10th March.... Siku Lilipochuruzika CHOZI LA DAMU!!!

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
216
kama mnakumbuka majuzi niliweka hapa ushuhuda ya rafiki yangu mmoja aliyejikuta akiishi katika mazingura magumu siku na tarehe kama ya leo miaka adhaa iliyopita. la kutia moyo ni kuwa MUNGU ALIINGILIA KATI HISTORIA YA MAISHA YAKE na kwa rehema kuu alimtoa humo na sasa ana ushuhudua wa mafanikio makubwa sana kielimu................ kwa story kamili soma kwenye link hii hapa chuni:

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/55201-sikieni-story-ya-rafiki-yangu-huyu.html

leo ndio kilele cha siku yake hiyo ya ushuhuda. naomba mimi na wewe tutafakari yafuatayo:

1.
je wadau mbalimbali kama wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na jamii nzima wana nafsi gani kuzuia janga hili ? na je wafanye nini?
2.
je, juhudi za serkali kupitia wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto inayo mikakati endelevu ya kushughulikia suala hili la watoto wa mitaani? je ifanye nini?

mwisho natoa ombi kwa wanJF wote kuangalia namna itakayofaa kwa miaka ijayo kujitolea kama sehemu ya huduma kwa jamii kutenga angalau siku oja kwa mwaka kutafakari tatizo la watoto waishio kwenye mazingira magumu na nini kifanyike kupunguza kama sio kumaliza tatizo hli

KAULI MBIU

CHOZI LA DAMU................WAZAZI WAKIAMUA WANAWEZA KILIFUTA

tafadhari sikiliza wimbo kamili wa CHOZI LA DAMU kama ulivyoimbwa na RC-PAROKIA YA MAKUBURI- DSM. wimbo huo unapatikana kwenye website hii ya Jamii Forums (BONYEZA PALIPOANDIKWA "INJILI") na pia kwa maadishi kwenye post #10 kwenye link hiyo hapo juu.

MUNGU AWABARIKI SANA
 
Nimeskiliza mpendwa,yani nimebarikiwa mpaka waliobarikiwa wanasema nimebarikiwa
pole zake nitamfikishia................... umesiiliza lakini ule wimbo? ni mzuri sana, unafikirisha sanaaaa..............
ubarikiwe na Bwana
 
Nimeskiliza mpendwa,yani nimebarikiwa mpaka waliobarikiwa wanasema nimebarikiwa

na ubarikiwe tena na tena................ sifa na utukufu apewe Bwana , aliyeziumba mbingu na nchi.........................
 
""""""Kwa sababu ya mambo haya ndugu zetu wanaumia,
wapo wanaorandaranda mitaani bila makazi,
wengi wamelazimika kuajiriwa bado wadogo,
hawana tena nafasi ya kusoma wapate elimu,
na wengi wanajiuza miili yao ili waishi,
mbona dunia umetugeuka watoto.........................................""""""

eee Mwenyezi Mungu, warehemu watoto wote waishio katika mazingira magumu, wakumbuke wakati wa shida zao, uwakinge na hasira za yule mwovu. Amen..............
 
Pole na hongera zake, sio wote wanaofanikiwa mwengine wanabaki na majonzi maisha yao yote!
Mungu ambariki!
 
1.
je wadau mbalimbali kama wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na jamii nzima wana nafsi gani kuzuia janga hili ? na je wafanye nini?

Watu kibao huwanahangaika kupata watoto, wakishindwa wanaanza kulalamika.Badala yakukaa nakulalamika wa-Adopt watoto wanaorandaranda ili wajaze hizo nafasi zilizo wazi majumbani mwao.
 
Watu kibao huwanahangaika kupata watoto, wakishindwa wanaanza kulalamika.Badala yakukaa nakulalamika wa-Adopt watoto wanaorandaranda ili wajaze hizo nafasi zilizo wazi majumbani mwao.

at least umetoa wazo mbadala............... nashukuru sana.

ila unaonaje kwa mazingira na utamaduni wetu hapa tanzanzania, hayo mambo ya ku-adopt yanawezekana?............ mi naona kama most people wanajisikia proud zaidi kama wanazaa wenyewe na kutozaa naona watu wanaona kama balaa fulani hivi? we unaonaje hapo.............????????
 
Wala hamna cha ajabu, itakua sawa na watu wanavyochukuaga watoto wa ndugu zao nakuwalea.Na kama mtu hataki kuadopt unamlea tu bila kujiwekea kifungo, cha muhimu hapo ni kumpa mtoto nafasi yakuishi maisha ya kawaida .

Kuhusu watu kujiskia proud , kama hana uwezo wakuwa na huyo mwenye damu yake je???Hayo malezi aliyotaka kumpa wa kwake wa damu ampe mwingine ambae tayari yupo na kakosa malezi.
 
kweli ni mawazo mazuri. kwenye nchi za wenzetu hayo mambo ni ya kawaida...........

lakini ni jambo lisiloniingia mimi binafsi kichwani kuzaa mtoto na ukashindwa umpenda na kuhangaika nae, ukamtelekeza hadi kishia mitaani..........

pia naona serkali haijaamua kushughulikia suala hili, ingefanya sensa fulani hivi ingebani watoto wengi wa mitaani wana wazazi na hao wazazi wanatakiwa kubanwa hata ikibidi wakatwe mishahara yao watoto wale wsomeshwe boarding school, yes, si ndio waliowazaaa kwa mapenzoi yao wenyewe?..... wangelazimishwa, kuwajibika ingesaidia kidogo................
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom