2012: Arusha tutaendelea kuwa majasiri wa kupinga uonevu - Godbless Lema (MB)

Ama kwel we ritz you are not a great thinker but itz not u, i know that unamaslahi kwenye ccm but rmemba that u can get mor from cdm
 
Ni hotuba yenye hisia kali kwa mtanzania mwenye kuipenda nchi LEMA anahitaji sapoti, laiti cdm wangeongoza halmashauri ya AR. under LEMA (MP) Arusha ingepaa.
 
Hoja tete Lema anamuda gani hapo arusha? Pili hao waliotangulia kabla yake walifanya nini nd kwa muda gani? Pia kwanini hukupenda kuhoji wale wa miaka 50 kwenye utawala katika nchi hii? Je wahisi Lema anatakiwa kujibu hoja kwanini maisha ni magumu kwa watu wa arusha? Wel wajua tanzania wote wanalia shida. So let Lema do his job
 
Hakika nimeamini kwa mara nyingine niseme Arusha wamepata jembe.Wapi wabunge wa ccm nao wajitokeze waeleze waliyoyafanya.Mbunge Lema usichoke endelea kupigania wananchi wa Arusha waliokupa dhamana.Pia usijali wanafiki na mafisadi wachache watakaokukatisha tamaa
hasa ngereja ajitokeze aseme amelifanyia nini jimbo lake.....nilishangaa sana kuona gazeti la mwanachi wamemuweka kwenye list ya watu wanaotafuta urais 2015.....kweli ukistajaabu ya musa utayaona ya filauni.
 
hongera kwa kusema chochote cha mwaka mpya mkuu. pamoja na maneno mazuri lakini natofautiana nawe kidogo kuhusu wewe kupenda kutumia maneno ya kidini na lugha nzuri ili kutupumbaza wana Arusha na watanzania kwa ujumla. pili umeeleza mengi lajkini umeegemea kwenye harakati za kupinga pinga tuuu,huelezi mikakati ya maendeleo hususan ahadi zako kwa wapiga kura.haki unayoeleza ni ile ya wewe kulala mahabusu kwa kupenda au ipi?kumbuka 2015 tutakuhoji miundombinu ya barabara,huduma za afya,elimu na kipato kwa mwananchi wa kawaida.wewe kama mbunge si sahihi kupinga kila kitu hata kile cha maendeleo kama hiki cha kaloleni.hebu angalia salamu za REGIA na mambo aliyoyafanya na pengine utajifunza kitu.uwe na mpango kazi na ulete report inayoeleweka katika specific issues.....waswahili husema akupendae hukwambia mapungufu yako,mnafiki hukusifia hata kama umekosea..
Mkuu imenena kweli. Ni vyema Lema akayafanyia hayo kazi.
 
Nilikuwepo arusha nimejionea mwenyewe ule mbanano wa pale mjini.naungana na wenzangu waliochangia kwa nini haoy maendeleo yasiende nje ya mji mpaka muwavunjie waliojenga toka enzi hizo
 
Naungana na issa shivji kuwa Tanzania hakuna chama mbadala ambacho kitaifanya tz kuwa taifa huru, kama ww dogo lema majukumu madogo tu uliyopata yanakufanya kua ombaomba ng'ambo nataraji cku moja ukiwa kiongozi utakua mara mia ya serikali ya ccm hata matakwa ya Davd camerun ungeyatekeleza..................kwl tatizo sio ccm bali cc watz wenyewe pamoja na ww coz huna mind attitude
hakuomba ila amepewa na isitoshe waliompa ni watanzania wenzetu wanao ishi ng'ambo...wanaogopa michango yao kuitoa moja kwa moja kwenye serikali ya ccm italiwa........hebu nikumbushe hela za rada ziko wp? halafu sina hakika kama prof.shivji alisema hayo.
 
Naungana na issa shivji kuwa Tanzania hakuna chama mbadala ambacho kitaifanya tz kuwa taifa huru, kama ww dogo lema majukumu madogo tu uliyopata yanakufanya kua ombaomba ng'ambo nataraji cku moja ukiwa kiongozi utakua mara mia ya serikali ya ccm hata matakwa ya Davd camerun ungeyatekeleza..................kwl tatizo sio ccm bali cc watz wenyewe pamoja na ww coz huna mind attitude

Vibaraka wa ccm utawajua tu,cause kwao tumbo mbele maendeleo nyuma.
 
Naungana na issa shivji kuwa Tanzania hakuna chama mbadala ambacho kitaifanya tz kuwa taifa huru, kama ww dogo lema majukumu madogo tu uliyopata yanakufanya kua ombaomba ng'ambo nataraji cku moja ukiwa kiongozi utakua mara mia ya serikali ya ccm hata matakwa ya Davd camerun ungeyatekeleza..................kwl tatizo sio ccm bali cc watz wenyewe pamoja na ww coz huna mind attitude

hivi kasema marafiki wake wazungu au wanaishi huko.
 
Hawa ndio wana Chadema huwa hawataki kujibu hoja.

Kazi yao kupinga yote yawe mema au mabaya tena wanapinga kila kitu ilimradi tu kudumisha sifa ya kuitwa wapinzani.

Kuna thread ya Hotuba ya Rais watu wanahoji na kuchambua bila tatizo.

Lakini hawataki watu wachambue na kuhoji hotuba za viongozi wao kama Lema.

kumbe ile hotuba ya jk ni hotuba ya ccm
 
Mkuu, JF sio sehemu ya porojo hunaweza kuweka ushahidi wa hayo maneno yako wafadhili wa Lema, Uingereza ni wana Arusha?

Lema, mwenyewe kwenye bandiko lake kasema kuna marafiki zake Uingereza wamemsaidia, wewe unasema wana Arusha

Kwani Lema akisaidiwa wewe inakuuma nini au unaendeleza ushoga wako humu jf ritz ngongo mwita 25 siyo kila kitun zuri unawaza pinga au kukosoa hakuna jambo lolote zuri la Lema nyie mkalikubali zaidi ya yote mtaliandika kwa mabaya ili mjaze posti zenu ebu mwaka huu mbadilike muache ushoga wenu humu jf cyo lazima kila posti inayo muhusu Lema mchangie au inayo muhusu Mbowe Slaa nilazima mchangia au inayo husu chadema mchangie kaeni kimya kama bossi wenu nape narudia tena acheni ushoga humu jf
 
Wapambe wake wanasema hakusema! Halafu wanasema ni kazi ya serikali sababu ndio wakusanya kodi..

Kuna sehemu Lema, kasema wataanza kutekeleza ahadi alizosema, lakini ajaweka wazi ni ahadi gani hizo labda ndio hizo za Machinga Complex pamoja na barabara za juu

ritz acha ushoga Lema hana mpambe wala hakuna mbunge wa chadema mwenye mpambe kwani wamekuwa wa ccm ndiyo wenye wapambe acha kumpa Lema ahadi za kikwete ahadi za Lema zina julikana napia ameziweka kwenye ujumbe ameshaanza na kiwanja cha uspitali sasa anaaza mwaka huu mapema ujenzi wa uspitali hiyo huu ni mwaka mmoja wa mbunge Lema anemesha fanya mengi mazuri naataendelea kufanya mazuri ila kwenu nyie mashoga ni mabaya nyie endeleni kujivua gamba namuache wivu wakike nyie mnao mpinga Lema kazi zake za kila siku
 
hongera kwa kusema chochote cha mwaka mpya mkuu. pamoja na maneno mazuri lakini natofautiana nawe kidogo kuhusu wewe kupenda kutumia maneno ya kidini na lugha nzuri ili kutupumbaza wana Arusha na watanzania kwa ujumla. pili umeeleza mengi lakini umeegemea kwenye harakati za kupinga pinga tuuu,huelezi mikakati ya maendeleo hususan ahadi zako kwa wapiga kura.haki unayoeleza ni ile ya wewe kulala mahabusu kwa kupenda au ipi?kumbuka 2015 tutakuhoji miundombinu ya barabara,huduma za afya,elimu na kipato kwa mwananchi wa kawaida.wewe kama mbunge si sahihi kupinga kila kitu hata kile cha maendeleo kama hiki cha kaloleni.hebu angalia salamu za REGIA na mambo aliyoyafanya na pengine utajifunza kitu.uwe na mpango kazi na ulete report inayoeleweka katika specific issues.....waswahili husema akupendae hukwambia mapungufu yako,mnafiki hukusifia hata kama umekosea..

Nikweli nazidi kuamini wewe ni mjinga mkubwa sana kwani maneno ya dini mtu akitumia anatumia kwa manufaa ya kumpendezesha mtu kwani Lema anataka kumpendezesha mtu au ni wewe na akili yako kwani Lema amekuwa kikwete na ahadi zake zakupendezesha wadanganyika kama wewe lini Lema alisema ataboresha barabara afya elimu na kipato cha mwananchi wewe unaweza ukawa mbunge ukaangalia kipato cha mwananchi hivi unajua maana ya kipato cha mwananchi kitu kama elimu akuhaidi ila amesomesha watoto 417 uspitali ndiyo alihaidi au wewe ndiyo kina ritz ngongo kwakupotosha ukweli???
 
Lema hongera sana;

Unajua mimi sio mbunge wako kwa kweli; na nashukuru kutokuwa mbunge wako. Nina machache ya kukuambia mdogo wangu maana mimi umri kidogo umekwenda.

1. Inasikitisha bado kiongozi kama wewe unaendeleza falsa ya kutembeza bakuli tena wakati mwingine kwa ajili ya huduma za kijamii, i thought uta-mobilize wananchi wenyewe wachangie kwa maendeleo yao kwa uwezo mkubwa uliopewa especially wa kupeleka watu barabarani... kwenye falsafa ya "wape ndoana ili waweze kuvua na kulisha familia zao milele as opposed na wape samaki ili wakuene wewe mungu kwao.

2. Mafanikio yako unaji-distance na viongozi wenzako wa Halmashauri, Serikali etc, huo sio uongozi mzuri; uongozi ni pamoja na kusema wazi, e.g. nawashukuru/tumekubaliana na serikali au halmashauri tumeamua hili au hata watu fulani wa Arusha na sio marafiki wa Ulaya, wananchi wajua unayowaahidi marafiki wako wa Ulaya?... you as a person bila kusema una wana Arusha wengine inaonyesha udhaifu mkubwa sana wa kiuongozi.

3. Umejisifia sana na kudai haki na hili unajipongeza sana etc, well and good ndio viongozi wetu wanatengeza manifesto zao baada ya kushinda; ila nadhani umesahau role yako.... wewe sio mbunge wa jimbo la kitaifa, wewe ni mbunge wa Arusha mjini; tekeleza ya Arusha alafu ndio u-capitalize ya kitaifa... otherwise ni sawa sawa na kuingia chumba cha mtihani uone kuna maswali ya kujibu uache hayo maswali utunge yako na kuyajibu kwa ufasa.

4. Kiongozi yeyote anajisifu kama wewe ulitakiwa kuonyesha uliyoahidi, uliyoyafanyia na ambayo yako mbele yako... kutoonyesha hayo hapa... ni upungufu mwingine. "progress report, lakini ni wazi kwamba hujaonyesha hilo, kwa makusudi kwa sababu unataka ficha mambo ndio viongozi wote wadhaifu wanavyofanya, kwenye public sector na private... great leaders wanaweka mambo wazi and let people to jurge.

Nakutakia safari njema, nadhani bado uta-wa-win waTanzania wengi not b'se you are good or rather great leader just b'se of the type of people you are leading.....
 
MWAKA 2012 - ARUSHA TUTAENDELEA KUWA MAJASIRI WAKUPINGA UKANDAMIZAJI POPOTE TANZANIA . GODBLESS LEMA (MB)
Ninapotafakari Wema wa Mungu katika maisha yangu na Jimbo langu , ndipo ninapopatwa wajibu wa kuleta salamu zangu za mwaka mpya kwenu , tumeuona mwaka 2012 salama. , Mwaka jana 2011 tumepita kwenye changamoto nyingi sana , tumepinga kila aina ya dhuluma , uonevu , na mateso bila woga , Watu wengi walituelewa tulipofanya harakati hizo na wachache wasiojua maana ya haki na utu walitupuuza na kutesema vibaya kwa sababu tu hawakuelewa maana ya Amani.
Nimesema na nitasema siku zote kuwa Arusha hatutakubali kuendelea kuona Haki ,Utu na Ukweli unapuuzwa kwa kisingizio cha utulivu na amani kwani “afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu” Arusha tuendelee kuwa imara bila kuogopa kejeli na matusi ya vyombo vya habari na vijana wanaotumika kwenye mitandao ya kijamii mbali mbali kudhoofisha ukweli , kwani ni lazima tujue kuwa tumeingia mwaka 2012 lakini shetani bado yuko hai na wafuasi wake wataendelea kufanya wajibu wao wa kupotosha ukweli na kudhalilisha utu wa Mwanadamu, pia ni lazima tutambue kuwa utakuwa ni udhahifu mkubwa kama tutaendelea kukaa kimya na kusema wametushinda kwa sababu tu wana majeshi ,silaha na magereza ni lazima tujue kuwa hakuna silaha au jeshi Duniani lilishawahi kushindana na Nguvu ya Umma na jeshi hilo likashinda , hivyo dhambi kubwa kuliko yote itakuwa ni uoga wala sio uwezo wa nguvu zetu na akili zetu.
Arusha, ni vyema tukatambua kuwa hakuna mmoja wenu mwenye sababu ya msingi hata moja ya kukaa kimya wakati mambo hayaendi sawa na kufanya hivyo ni kosa kubwa kuliko unavyofikiri kwani wenye hekima walisema “ uovu unatawala tu pale watu wema wanapokaa kimya” Tusiogope jina la mtu tena, wala cheo cha mtu , mwizi ni mwizi hata kama huyo mwizi ni baba yako, mwaka huu utakuwa mwaka mzuri kwetu kwani uzuri wake hautatokana na mabadiliko ya kalenda bali kwa kuwa tu tumekubaliana tena kwamba mapambano ya kupigania haki na ukweli katika Nchi yetu bado yanaendelea bila woga wala hofu.
Arusha ,thamani yetu katika harakati za Nchi yetu ni kubwa sana na wala msifikiri mnafanya kwa ajili ya Arusha tu , jipeni moyo kwani faida ya kuishi sio kula wala kunywa bali ni wajibu wa upendo na kupigania utu kwa jamii nyingine Duniani na hakika huu ukiwa ni msingi wa fikra zetu basi Nchi yetu itapata ukombozi hivi karibuni, lazima tutambue kuwa hakuna mabadiliko makubwa Duniani yaliyotokea kirahisi na kila jambo jema unaloliona nyuma yake kuna watu waliteseka na hata wengine kufa , kwa hiyo ni lazima mtambue kuwa kuendelea kusonga mbele kupigania Nchi yako sio wajibu mwepesi ni wajibu unaopaswa kuuchukua bila kuogopa vitisho wala mauti .

Wako miongoni mwetu hata ndani yetu watakaotumika kwa njia mbali mbali kudhoofisha mapambano ya kupigania Nchi yetu na wamekwishaanza na wanaendelea kwa sababu zao binafsi na masilahi yao , hawa pia msiwaogope kwani hila na uongo haviwezi kushindana na ukweli , hao nao, Tutawashinda tu wao na wapambe zao , haijalishi nani yuko nyuma yao , Bob Marley alisema “ only times will tell”.

Lakini pia pamoja na salamu hizi Arusha tumefanya mengi sana na mimi kama Mbunge niwaeleze machache tu ambayo tumeyafanya ndani ya changamoto nyingi tulizopitia mwaka jana
1) Tulizindua Taasisi ijulikanayo kama Arusha Development Foundation ( ArDF ) na kwa mwaka wa 2011 tumesomesha watoto takribani 417 bila kutegemea Halmashauri wala Serikali.
2) Mwaka 2011 - tulipokea Trekta kutoka kwa marafiki zangu walioko Uingereza na tulilima lakini kwa dhambi nyingi za Serikali mvua haikuwa nyingi na tulikosa mavuno ambayo tulikuwa tumepanga kuanzisha mfuko wa kusaidia yatima na wajane wanye hali duni sana.
3) Mwaka 2011 -Tumepewa ambulance (gari la kubeba wagojwa ) na rafiki zangu kutoka Uingreza na hivi majuzi baada ya kutoka magereza ambako nilikuwa nimeenda kwa hiari yangu kwa sababu ya kupinga uonevu , na sasa waliposoma habari hizo ,wamesema wameongeza nyingine moja na sasa zimekuwa mbili.
4) Lakini pia tumepata kiwanja kwa ujenzi wa Hosipatali ya Mama na Mtoto ambao ni matumaini yangu mwakani mapema Mungu atasaidia ujenzi utaanza na katika jambo hili hakuna mkono wa Serikali isipokuwa juhudi zetu binafsi na thamani yake ni zaidi ya milioni mia tatu ( 300,000,000)
5) Lakini vile vile tumesaidia sana sehemu mbali mbali kama magereza , vituo vya watoto yatima ukweli hii kwangu ni kama sadaka tu na si jambo la kujivunia sana Kama kazi za Mbunge, lakini nimesema niseme ili upate majibu ya kuwajibu wahuni wanaotudhiaki.
Sasa haya ni machache tu ili uweze kutambua dhamira yangu ya kweli katika utumishi kama Mbunge , pamoja na matatizo na changamoto zote tulizopitia lakini tumeweza kusonga mbele na yote niliyoaidi nitafanya , kwani vumilieni huku tukitiana moyo kwani tunajitahidi sana pia , natambua kutokufanya sio aibu yangu bali ni kuvunja moyo wanaharakati ambao wanamatumaini makubwa na sisi na chama chetu , na hivyo najua itakuwa ni kosa kubwa kuuwa tumaini lililopo katika chama chetu ambacho wananchi wengi wanakiona kama tumaini la kweli, hivyo ni lazima tufanye kazi zote tulizo ahidi wakati wa kampeni “ INAWEZEKANA.
Hata hivyo hiko Miradi ya barabara ambayo itaanza kujengwa mwaka huu wa 2012 kati kati ya mji wetu na ni rai yangu kuwa nitakuja kuongea nanyi tuweke utaratibu mzuri wakuweza kupisha maendeleo hayo ya hizo bara bara bila polisi kutumia nguvu , kwani ni imani yangu kuwa mnahitaji upendo zaidi na hekima katika hatua hii ya kuwahamisha kuliko nguvu ,Mimi kama Mbunge natambua jinsi hizo biashara zenu ndogo ndogo zilivyokuwa na maana katika familia zenu na maisha yenu , hivyo niwahakikishie kuwa upendo itakuwa silaha yetu kubwa katika kukubaliana kupisha maendeleo ya bara bara na ni imani yangu kuwa mtanielewa.
Vile vile ningependa salamu zangu za mwaka mpya niongelee kidogo suala la Nyumba za Kaloleni, ninapinga watu kuhamishwa na hii haina ukweli kuwa mimi Mbunge napinga maendeleo ya Arusha bali natambua kuwa maendeleo katika jamii sio tu kuwa na maduka na viwanda bali kuwa na uhakika wa maisha bora ya watu , hivyo maendeleo ya msingi kwangu yataanza na maisha ya watu na sio vitu.
Maswali mengi najiuliza katika mradi huu wa Kaloleni na ukweli sipati majibu na maswali haya ni kama yafuatayo ;
1) Kwanini jambo hili la huu mradi tenda haikutangazwa kama ambavyo ni sheria ya Serikali ?
2) Hivi kweli wamekosekana Watanzania wenye uwezo wa kujenga huo mradi mpaka tuende Nje ya Nchi kutafuta wawekezaji ? ni kweli wametuambia hatuwezi kuchimba madini ya uranium kwani yanahitaji utaalamu sana , je hata kujenga maduka hatuwezi ? hivi hata wenzetu tulioungana nao Waafrika Mashariki , hakuna wenye uwezo ?
3) Hivi kweli kama lengo ni kujenga Arusha na kuleta ufanisi wa Mji na ajira , je ni kwanini sasa Halmashauri isipanue Mji kwa kutoa maeneo ya pembezoni mwa Arusha ili kupanua Mji , kwani itasaidia kupunguza msongamano wa magari na kuwa ni mji mwingine wa Arusha wa kisasa .
4) Kaloleni ni makazi ya watu miaka yote , Aicc wanataka kujenga shopping complex eneo hilo hilo na Halmashauri ya Manisipaa ya Arusha inataka kujenga kitu hicho hicho kwenye eneo hilo hilo , je kweli hawa watu wanafikiria Mji wa kisasa au hii ni rushwa ya kisasa ? ndio maana mwekezaji feki alitoa ofa ya Madiwani kwenda kutembea Dubai ?
5) Maswali mengi yako hapo, lakini najua huwezi kumkata mototo mkono ili shati limtoshe , hivyo maendeleo ya msingi katika jamii ni yale yatakaojali utu na haki za binadamu na sio vitu , Kaloleni ni makazi ya watu muda mrefu sasa ni vyema makazi hayo yakaboreshwa na watu wakaishi wengi zaidi hasa watumishi wa Serikali ambao mishahara yao ni midogo sana, na kama Mwekezaji hatafuata utaratibu wa Serikali wa kupata tenda na hakashinda basi sehemu sahihi yakuwekeza kwa sasa ni kwenda nje ya Arusha ili kupanua Mji na kupunguza msongamano wa Jamii katikati ya Mji.
Hata hivyo machache hapo juu sio mambo ya kujivunia sana ,Mimi kama Mbunge wenu kitu nachojivunia kuliko vyote kwamba nimekifanya na kina maana kubwa sana ni kuweza kuwafanya watu wangu kuwa majasiri na kuwa tiyari kupigania haki zao wakati wowote hii kwangu ni Legacy na heshima kubwa katika maisha yangu.
Pengine leo itoshe hizi kuwa salamu zangu za mwaka mpya 2012 , Arusha ninawapenda sana , sina hila moyoni mwangu dhidi ya maisha ya Nchi yetu , ninatambua wema wenu katika Nchi yetu na tuna deni kubwa sana na wajibu wakuleta mabadiliko katika Nchi yetu , Tusiogope ,Tusiogope ,Tusiogope bado kitambo kidogo maadui zetu watakuwa chini ya miguu yetu.

Muhammad Ali , alisema “He who is not courageous enough to take risks will accomplish nothing in life “
Arusha tuendelee kuwa na nia nzuri na makusudi mazuri , Mapambano bado yanaendelea heri ya Mwaka 2012.

GODBLESS LEMA (MB)

mapambano yameanza na yanaendelea.
 
Wewe lema ni jembe sana...hata kama ccm wataamua kunyamazisha sauti yako ya kudai haki basi hata miti itatoa sauti ya kudai haki na democrasia na hapo ndipo ccm watalia na kusaga meno...
 
Back
Top Bottom