Naombeni msaada! Computer yangu Dell Optilex GX620 imekataa kuwaka na kwenye screen ambayo blank na nyeusi kuna message inayosema 'Windows could not open the following file is missing or corrupt: {Windows root}\system32\hal.dll. Please re-install a copy of the above file. Tatizo sijui pa kupata the said file wala cd yoyote! Nifanyeje niweze kuendelea na kazi?
BabaDesi, mimi nimlishapata tatizo kama hili. Hapo huna ujanja Tafuta CD ya windows ufanye re-instalation. Lakini usifanye fresh instalation kwa sababu itafuta kila kitu, chukua option ya Windows Repair
Njia ya kwanza iliyopendekezwa inaweza kuwa nyepesi kwa asiye na uzoefu wa computer troubleshooting. Hata hivyo, njia hiyo itafuta content iliyoko kwenye My Documents hali kadhalika Desktop
Nadhani njia ya pili itasaidia;(Using the Windows Recovery Console) angalia pale mwisho
Last edited by LazyDog; 29th June 2009 at 07:14 PM..
Nitaweza kukupatia cd hiyo kwa bei nzuri ya alfu 45 itakuwa na keys lakini inabidi ukimaliza kuinstall uchomeke katika mtandao kwa ajili ya update ujaze taarifa zako kuanzia hapo itakuwa ya kwako utaitumia jinsi unavyotaka wewe mwenyewe hii cd pia unaweza kuitumia kurepair incase kitu chochote kikienda mramba kinachohusiana na operating system ni sp 2
Shy, na Wakuu wengine, asanteni kwa msaada wenu. Computer imefunguka baada ya kupata CD husika kutoka mmoja wa Wadau wangu. Hata hivyo, Shy ninependa kupata ile genuine CD ya Windows OS uliyosema. Tafadhali niwekee bei yake na mobile namba yako kwenye pm ili nijikusanye kisha nikiwa tayari niwasiliane nawe, unaonaje?
Bado najikusanya ili kupata ile CD ya Window OS aliyosema Shy. Si mnajua tena mambo ya Financial Crisis wameshika chart! Hata hivyo comp sasa imezua tatizo lingine. Ninapoiwasha inaanza na logo ya Dell kisha inafuata logo ya Window kisha inajizima kwa nukta chache halafu inaanza tena mlolongo huo. Kwa kifupi imestuck hapo hapo. Hili nalo ni zao la lile tatizo la mwanzo la OS ama ndio niliuziwa Mbuzi kwenye gunia??
Bado najikusanya ili kupata ile CD ya Window OS aliyosema Shy. Si mnajua tena mambo ya Financial Crisis wameshika chart! Hata hivyo comp sasa imezua tatizo lingine. Ninapoiwasha inaanza na logo ya Dell kisha inafuata logo ya Window kisha inajizima kwa nukta chache halafu inaanza tena mlolongo huo. Kwa kifupi imestuck hapo hapo. Hili nalo ni zao la lile tatizo la mwanzo la OS ama ndio niliuziwa Mbuzi kwenye gunia??
Bila shaka hii ni shida ya OS yako. Ifanyie repair ya window XP kama ndiyo unayotumia.
__________________ If OUR God offends you, then I suggest you consider another part of the world as your new home, because OUR God is part of our culture.
HELP! Nimepata CD ya Windows XP sp2 na katika jitihada za DIY nikajaribu ku-repaire mwenyewe OS yangu lakini nilipofika mahali pa ku-enter chkdsk hakuna kinachoendelea. Kwa vile document nyingi niliisha save kwenye cd nikaamua ku-install upya os yangu. Kosa. Mafaili mengi yakawa yanakataa kuwa installed nikaamua ku-cancel zoezi na kureboot comp. Matokeo yake hata ile logo ya Windows ha4nekani tena na baada ya logo ya Dell screen inabaki nyeusi na upande wa juu kushoto kuna cursor ina flick tu lakini siwezi kuandika chochote. Nafanyaje hapo?? Lengo langu kusolve tatizo langu kwa msaada wa hapa hapa home of great thinkers
Jaribu kufuata yaliyoelekezwa hapo juu kurepair, ukireinstall utapoteza data na software ulizoinstall. Ukiamua kuchukua option ya kureinstall hakikisha unazo cd za software zako vile vile ubackup data.
Jaribu kufuata yaliyoelekezwa hapo juu kurepair, ukireinstall utapoteza data na software ulizoinstall. Ukiamua kuchukua option ya kureinstall hakikisha unazo cd za software zako vile vile ubackup data.
...Nimeamua ku-reinstall upya. tatizo ninalopata sasa ni kama ulilosema. nimepoteza software nyingi zilizokuwemo. Pia kila baada ya muda fulani, kwenye screen kulia chini kunakuja meseji kwamba 'Windows was unable tu save file xxxxx. The data has been lost'. Hii ni kwa nini? pia baada ya kumaliza ku-reinstall sasa ninapooweka DVD ilikucheza picha ama muziki napata mesage ya 'Windows cannot play disc because a Compartible DVD Decorder is not Installed in your Computer'. nafanyaje hapa??