2030: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki

kaburu mdogo

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
567
400
Nimesikilza wimbo mpya wa roma mkatoliki ni wimbo wenye ujumbe mkali sana na wenye kuongea kwa hisia kali.
ukuwapi wimbo na unaitwaje?

Unaitwa 2030.. Jibu la ule wimbo wake wa Mathematics.
baadhi tu ya mistari iliyomo
kipindi cha bungeni dodoma inanuka ngono,
spika akiairisha bunge wabunge wanashabikia mgomo
wanadai nyongeza ya posho ili wahonge dada zetu
kuna watoto wa mama salma chuoni usicheze peku
RPC usitume kikosi chadema wakiandamana
utalipa damu ya mwangosi iringa semeni amina
leo ridhiwani hafanani na makongoro....


ngoma ni kali balaa


Wimbo mpya wa HIP POP Kutoka kwa Msanii Roma Mkatoliki unaotamba kwa sasa katika anga la muziki Tanzania ukiwa una siku tatu tu tangu uachiwe hewani. wimbo huo unaonekana unaleta hisia kali za uasi na mapinduzi kwa vijana kutokana na mashairi yake yanayogusa mambo mazito yaliyolikumba taifa kama.

1. Kipigo cha Ulimboka ( kuna mstari unasema Damu ya Ulimboka iwe chachu ya Ukombozi kwa TZ)

2. Mauaji ya Mwandishi wa Habari Mwangosi kule iringa

3. Zitto na .......... Kasulu na Roma na Watanga kuwanga Pangani

4. Ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya Umma

5. Uamsho na vurugu za kidini

6. Ukabila na Ukanda

7. Kiitikio chake sasa yaani ( Chorus) inaizalilisha kabisa Serikali iliyopo madarakani kwani inasauti ya mtoto akilalamika kuhusu Tanzania yake inavyoharibika

8. Mnyukuano wa kisiasa unaondelea hivi sasa nchini nao ndani ya mistari

9. Na mambo yote unayoyafahamu yanayochochea uasi na vurugu kwa Rika la vijana yamezungumziwa katika wimbo huo wenye takribani dk 8 mnaweza ongezea hapo chini....

Kutokana na maudhui ya wimbo huo kuwa kisiasa zaidi inawezekana kabisa serikali sikivu na inayopenda amani kupitia waziri wa Habari na utamaduni kuufungia(Kuupiga BAN) wimbo huo kuendelea kusikika katika masikio ya watanzania kuepusha uasi, vurugu na uvunjifu wa amani unaoweza kutokea kutokana na mashairi ya wimbo huo unaitwa 2030.

Isikilize hapa:
[JFMP3]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=77912&d=1357126820[/JFMP3]
 
Sasa hapo kwenye kochi chandarua unakivaa kama shuka ili kuzuia mbu, la sivyo hata ukitaka kupost kitu unajikuta unajikuna maumivu kisha uzi haukamiliki.Ukiamka asubuhi shemeji anakuwekea mezani kitabu chenye historia ya mbu aina ya anopheles!
 
Dah! Huyu jamaa kweli anajiamini
sana maana mambo mengine mimi simwelewi vile!
 
Back
Top Bottom