2011: Visima Kuchimbwa Singida Mjini

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Wakuu hivi visima bado vinachimbwa mijini, yaani kama makao makuu ya mkoa wanaongelea kuchimba visima ni vipi kuhusu Igunga. Ok najua watu watasema mbona hata Dar mwendo ndiyo huo huo! Jamani haya ni mambo ya aibu kabisa wala si jambo la kufurahia hata kidogo. Yaani miaka 50 ya uhuru tunazungumzia maji ya visima mijini?????????

Kilichionimaliza hapa chini ni kuona kiongozi mkubwa kabisa wa chama tawala, waziri mzoefu kupiga picha hadharani akikabidhi hundi kwa mkandarasi iliyotolewa na Sabodo kwa ajili ya uchimbaji visima Singida Mjini. C'moon mambo mengine inabidi uone aibu Chiligati hakustahili kabisa kukaa karibu na hiyo hundi ni aibu.Hizi hela za Sabodo mimi nilifikiri ni kuchimba visima vijijini huko kusikofikika, sasa kumbe hata makao makuu ya mikoa??? Serikali hii ina nini cha kujivunia in 50 years kama hata mambo basic kabisa kama haya hawayawezi???????

68zeoy.jpg
 
Omr ungelikuwa ni mwanangu wa K ningekuoza hata pasipo kuhitaji mahali..you are really exceptional,good!
 
Kama ulivyosema, hata Dar tunahitaji Sabodo atuchimbie visima. Hivi unajua ni asilimia ngapi ya wakazi wa Dar wanapata maji ya bomba? Usingeshangaa Singida mjini wakati hali ni hiyo hiyo Dar. Hata hivyo halmashauri ya Singida mjini ina vijiji kadhaa, Unyamikumbi, Kisaki, Mtamaa, Kinyeto ,Kisasida nk ambavyo hivyo visima ni muhimu kwao.
Swala la miaka 50 tuko kapa ni kwa sababu ya ukilaza wa waTz kuichagua CCM kila siku....miaka mingine 100 tutakuwa hivi hivi kama tutazidi kuwa na vichwa maji.
 
Wewe ulitaka wa mjini wanywe bia?
Wewe unafikiri kwa kutumia masaburi,maji ya kisima siyo tatizo,tatizo ni visima kuchimbwa mjini,sngida ni katika mikoa iliyo na ukame mkubwa hakuna mito ya kuweza kupata maji mwaka mzima hivyo visima ni lazima,visima vichimbwe mbali na makazi ya watu halafu maji yaletwe mjini kwa njia ya mabomba.
 
Omr ungelikuwa ni mwanangu wa K ningekuoza hata pasipo kuhitaji mahali..you are really exceptional,good!

Unawaza kumuoza Omary kwa kua wewe mwenyewe umeolewa!,
anacho shangaa Omary ni uchimbaji wa visima katikati ya mji,Dar kuna visima vya namna hiyo ndiyo sababu kipindupindu Dar kila siku kipo hakiishi,maji machafu yanaingia kwenye visima na watu wanayanywa.
 
Kama ulivyosema, hata Dar tunahitaji Sabodo atuchimbie visima. Hivi unajua ni asilimia ngapi ya wakazi wa Dar wanapata maji ya bomba? Usingeshangaa Singida mjini wakati hali ni hiyo hiyo Dar. Hata hivyo halmashauri ya Singida mjini ina vijiji kadhaa, Unyamikumbi, Kisaki, Mtamaa, Kinyeto ,Kisasida nk ambavyo hivyo visima ni muhimu kwao.
Swala la miaka 50 tuko kapa ni kwa sababu ya ukilaza wa waTz kuichagua CCM kila siku....miaka mingine 100 tutakuwa hivi hivi kama tutazidi kuwa na vichwa maji.

Yaani ni mambo ya aibu kabisa mkuu!!!!, acha hivyo vijiji vya mbali maji hata masaki yanasombwa kwa malori, kuna maeneo kama Ubungo ile ya kuelekea Kimara mambomba yapo na bili zinakuja lakini maji hayajawahi kutoka!!!!!!! UkijaTabata maeneo kibao hakuna maji, ukienda kiwalani ndio usiseme....

Ni aibu isiyo kipimo!
 
Watanzania wote bila kujali ni wa mjini au vijijini wanahitaji maji...hiyo ya kulazimisha eti mjini kuwe na mabomba si hoja ya msingi,kipindupindu kinasababishwa na mchanganyiko wa uchafu mwingi incl.sewage system,vyoo,vyakula tunavokula pamoja na huko masokoni.unapoleta mada hapa ukumbuke inasomwa na watu wengi wenye akili zao acha propaganda za chuki.
 
Singida Mjini ni shamba la Bibi, Ngome kuu ya Chama cha Mapinduzi kwa sababu ya Kanga, Vitenge, shilingi elfu tano tano, na fulana za kiongozi wao. Wanadanganywa, wanadanganyika. Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, tuliahidiwa na Mohamedi Dewji kujenga Uwanja wa Namfua, na kukarabati pagara la ofisi ya Chama cha Magamba, lakini alimaliza muda wote hakuleta hata nondo moja wala mfuko mmoja wa Cementi. Alipokuja Mwaka 2010, Yeye na JK, wakawadanganya wana Singida kuwa wangejenga uwanja mpya badala ya kukarabati wa Zamani, tena akasema alikuwa ameleta nyasi za thamani ya milioni 300, ambazo angeweka mwezi Desemba 2010, baada ya Uchaguzi. amedanganya hadi leo. Chiligati naye ni kibaraka wao tu, ndio wanaohongwa ili kuja kuhadaa wana Singida. Aidha sijashangaa kumwona Chiligati amejitokeza maana ndio uwezo wake wa kufikiri umerudia hapo. siku mmoja alipokea mshindi wa mashindano ya Big Brother akasema ni utekelezaji wa sera za CCM. Tunamshukuru Sabodo kwa kusaidia wana Singida.
 
Watanzania wote bila kujali ni wa mjini au vijijini wanahitaji maji...hiyo ya kulazimisha eti mjini kuwe na mabomba si hoja ya msingi,kipindupindu kinasababishwa na mchanganyiko wa uchafu mwingi incl.sewage system,vyoo,vyakula tunavokula pamoja na huko masokoni.unapoleta mada hapa ukumbuke inasomwa na watu wengi wenye akili zao acha propaganda za chuki.

Unaongea nini maana sijakuelewa, propaganda za chuki ipi na kwa nani? Duh! mzee umepata mlo wa asubuhi au?
 
miaka 50 ya uhuru.
TUMETHUBUTU TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE.
OLE WAKE MTU ATAKAEWAKURUPUSHA WANYATURU MMEKURUPUSHA WACHAGA TUKANYAMAZA MAKAKURUPUSHA WAMASAI,WASUKUMA,WAHEHE,WANYAKYUSA,WAHA,WAHAYA ILA HILI LA WANYATURU TUTAUANA.
MTUACHIE HAWA NA WAGOGO WANATUTOSHA.
 
Unajua ubaya wa kujimba visima kwenye makazi ya watu? Ni kwamba kunakuwa na underground movement of particles(e.g. Salt, compounds consisted in wastes(kinyesi)) from toilets/dampo to wells. Kwahiyo kiafya hichokitu ni hatari sana hata kumong'onyoka meno wa watumiaji wa maji ya kisima inatokana na leakages na kuyeyuka kwa kemikali za cement iliyotumika kujengea kuta za kisima. Ushauri vijiji sana miji ni hapana.
Nimecheka hadi mbavu kutaka kuvujika eti Big Brother ni utekelezaji wa ilani ya majambazi kweli tumeishiwa.
 
Tatizo hapa ni serkali ya ccm kujisahau kiasi cha kutisha. Wasiwasi wa chama tawala baada ya CDM kukabidhi mchanganuo wa kuchimba visima kwenye majimbo yanayoongozwa na chama kikuu cha upinzani. Mzee mzima Chiligati katoka kichwa kichwa kukabidhi hundi eti kabla ya kupigwa bao. Kauli mbiu yao ya tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele mimi inanipa tabu kidogo kuamini baada ya miaka 50 ya uhuru watu wananyeshwa maji ya tope mijini. Kuna usemi unasema kuwa kama hujui ku "paste" usi "copy". Baada ya Dr wa kweli Slaa kwenda kwa Sabodo Upanga basi safari za viongozi wa CCM nyumbani kwa kada huyu sasa zimekuwa mfululizo. Hukumu ya wananchi kuhusu kunyimwa huduma kwa nusu karne yaja.
 
Unajua ubaya wa kujimba visima kwenye makazi ya watu? Ni kwamba kunakuwa na underground movement of particles(e.g. Salt, compounds consisted in wastes(kinyesi)) from toilets/dampo to wells. Kwahiyo kiafya hichokitu ni hatari sana hata kumong'onyoka meno wa watumiaji wa maji ya kisima inatokana na leakages na kuyeyuka kwa kemikali za cement iliyotumika kujengea kuta za kisima. Ushauri vijiji sana miji ni hapana.
Nimecheka hadi mbavu kutaka kuvujika eti Big Brother ni utekelezaji wa ilani ya majambazi kweli tumeishiwa.

Mkuu hicho ndiyo kinannifanya nishangae!!!!!!!!!!
 
Singida kuna ziwa Kindai. Hivi hilo ziwa haliwezi kutosheleza kutoa maji ya bomba kwa
wakazi wa Singida mjini kwa mwaka?
 
hilo bwawa la kindai ni chumvi kama bahari. Kama watachimba deep wells, water table ya singida ni nzuri maji mengi sana...mfano mzuri ni visima vya Makiu
ngu vinavyotumia windmill pumps.
 
Unajua ubaya wa kujimba visima kwenye makazi ya watu? Ni kwamba kunakuwa na underground movement of particles(e.g. Salt, compounds consisted in wastes(kinyesi)) from toilets/dampo to wells. Kwahiyo kiafya hichokitu ni hatari sana hata kumong'onyoka meno wa watumiaji wa maji ya kisima inatokana na leakages na kuyeyuka kwa kemikali za cement iliyotumika kujengea kuta za kisima. Ushauri vijiji sana miji ni hapana.
Nimecheka hadi mbavu kutaka kuvujika eti Big Brother ni utekelezaji wa ilani ya majambazi kweli tumeishiwa.

Mkuu kuna akina Omar humu hawaelewi Wanadhani watu wanakandiya maji ya kisima kutumika mjini. Hawaelewi kipindupindu kinatoka wapi hawajui kipindupindu kinatokana na kula au kunywa mavi fullstop. Mjini mvua zikinyesha watu wanatapisha vyoo vyao hadi kunatokea mafuriko. Sasa kama kisima Kipo maeneo yale Sijui kitakachopatikana ni nini kwenye yale maji.

Singida mjini nao wanapenda kuchagua wabunge waarabu na wahindi ngoja wafaidi matunda ya kura zao kwa kunywa kinyesi.
 
Back
Top Bottom