2015 nafikiri kutakuwa na CCM-islami na CCM-kristu

Hili swala ni hatari kweli kwa mwenendo mzima wa Taifa. Ningekuwa ccm ningewashauri ili kuondoka na hilo mgombea urais wa 2015 apigiwe kura na wanachama kwa uchaguzi huru.
 
Aisee ni hatari sana, ikotkea hivi mimi ntaanzisha kampeni yakupigia kura watu wasio na dini.. ubaya wa ccm-islam na ccm-kisto ni kwamba huu ugonjwa nikama minyoo kwenye ubongo, utaambukiza watu wasio ccm, yani utatumia CCM kaka infrastructure ya ccm katika ngazi ya kijiji kata wilaya mkoa kanda na taifa kusambaza SUMU ya ubaguzi. I sincerely hope you are wrong my friend otherwise, we will have a serious problem.

Vilevile inabidi Tanzania tuwe na ufahamu kuhusu faida yakutokuwa na matatizo yakibaguzi kama wenzetu wa nchi zinazotuzunguka na tujue jinsi gani wanatamani wao wawe kama sisi au sisi tudorore nakuwa kama wao (leveling the field in their favour). Nadhani hili ni moja ya mambo ambayo yanauwezekano mkubwa sana wa kuathiri usalama wa taifa kiujula ( high potential existential national security threat). Isije ikawa kuna foreign support yakutu destabilize or worse, just us destroying our own peace, security and real chance of developing.

I maintain the oppinion that religion is a dangerous entity if taken beyond a certain level in a secular state like ours, especially where there are two major abrahamic faiths represented in the population. I believe that we should be Tanzanian first and then everything else, religion should improve our lives not threaten our peace. When that happens then religion becomes destructive force. All the leaders in our country should actively condemn this type of thinking and we WANANCHI should not entertain hate-related religious dogma. God loves all man and we should love our neighbour not just the neighbour that goes to the same synagogue...
 
Mwaka 2015 natabiri ndo utakuwa mwazo halisi na uchaguzi wa kufuata dini. Kama Kenya wanavyofuata ukabila.

Sasa mnaanza kuleta utabiri JF. Keep utabiri wako kwako wewe na familia yako. Where are the JF great thinkers?
 
Sio hilo tu hata la ukabila limekwishaanza maana juzi tu tunamskia kamanda wa polisi kanda maalumu ya kipolisi ya Tarime-Rorya anatangazia umma wa watanzania kuwa kwani mkurya wa Nyamongo akiuawa an polisi wewe mtu {Tundu Lissu} wa Singida inakuhusu nini ama inakupunguzia nini kweli
 
Sio hilo tu hata la ukabila limekwishaanza maana juzi tu tunamskia kamanda wa polisi kanda maalumu ya kipolisi ya Tarime-Rorya anatangazia umma wa watanzania kuwa kwani mkurya wa Nyamongo akiuawa an polisi wewe mtu {Tundu Lissu} wa Singida inakuhusu nini ama inakupunguzia nini kweli

Ukabila hauwezi, nafikiri hauwezi fanya kazi. Lakini suala la 2015 kupiga kura kwa misingi ya udini lipo wazi. Kama Kinyambiss alivyosema ccm isipokuwa makini itatumika kama infrastructure kuharibu kila jema.
 
MkamaP,
Mkuu wangu athari za Udini hazitaweza kuathiri vyama kama inavyojengwa leo isipokuwa athari yake itakuwa kwa wananchi ambao sisi wenyewe tutawachagua viongozi kutokana na dini zao. Mkristu atamchagua Mkristu na Muislaam vile vile halafu itafikia hata ku question walichukua form mbona ni dini fulani tu ama kupinga majina mawili ya wagombea wa dini moja na kadhalika.

CCM wanacheza mchezo mbaya sana ambao kwao wao itakuwa kazi sana mwaka 2010 kama watamchagua tena mgombea Muislaam kwa sababu hizi hadithi za Udini wameizanzisha wao makusudi. Na itakuwa mbaya zaidi kama mgombea atakuwa tena Muislaam kwa sababu wao wanataka kuonyesha kwamba CCM hakuna Udini kwa kutazama dini za viongozi wake.

Nakumbuka kabla ya Uchaguzi mh. Membe mtu wangu nilokuwa nikimsifia sana alipohutubia kule Songea, aliwaambia wananchi kwamba JK hana Udini kwa kutazama viongozi wa chama na serikali yake. Hizi zilikuwa siasa chafu sana, siasa za kutenganisha na kuondoa maana halifu ya neno Udini kwa sababu alijenga hisia za kwamba inawezekana JK kuchagua watu kutokana na dini zao na sii uwezo wao kuongoza..

Toka hapo wananchi tumekuwa tukitazam kila kitu kwa majina ya dini za wahusika. Muislaam atamtetea Muislaam kutokana na jina lake hata kama hajui utendaji kazi wa huyo kiongozi. Mkristu vile vile basi ili mradi imani ya Udini kwa tafsiri ya kiimani imechukua sura mpya na kuwa main practice of leadership..

Na pengine haya mambo ya demokrasia ni utamaduni usiotufaa kabisa nchi zetu kwa sababu bado kabisa hatujavunja Ukabila na pia sio dini moja inayotawala imani za wananchi wengi kama nchi za Ulaya. Hawa wenzetu walishaondokana na Ukabila na hata dini zao ni madhehebu tu ndio tofauti zao kubwa hivyo ukiona Muislaam au Budha hawa ni wa kuja. Kwa hiyo swala la udini halipo kwa sababu tayari utamaduni wao ulitokana na chimbuko la dini nchini mwao toka enzi za masultan (King), kwa hiyo kisiasa makanisa yana sauti kubwa ktk chaguzi zao.

Lakini sisi watumwa wa kila kitu tunachoweza kufanya ni kuiga tu masters wetu. Tumeiga toka sheria kuvaa nywele za kubandika ili tuonekanae wazungu hadi kilimo cha kisasa. Kisiasa tunapokuja kuona Obama akiwa questioned kaa ni Muislaam nasi tunataka kuwa question viongozi wetu imani zao za dini ili hali sisi tuna masala ya utamaduni.

Kusema kweli hizi TV na hii mitandao kwa aina fulani imechangia sana madudu yote ya siasa za majitaka kwa nchi za Kiafrika kwa sababu, tunawaona wenzetu wazungu wakihoji imani ya mgombea hivyo nasi pasipo kuzingatia tofauti baina yetu na wao huanza kuhoji. Matokeo yake mkuu wangu uchaguzi mwaka 2015 utakuwa hatari tupu..Naogopa, nachelea kusema kwamba Wadanganyika wajiandae na makubwa zaidi ya hizi siasa za Udini na Ukabila kwani siku zote jiandae kuvuna kile ulichopanda..
 
Mwaka 2015 natabiri ndo utakuwa mwazo halisi na uchaguzi wa kufuata dini. Kama Kenya wanavyofuata ukabila.
wishful thoughts!!!! nadhani weye ni masalia ya Mtabiri Kajura ..sijui kaingilia wapi na kama katangulia basi mungu amrehemu.
 
Mwaka 2015 natabiri ndo utakuwa mwazo halisi na uchaguzi wa kufuata dini. Kama Kenya wanavyofuata ukabila.

mbona yalianza toka 2010, hukumbuki badhi ya makanisa yalifungwa ili waunini wakampigie kura mwenzao.
 
Tumuulize M.S kama mgombea urais wa ccm atakua mkristo ataendelea kuiunga mkono ccm?tukipata jibu basi twaweza jua ya 2015 ccm hatma yake
 
Udini aliunzisha nyerere pale alipoweka padre baraza kuwa mtendaji mkuu wa baraza la mitihani na si kwa uwezo wake bali kwa sababu tu alikuwa muumuni mzuri wa dini ya kikristo, hapo ndio majina ya waaslam yalipoanza kulimwa alipokuja kigoma malima akaliona hilo akaondoa kifunu cha kujaza dini yako na zitumike namba tu badala ya majina, matokeo yake tumeyaona kafanywa kitu gani na nyerere
 

IMANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
1.
Binadamu wote ni Sawa
shim.gif
2.
Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa
na kuthaminiwa utu wake
shim.gif
shim.gif
3.
Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya
kujenga jamii ya watu walio sawa na huru


 
Back
Top Bottom