Leo hasubuhi clouds kipindi cha magazeti nimesikia waziri wazamani wa mambo ya ndani ameenda ofisini kwa mbunge wa mwanza nymagana na kung`oa vitasa na kubeba picha ya rais kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe..
Je imekaaje hii?
Leo hasubuhi clouds kipindi cha magazeti nimesikia waziri wazamani wa mambo ya ndani ameenda ofisini kwa mbunge wa mwanza nymagana na kung`oa vitasa na kubeba picha ya rais kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe..
Je imekaaje hii?
Last edited by MONTESQUIEU; 30th November 2010 at 08:58.
Masha ang'oa vitasa ofisi ya Mbunge Mwanza
Tuesday, 30 November 2010 01:46
Frederick Katulanda, Mwanza
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amehamisha vifaa mbalimbali vya ofisi ya Bunge Jimbo la Nyamagana, kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe kipindi uongozi wake. Akizungumza na Mwananchi jana, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, alisema baada ya kutoka Bungeni alikwenda kuingia katika ofisi hiyo, lakini baada ya kukabidhiwa alikuta vitasa vya mlango, simu ya mezani picha ya Rais na samani za kukalia vikiwa zimechukuliwa.
Kwa mujibu wa Wanje, baada ya kufuatilia aliambiwa kuwa vifaa hivyo viliondolewa na Masha kwa madai kwamba, alivinunua kwa fedha zake mwenyewe.
“Nimefuatilia kwa DAS (Katibu Tawala wa Wilaya) nikaambiwa amechukua Masha, nikafuatilia kwa Katibu Tawala wa Mkoa yeye alijibu kuwa naye alifuatilia suala hilo kupitia kwa Das na kupewaa majibu kama yangu, sasa sijajua ni kwa nini, ninavyojua ofisi haipaswi kukosa samani kwa vile kuna fedha za kununulia vitu hivyo,” alisema.
Kwa Upande wake, Masha alikiri kuondoka na vitu hivyo na kwamba, asingeweza kuacha vifaa vyake binafsi katika ofisi hiyo.
Masha alisema vifaa alivyoondoka navyo ni vile tu ambavyo ni mali yake.
“Wakati naingia hapa nilikuta ofisi ikiwa na kiti kimoja na meza tu, vifaa vingine niliweka vyangu, kama kompyuta na meza zake, simu na samani nyingine kulingana na mahitaji yangu,” alisema Masha.
Alisema Wenje anapaswa kuwasiliana na ofisi ya mkuu wa wilaya, ili kupewa vifaa vya ofisi hiyo ambavyo yeye aliviondoa alikuwa havitumii kwa vile wao wanajua vilipo.
“Jamani vifaa vya ofisi anapaswa kuuliza ofisi ya mkuu wa wilaya, sasa kama anataka nimwachia na vyangu binafsi, mie nimetoa vyangu…hivyo vya ofisi vipo, nadhani amefika na kukutana na kiti kimoja na meza vile vingine vilivyokuwemo pia vilikuwa mali ya ofisi,” alieleza Masha.
Hata hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza (RAS), Doroth Mwanyika, hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa nje ya ofisi, lakini ofisa mmoja wa ofisi yake alithibitisha kuwepo kwa malalamiko ya Wenje na kwamba, yalikuwa yakishughulikiwa.
Source: Mwananchi
hii iunganishe na ile inayo muonelea Masha.
Ni utoto tu,akikua ataacha.
Kafulia huyoooooooooooooooo!!!!!!!!!!
A question that sometimes drives me hazy: am I or are the others crazy?
do kali kwelikweli ni huyu mwanasheria na aliyekua waziri? etiiiiiii
Sasa kama tunamruhusu mtu binafsi aeke vitasa vyake katika ofisi ya serikali tunategemea nini? Panatakiwa ipitishwe sheria kuwa mtumishi atatumia samani na vifaa alivyovikuta na kama ataingiza vya kwake itakuwa kama mchango wake na hataruhusiwa kuondoka navyo muda wake wa utumishi utakavyoisha.
Amandla.........
Fundi Utumbo
Hii ndio aina ya Viongozi tunaowapa dhamana ya Kutuongoza. Kwani angeviacha angepungukiwa na nini? Usikute siku alipoviweka kulikuwa na sherehe ya kumshukuru kwa mchango wake!
Sema Kwa Sauti, Mimi Ni Mweusi Na Najivunia Kuwa Hivyo!
Ni vituko tu vya huyu jamaa!siasa siyo ugonvi!asiyekubali kushindwa si mshindani!
Hivyo vitu vingine kama vyake anaweza kundoka navyo ila kiukweli kutoa vitasa ni uharibifu wa makusudi.
Unajua alishaona kuwa ofisi ni yake milele,hakujua kama cheo ni dhamana
upuuzi hivyo vifaa si aliviandikia vocha kwa taratibu za kiserekali na akalipwa? sasa kuchukua kunaonyesha alivyo fisadi
Embu tukagulieni na ofisi ya Waziri usikute pia amekomba kila kitu
Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
"The important thing is not to stop questioning" - Albert Einstein
sheria ichukue mkondo wake
"Each generation must, out of relative obscurity, discover its mission, fulfil it, or betray it"/Kila kizazi, katika utata wa kipindi chake, lazima kiutambue wajibu wake na kiutekeleze au kiusaliti - Frantz Fanon
Hahahahhahhahahahhahahhah,Mash aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa a!!!!!!!!!!
Malecela aling'oa mashine za maji kule Mtera baada kushindwa na bw Lusinde! Nadhani ni kawaida ya wapenda madaraka.
uh. mods unganisha hii na ile nyingine ya masha.
" If you hear a voice within you say "you cannot paint", then by all means paint, and that voice will be silenced"
[email protected]
huyo bado ana machungu kukikosa kiti cha ubunge
Follow Us Here