19 wamefariki kwa mgomo wa madaktari Sekou Toure Mwanza

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
Tangu mgomo uanze 23/06/2012 wagonjwa 19 wamefariki katika hospitali ya mkoa Mwanza ya Sekou Toure. Akihojiwa na Startv mganga mkuu wa hospital hiyo ina interns 20 ambao waligoma ila hadi sasa 6 wamerejea na kuendelea na kazi,14 wamerudishwa wizarani kwa kuendelea na mgomo.

Source:Startv Habari.

NB:Wewe unajisikiaje kwa watu kufa kwasababu ya mgomo? Najua kuna wengine wanaona nisawa kwakuwa wanavijisent vyakwenda private,lakini jiulize je kama ni ndugu yako kafariki wewe ungejisikiaje? Jamani tuache siasa kwenye afya!
 
Faida ya serikali DHAIFU & LEGELEGE na bila shaka ndio matunda yake hayo!

Poleni wafiwa na MUNGU awalaze marehemu wote mahala pema peponi!
 
Hata kabla ya mgomo wagonjwa walikuwa wanakufa tu hapo hospitali
 
Kwa vyovyote vile Spika wa bunge anastahili lawama. Kama serikali na madaktari wana mgogoro, kwa akili ya kawaida kabisa, bunge lingeingilia kati na kuweka pande hizi mbili pamoja. Lakini kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe Spika ameamua kuzima jitahada zozote za bunge kujadili na kupata muafaka.

Labda tujikumbushe mgomo wa wauza mafuta (fuel) ambao ulikuwa kati ya serikali na wauza mafuta. Bunge liliingilia kati na ndipo muafaka ukapatikana. Sasa kwa nini hili la madaktari Spika anakataa? Hata ile report ya kamati ya huduma za jamii ambayo ina maelezo toka pande mbili Spika kaweka chini ya mto wake! Spika ana maslahi gani kwenye huu mgogoro?

Na kwa nini kodi ya watanzania iendelee kutumika kulipa posho wabunge wakati hawafanyi mambo yanayowagusa wananachi wanaohitaji huduma za afya? Nini maana ya bunge kuwa ndio chombo kikuu kitakachoisimamia serikali? Spika anaongoza bunge kama chombo cha wawakilishi wa wananchi (wakiwemo wagonjwa) au anaongoza kikao cha serikali?
 
Hebu kachukue statistics za vifo ya wiki nzima kabla ya mgomo halaf uje nazo hapa.
walau utaleta hoja ya kujadilika.
 
Tangu mgomo uanze 23/06/2012 wagonjwa 19 wamefariki katika hospitali ya mkoa Mwanza ya Sekou Toure. Akihojiwa na Startv mganga mkuu wa hospital hiyo ina interns 20 ambao waligoma ila hadi sasa 6 wamerejea na kuendelea na kazi,14 wamerudishwa wizarani kwa kuendelea na mgomo.

Source:Startv Habari.

NB:Wewe unajisikiaje kwa watu kufa kwasababu ya mgomo? Najua kuna wengine wanaona nisawa kwakuwa wanavijisent vyakwenda private,lakini jiulize je kama ni ndugu yako kafariki wewe ungejisikiaje? Jamani tuache siasa kwenye afya!

hizo data zipo kisiasa zaidi, je kabla ya mgomo walikuwa wanakufa wangapi?ile tuweze kulinganisha na kuona kama kuna mabadiliko.pia katika hilo ukosefu wa vifaa, madawa umechangia kiasi gani?
 
Ukienda seko ture kama unataka kupiga x ray unaambiwa uende bugando,serekali dhifu huzaa wananchi dhaifu
 
kuna wakati hata kupima vipimo kama vile haja ndogo, mkojo, malaria nk wagonjwa wanaambiwa wakapime maabara binafsi, hapa S.Toure hata Asprin kupata ni shida. Huyo mganga mkuu (ambaye hajagoma) kila mwezi anajilipa zaidi ya sh.milioni tano zinazotokana na michango ya wagonjwa kama pesa za pango (hakuna nyumba ya mganga mkuu, nyumba za serikali ziliuzwa na mzee Magufuli zamani)
Ngoja nitafute picha ya hoteli anamokaa mganga mkuu( ipo jirani na U-turn supermarket)
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom