watu wengi waliofanikiwa hawakupata mafanikio hayo kwa msaada wa serikali kama wapo ni wachache sana, mtu mweyewe ndiyo mwenye jukumu ka kuhakikisha kuwa anajiwekea katika mazingira ambayo yatamrahisishia kufanikiwa. Kama ni mwanafunzi, kinachotakiwa ni kusoma kwa bidii ili kuweza kufaulu mitihani yake vizuri ili mwisho wa siku apate ajira au maarifa yatakayomwezesha kutoka kimaisha. Serikali inachofanya ni kuweka mazingira fulani tu ambayo yatamsafishia njia mtu kutoka. mtu yeyote sijidanganye kucheza na maisha akidhani kuwa anaweza kufanikiwa kirahisi juhudi na maarifa ya mtu mwenyewe ndiyo njia pekee ya kufanikiwa kimaisha. Uvivu na ulegevu wa namna yoyote pamoja na kujihusisha na vitendo viovu yote hayo matokeo yake ni kukudhoofisha kimaisha na baadae mtu anabaki kusingizia serikali kuwa haikufanya chochote. Fanya shughuli yako yoyote halali kwa bidii, kuwa na nidhamu ya pesa unayopata, jiepushe na starehe pamoja na matumizi mabaya ya pesa yako, kuwa mbunifu katika kazi yako au biashara yako, lenga soko lenye wataja au huduma utaona kama hutafanikiwa!!! Kamwe usisubiri muujiza wa mafanikio, muujiza upo kichwani mwako.:confused2: