Operesheni UKUTA: Kosa jingine la kimkakati la Mbowe na CHADEMA

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Nilifikiri nakutarajia kuwa kuwa Mbowe atatangaza kuwa kuanzia tarehe 01-09-2016 ni siku ya kwenda katika kila kona ya majimbo ya CHADEMA yote na kata na mitaa walizoshinda katika uchaguzi mkuu uliopita kushiriki na wananchi masuala ya maendeleo ikiwemo kuendeleza na kukusanya nguvu ya pamoja katika kuboresha na kujenga miundombinu mipya ya kuchochea maendeleo.

Ikiwa ni pamoja kupiga vita umasikini kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata vyumba vya madarasa, vyoo safi, vifaa vya mashuleni ili waweze kusoma na kuelewa vizuri katika kuleta maendeleo na demokrasia zaidi ndani ya chama ambayo bado ipo chini sana katika CHADEMA ili kukifanya chama kije kuwa na wanamainduzi na viongozi wazuri wa baadaye.

Badala yake Mbowe anataka kuendelea kupambana na polisi na serikali ya Rais Magufuli jambo amabalo litakipotezea muda mwingi CHADEMA na mwisho wa siku hakuna jipya ndani ya chama na kubakia kuitwa chama cha vurugu na maandamano nyasiyo na tija kwa wananchi.

Mwisho niwahusie Mbowe na CHADEMA, wanachotaka kufanya ni kosa la pili la kimkakati badala ya kosa la awali walilolifanya la kukimbia bungeni amabalo halina tija kwa wananchi walalahoi wenyewe.

Mbowe na CHADEMA badala ya kuendelea kufanya makosa ya kimkakati zaidi amabayo hayana tija kwa wananchi waliowachagua na badala yake wanataka kuendelea na maigizo wanayotarajia kuyafanya, CHADEMA haiwezi kufanikiwa kwa kutunishiana misuri na Jeshi la Polisi pamoja na serikali, watafanikiwa kwa kuleta mabadiliko katika majimbo na kata wanazoziongoza ili mradi tu kuonekanane tofauti ya kiuongozi baina yaoi na CCM tu.

Katika hili wanalotarajia kutaka kufanya, hakika sasa pengo la Dr. Slaa limeanza kuonekana live ndani ya CHADEMA na ni bora Lowassa akatafuta njia ya kutoka humo kwa kuwa hawezi kuizuia CHADEMA na siasa za uhanaharakati na hilo litamletea heshima zaidi kuliko kubaki ndani ya chama ambacho hawataki kubadilika.
 
Alafu unalalamika eti nacte wamebana sana mwaka huu. Sasa ulitaka ukasomee cheti cha fani gani kwa uandishi huu???
 
CDM jiandaeni kufa au kuvunjwa miguu, acheni kupambana na serikalini jamani, angalieni watu waliokufa kutokana na harakati zenu, ni kiongozi gani aliyekufa kutokana na harakati zenu?

Najua JPM ame-prove failure kwenye swala la Democracy ila tafutane njia mbadala ya ku-resolve hilo swala, mnaweza kuomba appointment na Rais ili mzungumze hayo mambo badala ya kuwaweka rehani wananchi na vijana ambao watapigwa na kuvunjwa miguu.
 
Yani hamna sehemu yoyote kwenye bandiko lao inayotaja rushwa na ufisadi!!
Yani Chadema wanatuambia Tz hamna rushwa wala ufisadi ila kuna udikteta tu???


Mbowe ajihudhuru kwa kuua chama
Utaanzaje kujadili Rushwa na Ufisadi kwenye Mkutano ambao Edward Lowassa ni mmoja wa wajumbe?
Chadema ya kupambana na Rushwa na Ufisadi ilikufa July 27, 2015
 
hawa umewaambia ukweli lkn watakutukana weeee. ila Luwassa akiona hili bandiko atacheka kimya kimya
 
Wow!UKUTA???? what a joke!wachambuzi waliposema magufuli atawafunika wapinzani na watakosa hoja,nilikua na mashaka kidogo but leo usemi wao una dhihirika!
 
Ushaambiwa...kupanda vyeo chadema kunatokana degree ya ukaidi pamoja na idadi ya kusekwa rumande- Mpendazoe (23 July 2016)
na wewe una recall kauli za wachumia na wanaofikiria kwa kutumia TUMBO?
Very tired Brain, mi nilidhani una nukuu kauli za watu wenye Uzalendo kama wakina Generali Ulimwengu....n.k
 
Back
Top Bottom