Joomla , Mambo , PHP PostNuke, TikiWiki, Xoops, b2evo zinaweza kupatikana kila sehemu katika mtandao haswa kupitia search engine na kama unajua tovuti zake au watu wanaotumia hizo vitu haswa katika forums na midahalo mengine zote hizi ni open source zinatumika katika ujenzi wa mambo kadhaa mtandaoni haswa katika tovuti . Nyingi ya programu hizi ni za bure zinatolewa kwa leseni maalumu , hii inamuwezesha mtumiaji aweze kutumia codes jinsi anavyotaka yeye kama kuongeza na kufanya mambo mengine .

Je kuna siri gani nyuma ya mafanikio haya ya open source , manake open source sasa inatumika na inazidi kupendwa zaidi kuliko wakati wowote ule na umaarufu wake unazidi kuongezeka , utumiaji wa open souce una faida zake kivitendo , tunaweza kujadili kidogo kama unapenda

Kwa kampuni ndogo au ambazo ndio zinachanua , kuna gharama sana haswa kama unataka kutumia programu katika kuendesha baadhi ya mambo yako hizi programu ni gharama wakati mwingine unahitaji watu wakufundishe au kutoa ujuzi wao kwako gharama zinaongezeka zaidi lakini unaweza kuondokana na gharama nyingi zaidi kwa kutumia programu za open source ambazo ni bure na raisi kutumia kwa mahitaji yako .

Katika ulimwengu wa programu za open source code ziko wazi na bure zinamwezesha mtumiaji kufanya mabadiliko na kukidhi mahitaji yake pengine yote , kama ukitumia pia unaweka mchango wako katika kuendeleza hiyo programe kwa kufanyia mabadiliko .

Pia unaweza kupata msaada wa bure na bila gharama za ziada kutoka kwa watumiaji au waendelezaji wa hizi programu za open source haswa kama unashiriki katika majukwaa yao kwa njia ya mtandao , wewe ukipata tatizo ukisaidiwa ndio njia moja wapo ya kuiendeleza programu hiyo zaidi .

Katika maendelezo ya codes na vitu vingine , zile code za mwanzo hazifutiki au kufutwa au wakati mwingine unaweza kufuata lakini hapo hapo utakuwa unatengeneza aina nyingine ya programu kwa kufuata mkondo wa programu ya kwanza wakati mwingine bila kujua kwa sababu unapenda kufanya programu hiyo ifanye yale unayotaka wewe .

Jumuiya ya watumiaji wa open source inafurahia sana kwa kuifanya iwe kubwa zaidi na kufanya programu hizi ziweze kutumika zaidi wakati huu ambako watu wengi wanahitaji huduma zao , kwa mwanga huu wa open source unaweza kusema sasa , siku za programu zinazouzwa bei ghari zinahesabika au ziko ukingoni .
Lakini zinahitaji muda katika kuzitengeneza , kuzifanyia majaribio na matumizi yake kwa ujumla , na kama huna muda basi una njia mbili za kufanya chagua moja

1 ) Nunua Programu za gharama

2 ) Au , jisajili katika webhost mzuri ambaye ataweza kukufanyia shuguli zako na kukupa msaada programu yako ikipata tatizo au kuwa katika mshike mshike au jiandae na gharama nyingi za kuita wataalamu kila siku kuja kuondoa bugs na vitu zingine .