namna gani niepuke hizi message za promotion kwenye simu yangu. In box inajaa kilasiku.
si ajabu kuwa wengi hili linawaudhi ila hawana jinsi ya kuepukana na nalo. Na kama una simu ya laini mbili ni adhabu tosha.Matangazo ya promotion kila dakika hadi simu inajaa na unashindwa kupata message zako za maana. Hii ni kwa karibu makampuni yote ya simu. Hivi hakuna njia ya kuweza kublock hawa jamaa waache kutusumbua? Bahati mbaya vyombo vyetu vya udhibiti vimelala usingizi mzito. Kama simu ni ya kwangu, sidhani haya makampuni yana haki ya kuitumia wanavyotaka eti kwa sababu natumia laini `yao` ambayo kimsingi naimiliki kwani nimeinunua. Wana JF ebu fanyeni mautundu tuepukane na vurugu za haya makampuni ya simu kwani regulators hawana ubavu wa kupambana nayo.
Wakati mwingine upo kwenye jambo la maana unaona simu inaita na unaamua kusitisha ukaisikileze, na unaishia kupokea promotion.
Re: namna gani niepuke hizi message za promotion kwenye simu yangu. In box inajaa kilasiku.
Si bora hiyo ya msg, airtel na voda wameanzisha mtindo wa kuwapigia wateja wao simu mteja unakimbilia kupokea ukidhani ni simu ya muhimu lahaula lakwata!!!!!!! eti unapewa maelekezo jinsi ya kuchagua wimbo khaaa mimi siku hizi huwa nawakatia hapo hapo manake ni ujinga kabisa ! Inabidi mamlaka ya mawasiliano itusaidie kwenye hili tunakerwa sana na hii mitandao ya simu !
Re: namna gani niepuke hizi message za promotion kwenye simu yangu. In box inajaa kilasiku.
Kudelete ni moja ya mazoezi ya kuustua ubongo na kuufanya uwe active. Punguza magonjwa kwakufuatilia hii system. Yaani inbox inajaa hata haudiliti uko bize na monotonous jobs za ofisini? Kweli watanzania ni wazembe sana yaani mpaka msg unaishtakia JF?
Re: namna gani niepuke hizi message za promotion kwenye simu yangu. In box inajaa kilasiku.
Unalichowasilisha sweetlady nakubaliana nacho hasa! Imekuwa kero!!! Binafsi huo mtindo wa VODA na TIGO
kupigia wateja simu kwa ajili ya matangazo yao unakera sana! Nadhani message sent Lol.
Pole sana wa JF hata mimi nakeleka sana, nina bb na samsung yenye line 2, ina option ya kublock sms. By subject,phone number, name or by address etc but for this case of promotions messages by Address ndo mwarobaini tosha.
Kudelete ni moja ya mazoezi ya kuustua ubongo na kuufanya uwe active. Punguza magonjwa kwakufuatilia hii system. Yaani inbox inajaa hata haudiliti uko bize na monotonous jobs za ofisini? Kweli watanzania ni wazembe sana yaani mpaka msg unaishtakia JF?
Kwani kaishtaka ama kaomba njia ya kublock hizo sms, mbona watakakujifanya mgumu wakuelewa?
Never reply coz these are automated messages.
The best u can will depend with type of ur hand set. Just block them by either. Address or topic/subject. Samsung can.
Follow Us Here