Wakuu sijui kama mmeshtukia kuwa Internet Service Providers kwa Tanzania speed imeshuka ghafla tangu Jumamosi (24/April/2010); mimi tatizo hili nilianza kulihisi na kubadilisha connections bila mafanikio.
Leo nimelazimika kuwasiliana na TTCL ambapo sikupata response yoyote, nikawasiliana na VodaCom wakani-hold mpaka nikajikuta nakata simu tu; Zantel nilipowasiliana nao wamenieleza hivi:
"We are very sorry for this, there is an outage on SEACOM since Saturday and we do expect this issue to be resolved today"
Nilipouliza kama ni kwao pekee wakasema ni kwa wote ambao wanatumia Fibre Cable ya SEACOM.
Sijui kama wakuu wengine mmekumbana na issue hii. TTCL kwangu ilikuwa ina-connect lakini hakuna response kwenye browser.


Reply With Quote




If you love something, set it free; if it comes back.....its yours,... 
Follow Us Here