Hallo wadau,
naomba msaada nataka kujiunga na bundle ndogo kabisa ya internet ya vodacom , inaanzia na shillingi ngapi? nimeona airtel wao wako safi sana Tshs 2,500/= tu unapata MB400 mwezi mzima. naomba msaada kwa anayefahamu vodacom wao wamekaaje?
Hallo wadau,
naomba msaada nataka kujiunga na bundle ndogo kabisa ya internet ya vodacom , inaanzia na shillingi ngapi? nimeona airtel wao wako safi sana Tshs 2,500/= tu unapata MB400 mwezi mzima. naomba msaada kwa anayefahamu vodacom wao wamekaaje?
Nisipofikia Malengo Yangu basi sisitahili kuishi duniani.
The signature you are looking at now does not exist.....
Toa maelezo ya kutosha basi mkuu!
Nisipofikia Malengo Yangu basi sisitahili kuishi duniani.
bundle ya chini kabisa kwa voda ni mb 20 ambayo ni shs 500 na unalipia kwa siku. Ila wana ya Mb 50 ambayo ni shs 2000 na ni siku 30.
Bonyeza *149*01# utapata maelezo ya kutosha.
Fuata maelezo kwa makını walıyokuambıa
mkuu inategemea na matumizi ya watu...mi siipendi sana voda ila internet yao natumia vizuri tu...bomba 30 nikiweka tunatumia office nzima (zaidi ya watu 10) kwa pamoja(nimei feed into router) na nadowload games and muvies mpaka karibu 100GB kwa mwezi (juzi tu nimemeliza ku download fifa 11<6.3GB> baada ya kumaliza kudownload muvi kama tatu hivi za 2GB kila moja ingawa natumia torrents na zinatumiamda mrefu kidogo ila napata ninachokitaka na pamja na kuwa nadowload bado watu wengine wanapata net safi tu kwa shughuli zingine za kila siku bila tatizo lolote na speed ni saaafi tu tofauti na mitandao mengine ambayo unapewa kiasi flan cha bandwith na kikiisha you are doomed!!
The signature you are looking at now does not exist.....
dah natumia sasatel wananlamba kinoma,zaidi ya mara mbili nimenunua 5000 kwa 200 mbt wamesema unatumia week badala yake inaisha 1 hr.nikiwaambia wananchekea tu
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, voda ina afadhali. Kama una hofu na mambo ya bundle jaribu, bomba. Bomba 30 kwa mfano unapewa 2GB, ukimaliza unarudi kwenye 64kbps mpaka siku zako 30 ziishe. Hata hao TTCL wanaonekana nafuu wanatoa 2GB kwa mwezi bila nyongeza. Mwacheni ajaribu na kuona mwenyewe.
The signature you are looking at now does not exist.....
Nimejaribu internet za makampuni mengi ZANTEL spidi ni nzuri ila wana limit ya bundles na masharti ya utumie muda flani wa maongezi kwenye simu kwanza kwa wale wanaotumia Highlife.TIGO ovyoo spidi na mtandao vimeoza kabisa siku hizi hakuna mtandao,AIRTEL sio poa na SASATEL spidi ni nzuri sana.
VODA kwa bundle ndogo ndogo kama cheka internet ni wizi mtupu ila HIZI BOMBA services zao ni nzuri sana ni unlimited downloads.Kujiunga BOMBA YA WIKI tuma neno BOMBA 7 kwenda 15300 kwa elfu 10 tu utapewa 750 mb kwa spidi ya ajabu kisha itapungua kidogo kwwa siku zako 7 ila ni bomba kama neno lenyewe lilivyo.Vile vile kuna Bomba 30....
to make things clear..ukiandika BOMBASPIDIunapewa bundle kama 1.5 gb hivi but at high speed up to 300kb/s...ila uiandika BOMBA7 unapewa 700mb at high speed then wanakuswitch at low speed(64kb/s) but unlimited downloads adi wiki iishe..voda wako cheap jaman,sema haka ka speed wanakabana so inabidi utumie torrents
Mnafanyia VODA Marketing, au ni damage controll?. Voda ni hakuna kitu! You will live to tell.
Independent thinker
Humu jf baadhi yetu wametengeneza haki miliki ya they way they think, you have to think like them and have drawn a line of where one has to belong, you are either "with us" or "against us", if you don't sail the same boat then you are an enemy!. -Pasco wa JF
Follow Us Here