2012: Arusha tutaendelea kuwa majasiri wa kupinga uonevu - Godbless Lema (MB)

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Feb 9, 2010
899
1,084
MWAKA 2012 - ARUSHA TUTAENDELEA KUWA MAJASIRI WAKUPINGA UKANDAMIZAJI POPOTE TANZANIA . GODBLESS LEMA (MB)
Ninapotafakari Wema wa Mungu katika maisha yangu na Jimbo langu , ndipo ninapopatwa wajibu wa kuleta salamu zangu za mwaka mpya kwenu , tumeuona mwaka 2012 salama. , Mwaka jana 2011 tumepita kwenye changamoto nyingi sana , tumepinga kila aina ya dhuluma , uonevu , na mateso bila woga , Watu wengi walituelewa tulipofanya harakati hizo na wachache wasiojua maana ya haki na utu walitupuuza na kutesema vibaya kwa sababu tu hawakuelewa maana ya Amani.
Nimesema na nitasema siku zote kuwa Arusha hatutakubali kuendelea kuona Haki ,Utu na Ukweli unapuuzwa kwa kisingizio cha utulivu na amani kwani “afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu” Arusha tuendelee kuwa imara bila kuogopa kejeli na matusi ya vyombo vya habari na vijana wanaotumika kwenye mitandao ya kijamii mbali mbali kudhoofisha ukweli , kwani ni lazima tujue kuwa tumeingia mwaka 2012 lakini shetani bado yuko hai na wafuasi wake wataendelea kufanya wajibu wao wa kupotosha ukweli na kudhalilisha utu wa Mwanadamu, pia ni lazima tutambue kuwa utakuwa ni udhahifu mkubwa kama tutaendelea kukaa kimya na kusema wametushinda kwa sababu tu wana majeshi ,silaha na magereza ni lazima tujue kuwa hakuna silaha au jeshi Duniani lilishawahi kushindana na Nguvu ya Umma na jeshi hilo likashinda , hivyo dhambi kubwa kuliko yote itakuwa ni uoga wala sio uwezo wa nguvu zetu na akili zetu.
Arusha, ni vyema tukatambua kuwa hakuna mmoja wenu mwenye sababu ya msingi hata moja ya kukaa kimya wakati mambo hayaendi sawa na kufanya hivyo ni kosa kubwa kuliko unavyofikiri kwani wenye hekima walisema “ uovu unatawala tu pale watu wema wanapokaa kimya” Tusiogope jina la mtu tena, wala cheo cha mtu , mwizi ni mwizi hata kama huyo mwizi ni baba yako, mwaka huu utakuwa mwaka mzuri kwetu kwani uzuri wake hautatokana na mabadiliko ya kalenda bali kwa kuwa tu tumekubaliana tena kwamba mapambano ya kupigania haki na ukweli katika Nchi yetu bado yanaendelea bila woga wala hofu.
Arusha ,thamani yetu katika harakati za Nchi yetu ni kubwa sana na wala msifikiri mnafanya kwa ajili ya Arusha tu , jipeni moyo kwani faida ya kuishi sio kula wala kunywa bali ni wajibu wa upendo na kupigania utu kwa jamii nyingine Duniani na hakika huu ukiwa ni msingi wa fikra zetu basi Nchi yetu itapata ukombozi hivi karibuni, lazima tutambue kuwa hakuna mabadiliko makubwa Duniani yaliyotokea kirahisi na kila jambo jema unaloliona nyuma yake kuna watu waliteseka na hata wengine kufa , kwa hiyo ni lazima mtambue kuwa kuendelea kusonga mbele kupigania Nchi yako sio wajibu mwepesi ni wajibu unaopaswa kuuchukua bila kuogopa vitisho wala mauti .

Wako miongoni mwetu hata ndani yetu watakaotumika kwa njia mbali mbali kudhoofisha mapambano ya kupigania Nchi yetu na wamekwishaanza na wanaendelea kwa sababu zao binafsi na masilahi yao , hawa pia msiwaogope kwani hila na uongo haviwezi kushindana na ukweli , hao nao, Tutawashinda tu wao na wapambe zao , haijalishi nani yuko nyuma yao , Bob Marley alisema “ only times will tell”.

Lakini pia pamoja na salamu hizi Arusha tumefanya mengi sana na mimi kama Mbunge niwaeleze machache tu ambayo tumeyafanya ndani ya changamoto nyingi tulizopitia mwaka jana
1) Tulizindua Taasisi ijulikanayo kama Arusha Development Foundation ( ArDF ) na kwa mwaka wa 2011 tumesomesha watoto takribani 417 bila kutegemea Halmashauri wala Serikali.
2) Mwaka 2011 - tulipokea Trekta kutoka kwa marafiki zangu walioko Uingereza na tulilima lakini kwa dhambi nyingi za Serikali mvua haikuwa nyingi na tulikosa mavuno ambayo tulikuwa tumepanga kuanzisha mfuko wa kusaidia yatima na wajane wanye hali duni sana.
3) Mwaka 2011 -Tumepewa ambulance (gari la kubeba wagojwa ) na rafiki zangu kutoka Uingreza na hivi majuzi baada ya kutoka magereza ambako nilikuwa nimeenda kwa hiari yangu kwa sababu ya kupinga uonevu , na sasa waliposoma habari hizo ,wamesema wameongeza nyingine moja na sasa zimekuwa mbili.
4) Lakini pia tumepata kiwanja kwa ujenzi wa Hosipatali ya Mama na Mtoto ambao ni matumaini yangu mwakani mapema Mungu atasaidia ujenzi utaanza na katika jambo hili hakuna mkono wa Serikali isipokuwa juhudi zetu binafsi na thamani yake ni zaidi ya milioni mia tatu ( 300,000,000)
5) Lakini vile vile tumesaidia sana sehemu mbali mbali kama magereza , vituo vya watoto yatima ukweli hii kwangu ni kama sadaka tu na si jambo la kujivunia sana Kama kazi za Mbunge, lakini nimesema niseme ili upate majibu ya kuwajibu wahuni wanaotudhiaki.
Sasa haya ni machache tu ili uweze kutambua dhamira yangu ya kweli katika utumishi kama Mbunge , pamoja na matatizo na changamoto zote tulizopitia lakini tumeweza kusonga mbele na yote niliyoaidi nitafanya , kwani vumilieni huku tukitiana moyo kwani tunajitahidi sana pia , natambua kutokufanya sio aibu yangu bali ni kuvunja moyo wanaharakati ambao wanamatumaini makubwa na sisi na chama chetu , na hivyo najua itakuwa ni kosa kubwa kuuwa tumaini lililopo katika chama chetu ambacho wananchi wengi wanakiona kama tumaini la kweli, hivyo ni lazima tufanye kazi zote tulizo ahidi wakati wa kampeni “ INAWEZEKANA.
Hata hivyo hiko Miradi ya barabara ambayo itaanza kujengwa mwaka huu wa 2012 kati kati ya mji wetu na ni rai yangu kuwa nitakuja kuongea nanyi tuweke utaratibu mzuri wakuweza kupisha maendeleo hayo ya hizo bara bara bila polisi kutumia nguvu , kwani ni imani yangu kuwa mnahitaji upendo zaidi na hekima katika hatua hii ya kuwahamisha kuliko nguvu ,Mimi kama Mbunge natambua jinsi hizo biashara zenu ndogo ndogo zilivyokuwa na maana katika familia zenu na maisha yenu , hivyo niwahakikishie kuwa upendo itakuwa silaha yetu kubwa katika kukubaliana kupisha maendeleo ya bara bara na ni imani yangu kuwa mtanielewa.
Vile vile ningependa salamu zangu za mwaka mpya niongelee kidogo suala la Nyumba za Kaloleni, ninapinga watu kuhamishwa na hii haina ukweli kuwa mimi Mbunge napinga maendeleo ya Arusha bali natambua kuwa maendeleo katika jamii sio tu kuwa na maduka na viwanda bali kuwa na uhakika wa maisha bora ya watu , hivyo maendeleo ya msingi kwangu yataanza na maisha ya watu na sio vitu.
Maswali mengi najiuliza katika mradi huu wa Kaloleni na ukweli sipati majibu na maswali haya ni kama yafuatayo ;
1) Kwanini jambo hili la huu mradi tenda haikutangazwa kama ambavyo ni sheria ya Serikali ?
2) Hivi kweli wamekosekana Watanzania wenye uwezo wa kujenga huo mradi mpaka tuende Nje ya Nchi kutafuta wawekezaji ? ni kweli wametuambia hatuwezi kuchimba madini ya uranium kwani yanahitaji utaalamu sana , je hata kujenga maduka hatuwezi ? hivi hata wenzetu tulioungana nao Waafrika Mashariki , hakuna wenye uwezo ?
3) Hivi kweli kama lengo ni kujenga Arusha na kuleta ufanisi wa Mji na ajira , je ni kwanini sasa Halmashauri isipanue Mji kwa kutoa maeneo ya pembezoni mwa Arusha ili kupanua Mji , kwani itasaidia kupunguza msongamano wa magari na kuwa ni mji mwingine wa Arusha wa kisasa .
4) Kaloleni ni makazi ya watu miaka yote , Aicc wanataka kujenga shopping complex eneo hilo hilo na Halmashauri ya Manisipaa ya Arusha inataka kujenga kitu hicho hicho kwenye eneo hilo hilo , je kweli hawa watu wanafikiria Mji wa kisasa au hii ni rushwa ya kisasa ? ndio maana mwekezaji feki alitoa ofa ya Madiwani kwenda kutembea Dubai ?
5) Maswali mengi yako hapo, lakini najua huwezi kumkata mototo mkono ili shati limtoshe , hivyo maendeleo ya msingi katika jamii ni yale yatakaojali utu na haki za binadamu na sio vitu , Kaloleni ni makazi ya watu muda mrefu sasa ni vyema makazi hayo yakaboreshwa na watu wakaishi wengi zaidi hasa watumishi wa Serikali ambao mishahara yao ni midogo sana, na kama Mwekezaji hatafuata utaratibu wa Serikali wa kupata tenda na hakashinda basi sehemu sahihi yakuwekeza kwa sasa ni kwenda nje ya Arusha ili kupanua Mji na kupunguza msongamano wa Jamii katikati ya Mji.
Hata hivyo machache hapo juu sio mambo ya kujivunia sana ,Mimi kama Mbunge wenu kitu nachojivunia kuliko vyote kwamba nimekifanya na kina maana kubwa sana ni kuweza kuwafanya watu wangu kuwa majasiri na kuwa tiyari kupigania haki zao wakati wowote hii kwangu ni Legacy na heshima kubwa katika maisha yangu.
Pengine leo itoshe hizi kuwa salamu zangu za mwaka mpya 2012 , Arusha ninawapenda sana , sina hila moyoni mwangu dhidi ya maisha ya Nchi yetu , ninatambua wema wenu katika Nchi yetu na tuna deni kubwa sana na wajibu wakuleta mabadiliko katika Nchi yetu , Tusiogope ,Tusiogope ,Tusiogope bado kitambo kidogo maadui zetu watakuwa chini ya miguu yetu.

Muhammad Ali , alisema “ He who is not courageous enough to take risks will accomplish nothing in life “
Arusha tuendelee kuwa na nia nzuri na makusudi mazuri , Mapambano bado yanaendelea heri ya Mwaka 2012.

GODBLESS LEMA (MB)
 
Nakubaliana na Lema kuondoa watu kaloleni siyo maendeleo kabisa; wakitaka wakajenga hayo shopping centre kisongo au mbali na mji kuleta maendeleo ya kweli
 
Hakika nimeamini kwa mara nyingine niseme Arusha wamepata jembe.Wapi wabunge wa ccm nao wajitokeze waeleze waliyoyafanya.Mbunge Lema usichoke endelea kupigania wananchi wa Arusha waliokupa dhamana.Pia usijali wanafiki na mafisadi wachache watakaokukatisha tamaa
 
Nakubaliana na Lema kuondoa watu kaloleni siyo maendeleo kabisa; wakitaka wakajenga hayo shopping centre kisongo au mbali na mji kuleta maendeleo ya kweli

hakika Topical umenikuna.Una hekima sama mkuu
 
Nakubaliana na Lema kuondoa watu kaloleni siyo maendeleo kabisa; wakitaka wakajenga hayo shopping centre kisongo au mbali na mji kuleta maendeleo ya kweli
Mkuu ni kweli eneo la kisongo ni ideal kwa ajili ya shopping centres. watakuwa wanaupanua mji wa arusha badala ya kuvuruga.
 
hakika Topical umenikuna.Una hekima sama mkuu

Sipendi watu wanaofikiri kubomoa, kuchukua mali ya mtu hasa nyumba...wakajenga mbali na mjini kaloleni ni resedential tena imepangika vizuri; kwanini wasiende nje ya mji ili kuendeleza ule wa mji wa arusha km5 tu kutoka mjini unakutana na mashamba na nyumba za wamasai unplanned...it is cheap and easy kuliko kuvunja za watu
 
Nakubaliana na Lema kuondoa watu kaloleni siyo maendeleo kabisa; wakitaka wakajenga hayo shopping centre kisongo au mbali na mji kuleta maendeleo ya kweli

hakika Topical umenikuna.Una hekima sama mkuu
 
Hongera mb Lema kuhusu issue ya Kaloleni .Arusha bado inanafasi ya kutosha kupanuka na kujengeka kisasa kuendelea kurundika kila kitu katikati ya Mji ni mipango finyu isiyozingatia taaluma . Naungana nawe katika kapinga suala hili na najivunia Kuishi Arusha.

Mbali na hayo naomba uweke wazi mipango ya halmashauri na mkoa ili tuweze kuwauliza Kama haitatekelezwa. Hii itatusaidia kihoji na kushinikiza serikali Juu ya utekelezaji wake
 
Sipendi watu wanaofikiri kubomoa, kuchukua mali ya mtu hasa nyumba...wakajenga mbali na mjini kaloleni ni resedential tena imepangika vizuri; kwanini wasiende nje ya mji ili kuendeleza ule wa mji wa arusha km5 tu kutoka mjini unakutana na mashamba na nyumba za wamasai unplanned...it is cheap and easy kuliko kuvunja za watu

asante sana mkuu Topical.Tupingane kwa mambo mengine lakini tuungane kwa mambo yakitaifa kama haya.
 
Kweli mbunge,wapanue mji.Kisongo,Njiro chini,Kikatiti,Ukielekea maeneo ya Oldo sambu n.kHaya ni maeneo ambayo yanatakiwa planners wa mji huu Arusha wakune vichwa sio kuwatia watu umasikini kwa kuwabomolea.Poor thinking,poor planners.
 
Safi sana Mh lema hakika wewe ni mpigania utu na haki ya mwanadamu,tupo pamoja katika mapambano haya dìdi ya mkoloni mweusi CCM,tupo pamoja daima Mh lema.
 
Muheshimiwa Mbunge ameshema yale ambayo yamikamilika au mchakato wake upo mwisho kukamilika, so machinga complex ipo kwenye plain ikifika wakati wake atatujuza wapiga kura wake. Lema brother keep on napenda majibu kwa hawa jamaa yawe kwa vitendo and nt otherwise.
 
Mbona hajazungumzia ile Machinga complex aliyoahidi kuijenga pale stendi ya mabasi?

Wapambe wake wanasema hakusema! Halafu wanasema ni kazi ya serikali sababu ndio wakusanya kodi..

Kuna sehemu Lema, kasema wataanza kutekeleza ahadi alizosema, lakini ajaweka wazi ni ahadi gani hizo labda ndio hizo za Machinga Complex pamoja na barabara za juu
 
eneo la kaloleni limeuzwa kwa wale wanaojiita WAWEKEZAJ wala sio maendeleo. Nje ya jiji maeneo kama lemara, uswahilini, sinoni, sokon, engosengiu, muriet, murumbo, mkonoo, nadosoito, terat, njiro nk. Maeneo ya jiji la Arusha maeneo mengi yako wazi mengine ni mashamba tena hayalimwi kabisa. Ndo maeneo yanayostahi upanuzi wa maendeo.
 
Naungana na issa shivji kuwa Tanzania hakuna chama mbadala ambacho kitaifanya tz kuwa taifa huru, kama ww dogo lema majukumu madogo tu uliyopata yanakufanya kua ombaomba ng'ambo nataraji cku moja ukiwa kiongozi utakua mara mia ya serikali ya ccm hata matakwa ya Davd camerun ungeyatekeleza..................kwl tatizo sio ccm bali cc watz wenyewe pamoja na ww coz huna mind attitude
 
Wapambe wake wanasema hakusema! Halafu wanasema ni kazi ya serikali sababu ndio wakusanya kodi..

Kuna sehemu Lema, kasema wataanza kutekeleza ahadi alizosema, lakini ajaweka wazi ni ahadi gani hizo labda ndio hizo za Machinga Complex pamoja na barabara za juu

waambie wabunge wako wa ccm nao wajipambanue kama hawa mashujaa wa chadema
 
Back
Top Bottom