2011 ni mwaka wa Mfumuko wa Bei, maisha magumu na Ujambazi juu!

single zake za "TAARAB" zimeisha tusubir aandike/aandikiwe mashairi mapya labda atarud jukwaani tena
 
Unajua nimegundua kuwa kumbe hata Obama mwenyewe hana utaratibu wa kuongea na wananchi wake kila mwezi. Nadhani JK naye ana kila sababu ya kutoendelea na huu utaratibu uliopitwa na wakati. Kinachoonekana kwa sasa ni kuwa ameamua kuwa mtendaji zaidi kuliko muongeaji, kitu ambacho kinastahili sifa sana. Si umeona bei za mafuta zilivyoshuka sasa.

Gas, electricity and food prices have dropped dramatically
 
Eti wana jf sometimes naona hamna umuhimu wa kwenda shule ona ajira hakuna kila cku tunaapply lakini hatupati ajira. Dah
 
Hua najilaumu sana kwanini nimepoteza miaka 3 chuo, maana sasa naangaika kila siku kutafuta kazi ambazo hazipatikani nimechoka hadi kuapply
 
hana jipya la kuongea maana ahadi zote kamaliza na matumaini yote kamaliza ila sasa hali ya wapiga kura ainazidi kuwa mbaya, Kuhusu kuchaguliwa halo nalo linazidi kujidhihirisha kila siku kwamba yeye si kipenzi cha watanzania so HAKUCHAGULIWA kajichagua mwenyewe na Jaji Makame a.k.a. Kivuitu
 
Say NO MORE CCM.

thumbnail.aspx
 
dont give up kaka.then inawezekana tatizo ikawa ni ww mwenyewe may b huwezi kujieleza au unachagua kazi au ndo walewale mnataka mshahara kuanzia milioni sababu ndo mlikua mnadanganyana mkiwa chuo.fanya kazi yoyote halali upate hela bahasha na stamp kuombea kazi unayoitaka.pia kujiajiri ndo njia rahisi sana.mimi nimemaliza degree naona sipati kazi nauza mitumba huku nafanya masters.
 
Hua najilaumu sana kwanini nimepoteza miaka 3 chuo, maana sasa naangaika kila siku kutafuta kazi ambazo hazipatikani nimechoka hadi kuapply
Hujapoteza muda mkuu. Ipo siku kitu cha kufanya ili kujipatia kipato kitapatikana. Omba mungu na uzidi kuhangaika bila kukata tamaa.
 
Usikate tamaa hata kidogo,Siku yaja ambayo utaona hukupoteza muda,Vilevile hiyo elimu yako ndo inakufanya uone ulipoteza muda ungekuwa huna usingeweza kufikiria hivyo,nakushauri anza na kidogo then utaona tu,Mimi nilitafuta sana kazi nikakata tamaa nikaanza kuwafundisha watoto wa primary kwa kuwafuata majumbani kwao kupitia moja ya mzazi wa watoto niliokuwa nawapa darasa akanipeleka offisini kwao kama msaidizi pale ofisini na nikawa nalipwa kama casual labor(Tsh 75,000),then nikawatoa kimasomaso kwa kujituma,fikiria nilikuwa natumwa hadi chai sometimes na nina degree yangu, kuptia pale nikaja kupata kazi inayoendana na fan yangu ingawa nayo haikudumu.
 
Leo asbh wife aliniambia stoo ya msosi ni nyeupe, taratibu nikajikongoja hadi CRDB kuangalia masalia nikachukua elfu 50, wife alihitaji kununua vitu vidogovidogo kama mchele, sukari, chumvi na mboga kidogo. Huwezi amini bei za vitu zinapanda kila siku wife karudi na kuniambia pesa haijatosha. Nimeapa kabisa hakika KIKWETE havumiliki.
 
Nashukuru na wewe umeliona hilo sijui wale wa kijijini wanaionaje hali
 
Leo asbh wife aliniambia stoo ya msosi ni nyeupe, taratibu nikajikongoja hadi CRDB kuangalia masalia nikachukua elfu 50, wife alihitaji kununua vitu vidogovidogo kama mchele, sukari, chumvi na mboga kidogo. Huwezi amini bei za vitu zinapanda kila siku wife karudi na kuniambia pesa haijatosha. Nimeapa kabisa hakika KIKWETE havumiliki.

Pole sana mkuu ila pia nasikitika kwani umechelewa mno kulijua hili. Wengi wetu kilio hiki kilianza miaka kama minne iliyopita ila ndio hivyo binadam wengi tumeumbwa Kitomaso zaidi yaani huwa hatuamini mpaka yatutokee! I hope now you and my sis inlaw have made up your mind through this simple lesson. Na hilo ni moja tu, waulize wafanyabiashara wanoenda china sikuhizi wanaenda na box la tshillings pale mtaa ya samora kuchange wanarudi na dolali za kwenye wallet tu! Hapo mgao wa umeme, ufisadi, huduma mbovu za hospital na mengineyo tuizungumzie!
 
ndio sasa hivi nchi inatokota.

Hali mbaya ya uchumi wa nchi inachangia wananchi kuwa na hasira.

Shillingi imeshuka thamani, vitu vimepanda bei mno

kipato cha mwananchi kimepungua

Ajira hakuna, vijana hawana ajira.

Bidhaa muhimu kuadimika na kupanda bei.

Nchi sasa haitawaliki tena....

Watu wa vijijini wanategemea sana sukari, pia sukari inategemewa na wagonjwa.

Vyombo vya dola -Polisi na sasa hata mhimili wa nchi mahakama vinatumika kama fimbo ya kuwachapa wananchi, dhuluma. Sijui kama mabavu ndo maisha bora???

Mafuta taa, nishati ya wanyonge, sasa imepandishwa bei, hapo ndo mbaya zaidi. Sasa unategemea tena amani hapo, kweli. Mtu mwenye njaa utamwambia amani???? Maandamano yanakuja, tena makubwa sana. Watawala waliambiwa sana, wakaziba masikio, wamekuja kuambiwa na IMF wabane matumizi, hapo ndo kimbembe- tusubiri sasa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom