05 Julai 2012!

mwangalizi

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
842
512
Sijui nchi hii itakuwa vipi endapo mgomo wa madaktari utakutana na ule wa walimu unaotarajiwa kuanza tarehe 05 Julai! Ee Mungu turehemu Watanzania.
 
Walimu hawajapanga kugoma tar. 05. July. ila hiyo tarehe ndo mwisho wa kusubiri kama serikari in nia ya kukaa meza ya mazungumzo na CWT. Kama hii tarehe itapita, walimu watapitishiwa karatasi kusaini kuamua wanataka kugoma au hawataki kugoma. Baada ya hapo CWT itatoa notice ya kugoma.
 
  • Thanks
Reactions: KUN
viongozi migomo ya walimu waoga. Wakichimbwa mkwara wanatulia.
 
Walimu tunagoma kimyakimya kwa kushusha kiwango cha elimu, kama pesa kidogo tunafanya kazi kidogo. Ndo mana walimu wengi ck hz wanaomba kwenda kusoma halafu wanakwenda kupg job private
chezea walimu weye!!
 
Serikali ya CCM ikitaka kuendelea kuongoza Tanzania vyema mpaka 2015, inatakiwa irudishe madaraka ya nchi kwa wananchi wenyewe. Vinginevyo Mkuu ataendelea kupiga mwereka kila kukicha!
 
Mgomo wa walimu ni hatari kama wa Madaktari kwa kustakabali wa taifa letu. Hawa jamaa wako kwenye mgomo siku nyingi mpaka serikali ikaamua kutaja kuwa div IV ni kufaulu kupunguza makali.
Tanzania mtoto wa masikini atazidi kuwa masikini
 
ajichunge kiongozi wa walim maana nae atajikuta msitu wa pande soon
 
Ikiwezekana Tugome wote tuwaunge mkono madaktari na walimu na sisi wenyewe pia waboreshe shule hospitali na waondoe mfumuko wa bei sababu ziko nyingi za Watanzania kuigomea hii serikali Dhaifu jamani tuhamasishane.
 
Usitulazimishe wananchi wote tugome kwa lipi?? mimi sio mtumishi wa serikali ,mimi ni mkulima ,nimetumia elimu yangu ya juu kwa kilimo na inanipatia faida kubwa sana kuendeleza msisha yangu na ya familia zangu kwa ujumla...kama wewe umeshindwa kutumia akili yao uweze kuishi tafuta njia mbadala ba sio kuwashawishi wengine kwa malengo yako binafsi
 
Usitulazimishe wananchi wote tugome kwa lipi?? mimi sio mtumishi wa serikali ,mimi ni mkulima ,nimetumia elimu yangu ya juu kwa kilimo na inanipatia faida kubwa sana kuendeleza msisha yangu na ya familia zangu kwa ujumla...kama wewe umeshindwa kutumia akili yao uweze kuishi tafuta njia mbadala ba sio kuwashawishi wengine kwa malengo yako binafsi
UNA UNDUGU NA zomba? naona umekoroga juice ya omo, ni povu tu!
 
Last edited by a moderator:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom