi naona wewe ndo unayeleta uchochezi juu ya wimbo huu, yote yanayoongelewa kwenye wimbo huo hakuna Mtanzania mwenye akili timamu ambaye hajui hayo na bado yamo kwenye mioyo ya watanzania na hayatafutika hadi hapo CCM itakapoondoka madarakani na wahusika wote kuchukuliwa Hatua na serikali Sikivu na itakayokuwa na uchungu na watanzania na rasilimali zake.
 
Wimbo mpya wa HIP POP Kutoka kwa Msanii Roma Mkatoliki unaotamba kwa sasa katika anga la muziki Tanzania ukiwa una siku tatu tu tangu uachiwe hewani. wimbo huo unaonekana unaleta hisia kali za uasi na mapinduzi kwa vijana kutokana na mashairi yake yanayogusa mambo mazito yaliyolikumba taifa kama.

1. Kipigo cha Ulimboka ( kuna mstari unasema Damu ya Ulimboka iwe chachu ya Ukombozi kwa TZ)

2. Mauaji ya Mwandishi wa Habari Mwangosi kule iringa

3. Zitto na .......... Kasulu na Roma na Watanga kuwanga Pangani

4. Ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya Umma

5. Uamsho na vurugu za kidini

6. Ukabila na Ukanda

7. Kiitikio chake sasa yaani ( Chorus) inaizalilisha kabisa Serikali iliyopo madarakani kwani inasauti ya mtoto akilalamika kuhusu Tanzania yake inavyoharibika

8. Mnyukuano wa kisiasa unaondelea hivi sasa nchini nao ndani ya mistari

9. Na mambo yote unayoyafahamu yanayochochea uasi na vurugu kwa Rika la vijana yamezungumziwa katika wimbo huo wenye takribani dk 8 mnaweza ongezea hapo chini....

Kutokana na maudhui ya wimbo huo kuwa kisiasa zaidi inawezekana kabisa serikali sikivu na inayopenda amani kupitia waziri wa Habari na utamaduni kuufungia(Kuupiga BAN) wimbo huo kuendelea kusikika katika masikio ya watanzania kuepusha uasi, vurugu na uvunjifu wa amani unaoweza kutokea kutokana na mashairi ya wimbo huo unaitwa 2030.
Nilifikiri umepigwa BAN kumbe umekuja kuleta umbea wa kuuchongea?! Poor you.
 
Bila shaka vyombo vya habari kama TBCCM na Clouds (Not sure) hawawezi kuupiga huu wimbo!
 
Mleta mada sijajua umeanza lini muziki wa harakati. Nimeusikia wimbo mzima wa Roma, version zote mbili, sijaona alipoongea uchochezi. Zote ni facts tupu za kilichotokea mwaka huu. Kwamba Ulimboka alitekwa ni uchochezi? Kwamba Mwangosi aliuawa na polisi ni uongo? Usiisemee serikali, ina wasemaji wake akina Billy Lukuvi. Joseph Haule, Sugu (Mikononi mwa Polisi) , Wagosi wa Kaya (Hotuba, Kero zetu) wameimba nyimbo zenye maudhui ya kukera serikali kuliko alivyoimba Roma, hawakufungiwa wala kuonywa. Zinduka, Roma si Diamond, kuimba mapenzi kila siku.
 
Bila shaka vyombo vya habari kama TBCCM na Clouds (Not sure) hawawezi kuupiga huu wimbo!
Labda Tbc, ila mie nimeusikia Clouds Fm ijumaa, na jana nimeusikia East Africa Fm. Ni wimbo wa harakati, ni mzuri.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom