Elections 2010 2010 - Ni Mwaka wa Uhuru Wetu

Kwa maoni yangu, inabidi watu waungane na vyama vya upinzani. Lengo liwe moja tu kwa uchaguzi ujao, "Kuongeza Upinzani Bungeni". That should be the only goal in next year election.

From there we can start challenging the government in other fronts especially the constitution, and I believe it will be easier for other parties and NGO to show up their support.

Also lets remember to utilize all the tools we have to communicate with our family members anywhere in the rural areas. Pick two or three reasons why they should not elect chama cha mafisadi. If you keep pounding those three points day in day out, you will have a chance to convince them, at least 50%.

I believe we can come up with simple-to-follow stratergy we can share with our family and friends.

Lets Do It!
 
Tatu.. muungano huo ni lazima uwe muungano wenye misingi yake; muungano wenye lengo la kuingusha CCM tu ni muungano unaojiandaa kushindwa. Lengo la kuunganisha nguvu liwe ni zaidi ya kuiangusha CCM; yaani, kuanguka kwa CCM kuwe ni matokeo tu ya lengo hilo kuu.
 
Zakumi Kuli yupo nchini, anaudai uhuru hapa hapa kwa ajili yetu na ninyi mlioikimbia nchi yenu wenyewe na kuwaachia mafisadi na wawekezaji waipepete kama ngano!
 
Lugha rahisi na nyepesi ni kuchukua KITI CHA IKULU..binafsi naamini kabisa utawala wowote hasa nci zetu maskini huanzia IKULU. Nikitazama sehemu zote za Ufisadi zimetokana na Teuzi za rais kuwapa nyadhifa hao Mafisadi toka mawaziri, wakuu wa mashirika ya Umma, wakuu wa mikoa na nafasi zote nyeti za kuvuta mtaji hutokana na uchaguzi wa rais.

Kushinda Ubunge sii tiketi ya kupewa wadhifa wa juu, wapo wabunge wengi sana walichaguliwa, wapo nje ya uongozi wa serikali yetu na ndivyo inavyotakiwa lakini kwa kutumia mfumo wa zamani unaosisitiza hatua ya kwanza kwa uteuzi wa kiongozi wa serikali unatokana na kushinda chaguzi za Ubunge sasa kumepotea na wala hauna maana tena,sioni mchango wa mbunge ktk kupata Uhuru chini ya mfumo uliopo zaidi ya kuona jina la mwakilishi, sababu RAIS ndiye mchaguzi wa viongozi wetu na ndiko tunakopata Mafisadi.

Hivyo inanipa shida kubwa sana kutambua vita hii itaelekeza majeshi wapi..Umesema kukiondoa chama CCM madarakani sii hoja haujali ni chama gani kitaingia madarakani..wakati namsoma Mwalimu Augustine Moshi akisisitiza ni wakati wa kukiondoa chama..Hii inanikumbusha uchaguzi wa Iran.. Hivi kweli lengo la wananchi ilikuwa kumwondoa Ahmadinajad au ilikuwa kukiondoa chama tawala. Kenya na Zimbabwe kote tumeona utata uliopo ktk kumwondoa kiongozi madarakani na itakuwa vizuri tukizungumzia zaidi majeshi yetu yaelekeze nguvu zake wapi, kwa maana fupi TATIZO LIKO WAPI?..
1. Je, kumwondoa JK Ikulu itaondoa uongozi mbaya..
2. Je, kukiondoa chama CCM madarakani (Ubunge) kutapunguza nguvu ya rais ktk kuchagua viongozi wabovu?..
3. Je, Kuonndoka kwa vyote hivi viwili kutaleta Uhuru wa kweli? na Kivipi yaani..
Huo Uongozi utakao kuja utakuwa na agenda zipi muhimu ktk kuhakikisha Uhuru wa kweli unapatikana.
 
Last edited:
Zakumi Kuli yupo nchini, anaudai uhuru hapa hapa kwa ajili yetu na ninyi mlioikimbia nchi yenu wenyewe na kuwaachia mafisadi na wawekezaji waipepete kama ngano!

Mimi narudi lakini sio kwenye siasa. Mwakani narudi kuwa kabaila. Nitayarishie mashamba tu.
 
Uhuru mnadahi mkiwa majuu.

Wewe bado unaamini penye daraja lazima kuna mto unapita chini. Hizo zama zimepitwa siku nyingi sana.

Kwa taarifa yako, jikumbushe South Africa walipataje uhuru wao kutoka kwa makaburu. Sina haja ya kusema mengi.

There's are so many avenue to advance this fight as long as everyone play their part.
 
Uhuru unatakiwa kudaiwa mtu akiwa wapi? na kwanini ni mahali pekee hapo panapotakiwa kudaiwa uhuru?

Mwanakijiji:

Don't get me wrong. Sehemu yoyote unaweza kupambana. Kwa kipaji chako na kwa matukio yaliotokea Tanzania katika kipindi cha sasa, kama ungekuwa ndani ya CCM na kuanzisha vuguvugu humo, huo uhuru ungepatikana.
 
Tatu.. muungano huo ni lazima uwe muungano wenye misingi yake; muungano wenye lengo la kuingusha CCM tu ni muungano unaojiandaa kushindwa. Lengo la kuunganisha nguvu liwe ni zaidi ya kuiangusha CCM; yaani, kuanguka kwa CCM kuwe ni matokeo tu ya lengo hilo kuu.

I don't disagree with you but your approach is so broad. We need to have one "defined goal" which will advance a broad change. If we can have a great number of MP's we will be able to block all these nonsense laws and loopholes the government is using now to sabotage nation resources.

Again, lets keep ideas going. I would to see other intellectials from our higher institutions and NGO get their ideas out.
 
Zakumi mashamba wameshagawana, yale ya NAFCO wamepewa wawekezaji - ni 2 tu yamerudishwa kwa wananchi ila na hayo bado hali ya ugawaji wake ni tete. Kule Kilosa ndio usiseme, wakuu wana ekari na mahekta. Na hapo Mvomero nako mmh. Ibwagwamoyo wameuza kwa bei chee mashamba ambayo wajamaa tuliyataifisha kwa maslahi ya umma. Hivyo kama unarudi basi huwezi kuikimbia siasa ya ukombozi, lazima kwanza ujiunge kupigania uhuru wa pili - na tutakapoupata huo uhuru wetu mwaka 2010 kamwe hatutakubali uwe kabaila humu, labda uwe mkulima mwenza wa kijamaa!
 
Mwanakijiji:

Don't get me wrong. Sehemu yoyote unaweza kupambana. Kwa kipaji chako na kwa matukio yaliotokea Tanzania katika kipindi cha sasa, kama ungekuwa ndani ya CCM na kuanzisha vuguvugu humo, huo uhuru ungepatikana.

kila kitu ni mikakati na kwenye siasa hakuna kitu muhimu kama mikakati yenye timing. Believe me, ningekuwa nyumbani labda sasa hivi nisingekuwa na muda wa kufanya ninayofanya.

ulivyosema hapo juu ni kama kuashiria kwamba ambaye hayuko Tanzania hapaswi kupigania uhuru wa taifa lake na ni wale walioko nyumbani tu ndio wenye haki na sababu ya kufanya hivyo.
 
Lugha rahisi na nyepesi ni kuchukua KITI CHA IKULU..binafsi naamini kabisa utawala wowote hasa nci zetu maskini huanzia IKULU. Nikitazama sehemu zote za Ufisadi zimetokana na Teuzi za rais kuwapa nyadhifa hao Mafisadi toka mawaziri, wakuu wa mashirika ya Umma, wakuu wa mikoa na nafasi zote nyeti za kuvuta mtaji hutokana na uchaguzi wa rais.

Kushinda Ubunge sii tiketi ya kupewa wadhifa wa juu, wapo wabunge wengi sana walichaguliwa nje ya uongozi wa serikali na ndivyo inavyotakiwa lakini kwa kutumia mfumo wa zamani unaosisitiza hatua ya kwanza kwa uteuzi wa kiongozi wa serikali unatokana na kushinda chaguzi za Ubunge sasa hivi umepotea na wala hauna maana tena zaidi ya jina la mwakilishi kwa sababu RAIS ndiye mchaguzi wa viongozi wetu.

Hivyo inanipa shida kubwa sana kutambua vita hii itaelekeza majeshi wapi..Umesema kukiondoa chama CCM madarakani sii hoja haujali ni chama gani kitaingia madarakani..wakati namsoma Mwalimu Augustine Moshi akisisitiza ni wakati wa kukiondoa chama..Hii inanikumbusha uchaguzi wa Iran.. Hivi kweli lengo la wananchi ilikuwa kumwondoa Ahmadinajad au ilikuwa kukiondoa chama tawala. Kenya na Zimbabwe kote tumeona utata uliopo ktk kumwondoa kiongozi madarakani na itakuwa vizuri tukizungumzia zaidi majeshi yetu yaelekeze nguvu zake wapi, kwa maana fupi TATIZO LIKO WAPI?..
1. Je, kumwondoa JK Ikulu itaondoa uongozi mbaya..
2. Je, kukiondoa chama CCM madarakani (Ubunge) kutapunguza nguvu ya rais ktk kuchagua viongozi wabovu?..
3. Je, Kuonndoka kwa vyote hivi viwili kutaleta Uhuru wa kweli? na Kivipi yaani..
Huo Uongozi utakao kuja utakuwa na agenda zipi muhimu ktk kuhakikisha Uhuru wa kweli unapatikana.

tatizo sio ccm ,ccm bomba kama vilivyo vyama vingine na kufikiri kubadili chama ndio ukombozi.. thubutuuuuu ,

tatizo ni fikra zetu watanzania ktk hali bapa na iliyo na mwelekeo sahihi ni ukombozi wa fikra zetu wenyewe.
Tatizo letu ni fikra ndio maaneo ya ukombozi ni maeneo ambayo tunatakiwa kuyafanyia kazi ktk ukombozi wa kweli na si ukombozi maomboleo wa kuidondosha ccm.
 
Wewe bado unaamini penye daraja lazima kuna mto unapita chini. Hizo zama zimepitwa siku nyingi sana.

Kwa taarifa yako, jikumbushe South Africa walipataje uhuru wao kutoka kwa makaburu. Sina haja ya kusema mengi.

There's are so many avenue to advance this fight as long as everyone play their part.

Kuna kitu kinaitwa common enemy. South Africa waliweza kufanya vile kwa sababu walikuwa na common enemy, (mzungu na siasa zake za ubaguzi).

Leo hii Mwanakijiji anapigania haki sahihi, lakini maadui ndugu zake tena wengine wa damu. Akirudi kwao kijijini anamkuta mjomba wake ana shati la CCM. Binadamu yake kajenga nyumba nzuri aliyofikia kwa kutumia pesa za akaunti ya EPA.

Mambo yanayofanywa na watawala wetu yangekuwa yanafanywa na wageni, tayari tungekuwa na sirikali mpya.
 
2010 kuwa mwaka wa uhuru wetu? Sidhani. Jamaa hawa bado wamekamata sehemu zote muhimu na nyeti za Nchi yetu. CCM yenye wengi wa watu bado ndio yenye SERIKALI. Itashinda tena 2010 kote kuanzia uongozi wa mitaa na vijiji vyetu mwaka huu na MADIWANI, UBUNGE na URAIS mwakani.
Tunaojua Nchi ilikokuwa, ilipo na inakoelekea bado ni wachache mno na miongoni mwa hao tunaojua, WAOGA tuko wengi, TUNAOFAIDIKA na mfumo wa sasa hatuambiwi kitu tukasikia, NGOs, MAKANISA, MISIKITI ndio vinaamka sasa.
Kazi bado mbichi kabisa lakini tusikate tamaa kwa kuwa UHURU na MABADILIKO huletwa na WACHACHE.

:confused: Hivi kwa nini tunakuwa na mashaka na woga kuhusu ukombozi wetu? Hakuna lisilowezekana. Kinachotakiwa ni nguvu ya kueneza elimu ya uraia, hasa vijijini, ili waTz watambue kwamba nchi yao ni tajiri sana lakini utajiri wote unahamishiwa nje na MAFISADI wachache wanaokula pamoja na Chama Cha Mafisadi (CCM). Wakishatambua hilo ni rahisi kusonga mbele.
 
Last edited:
Zakumi mashamba wameshagawana, yale ya NAFCO wamepewa wawekezaji - ni 2 tu yamerudishwa kwa wananchi ila na hayo bado hali ya ugawaji wake ni tete. Kule Kilosa ndio usiseme, wakuu wana ekari na mahekta. Na hapo Mvomero nako mmh. Ibwagwamoyo wameuza kwa bei chee mashamba ambayo wajamaa tuliyataifisha kwa maslahi ya umma. Hivyo kama unarudi basi huwezi kuikimbia siasa ya ukombozi, lazima kwanza ujiunge kupigania uhuru wa pili - na tutakapoupata huo uhuru wetu mwaka 2010 kamwe hatutakubali uwe kabaila humu, labda uwe mkulima mwenza wa kijamaa!

Nakusikia mkuu. Lakini si umeona waKenya wamemtolea uvivu mzungu wa madini?

Nataka kuwekeza kule wanakokumbia wao, sehemu zilizochoka. Kwa sababu mimi ni kabaila mbunifu Kwikwikwi.

Pamoja na hayo mipango mibaya ya ardhi ni kutembelea kwenye mabomu ya kutegwa.
 
Kuna kitu kinaitwa common enemy. South Africa waliweza kufanya vile kwa sababu walikuwa na common enemy, (mzungu na siasa zake za ubaguzi).

Leo hii Mwanakijiji anapigania haki sahihi, lakini maadui ndugu zake tena wengine wa damu. Akirudi kwao kijijini anamkuta mjomba wake ana shati la CCM. Binadamu yake kajenga nyumba nzuri aliyofikia kwa kutumia pesa za akaunti ya EPA.

Mambo yanayofanywa na watawala wetu yangekuwa yanafanywa na wageni, tayari tungekuwa na sirikali mpya.

Hivi unafikiri hadi hivi sasa sijui ndugu zangu ambao ni sehemu ya ufisadi huu? Unafikiri ninaangalia damu yangu ili kujua kama nikemee au la. Sina umoja wa aina yoyote wa kidini, kidamu, kilugha, kirangi au kimahali na anayeshiriki kwenye ufisadi. Wana matatizo wenye kuangalia fisadi kwa minajili ya dini, rangi, kabila au urafiki wao. Kama hii kweli ni vita basi ichukuliwe kama hivyo. Ndugu aliyeungana na adui siyo ndugu yangu tena!
 
Kuna kitu kinaitwa common enemy. South Africa waliweza kufanya vile kwa sababu walikuwa na common enemy, (mzungu na siasa zake za ubaguzi).

Leo hii Mwanakijiji anapigania haki sahihi, lakini maadui ndugu zake tena wengine wa damu. Akirudi kwao kijijini anamkuta mjomba wake ana shati la CCM. Binadamu yake kajenga nyumba nzuri aliyofikia kwa kutumia pesa za akaunti ya EPA.

Mambo yanayofanywa na watawala wetu yangekuwa yanafanywa na wageni, tayari tungekuwa na sirikali mpya.

Nafahamu hilo lakini pia wahenga walisema, "Kikulacho ki nguoni mwako."

Kwa hiyo wewe unaniambia kuwa ndugu yako au baba yako akiua kwa makusudi hauta mpeleka police?

Yes, we know who is our common enemy. CCM knows who is our common enemy. They are on the driver seat. Are they taking any action? No.

Do you think if they take action I will support them 100%? You bet.

So, we need to think outside the box.
 
kila kitu ni mikakati na kwenye siasa hakuna kitu muhimu kama mikakati yenye timing. Believe me, ningekuwa nyumbani labda sasa hivi nisingekuwa na muda wa kufanya ninayofanya.

ulivyosema hapo juu ni kama kuashiria kwamba ambaye hayuko Tanzania hapaswi kupigania uhuru wa taifa lake na ni wale walioko nyumbani tu ndio wenye haki na sababu ya kufanya hivyo.

Mwanakijiji:

You are absolutely right, mikakati yenye timing ni kitu muhimu. Lakini watanzania wengi hatujuhi tunapigania nini?

Kama unashindwa ku-define unachopigania, mikakati yako yenye timing itakuwa ni kitu cha bure.

Kwa mfano katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, vita vilikuwa dhidi ya ufisadi. Now, uchaguzi unakaribia vita vipo kwenye uhuru, na baadhi ya mafisadi wamekuwa viongozi wa kupambana na ufisadi na wengine wanaogopa usalama wa maisha yao.
 
hapana.. ufisadi ni dalili tu za tatizo tulilonalo; the underlying cause ni masuala yanyohusiana na uhuru. Kwa kadiri tunavyoendelea mbele ndivyo tunalielewa vizuri zaidi tatizo letu. Mwanzoni kwa kiasi kikubwa kuna kile kinachoitwa "fog of war" ambapo hatuoni vizuri zaidi lakini kwa kadiri tunavyopiga hatua ndivyo tunazidi kulewa the nature of the war and the capabilities of the enemy.

Nitakuwa nikijidai nikisema kuwa miaka minne iliyopita nilimuelewa adui, uwezo na mikakati yake; sikumuelewa. Mwanzoni nilifikiri ni suala la kisiasa zaidi na linaweza kubadilika kwa kuibua uozo na kufichua udhaifu wao watawala walioko madarakani. Hili tumelionesha vizuri lakini wakati huo huo wao (mafisadi na vikaragosi wao) wanatuma ujumbe unaosikika ukisema "we are here to stay" na dalili zinazoonekana hadi hivi sasa ni kweli hawaendi popote.

Ndio maana kwenye makala hii, I have gone at lenght kuelezea what is at stake kwani sas ninamuelewa vizuri zaidi adui, mkakati wake na uwezo wake. Ninaamini kabisa kuwa endapo kundi la viongozi hao watarudi tena madarakani 2010, tutakuwa tumepoteza nafasi nzuri sana ya kufanya mabadiliko ya watawala wa taifa letu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom