2012 tuanze na haya au mnasemaje wakuu ?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Mwaka 2012 nadhani sasa ni mwaka mpya wa changes .Siku zote wakuu ninachukizwa na neno hili la mtu kuitwa Mheshimiwa .Yaani tunaacha kumwita Ndugu mbunge Regia tunamwita Mheshimiwa .Sipendi tena nasema nimekerwa , nimekereka ninakerwa hata sasa .Watu kama Mnyinga , Mbowe , Regia ,Lema , mnaweza kuuliza huko Bungeni kwenu kama itawezekana kufuata nyayo za Mwalimu ili kuleta usawa mbele ya jamii kwa kusisitiza kumwita JK ndugu Rais badala ya Mh.Rais au Mh.Mbunge na badala yake iwe ndugu Mbunge , ndugu Spika nk ?

Wewe unasemaje mwana JF ?
 
hawafai kuitwa waheshimiwa; hakuna chochote cha heshima wanayotufanyia

Nafikiri siyo ndugu wangeitwa " makupe wa wananchi" maana ukweli ni kwamba tunawalipa sana halafu wanatunyonya sana kupita watu wengine wote tunaotegemea service zao kama walimu, hakimu nk.
 
Mwaka 2012 nadhani sasa ni mwaka mpya wa changes .Siku zote wakuu ninachukizwa na neno hili la mtu kuitwa Mheshimiwa .Yaani tunaacha kumwita Ndugu mbunge Regia tunamwita Mheshimiwa .Sipendi tena nasema nimekerwa , nimekereka ninakerwa hata sasa .Watu kama Mnyinga , Mbowe , Regia ,Lema , mnaweza kuuliza huko Bungeni kwenu kama itawezekana kufuata nyayo za Mwalimu ili kuleta usawa mbele ya jamii kwa kusisitiza kumwita JK ndugu Rais badala ya Mh.Rais au Mh.Mbunge na badala yake iwe ndugu Mbunge , ndugu Spika nk ?

Wewe unasemaje mwana JF ?

Huo nao ni mtazamo Mnyinga ndo nani?
 
kwa tafsiri yangu.UNAWEZA KUNUNUA CHEO, LAKINI HUWEZI KUNUNUA HESHIMA.
Hivyo kama asilimia kubwa wanashinda uchaguzi kwa mbinu chafu,hila na udanganyifu.basi ni dhahiri kwamba hawa wanakuwa si waheshimiwa bali 'WAISHIWA'
 
Kwa kweli sijui kwa nini wanapenda kutukuzwa hivyo... Hakuna chochote kinachowapa haki ya kuitwa waheshimiwa...
 
kwa tafsiri yangu.unaweza kununua cheo, lakini huwezi kununua heshima.
Hivyo kama asilimia kubwa wanashinda uchaguzi kwa mbinu chafu,hila na udanganyifu.basi ni dhahiri kwamba hawa wanakuwa si waheshimiwa bali 'waishiwa'
imeshiba " mh. Mwana jf"
 
Back
Top Bottom