Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

    Report Post
    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 117
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,512
      Rep Power : 46712
      Likes Received
      16401
      Likes Given
      8461

      Default Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Tunataka kutetea demokrasia na utawala wa demokrasia, hivyo hatuwezi kuwa wa kwanza kupendekeza njia zisizo za kidemokrasia kushughulikia matatizo ya kidemokrasia. Tupo ambao tumechukizwa, kukerwa na kuumizwa na jinsi ambavyo matokeo ya uchaguzi mkuu katika ngazi zote yalivyotolewa na yanavyoendelea kutolewa na hasa mahali tulipofikia vijana wetu kulazimika "kulinda kura". Wapo ambao wanaona kabisa kuwa baadhi ya watu waliotangazwa au watakaotangazwa washindi wamekosa uhalali wa nafasi hizo.

      Pamoja na ukweli wa hilo siku za karibuni kuanzia mvurugano wa Tume na Matokeo ya Uchaguzi nimefuatilia wapo watu wamejiunga ghafla ghafla au wengine wa muda kidogo ambao wamekuja na siasa kali za kutaka kutumia JF kama jukwaa la kuanzishia itikadi ya nguvu dhidi ya utawala wa kisiasa (violence against public officials).

      Mimi binafsi nikiwa ni muumini wa nadharia ya nguvu ya hoja siungi mkono hoja za nguvu kwani katika kutumia hoja za nguvu kunathibitisha kuwa umeshindwa kutumia nguvu za hoja kuweza kuwashawishi watu wengine. Lakini ukweli ni kwamba, hadi hivi sasa tumeweza kwa kutumia hoja tu kujenga hoja na kuwashawishi mamilioni ya Watanzania kuchagua mabadiliko. Hatuna sababu ya kubadili mbinu hiyo sasa hata kama tunajisikia hasira kiasi gani.

      Binafsi napinga na kulaani vikali kauli zinazotolewa aidha kama entrapment ya JF au kutoka moyoni kweli yenye kuashiria kuwa ni bora kutumia nguvu kuweza kupata matokeo ya kisiasa. Tulipoanza JF miaka michache iliyopita hatukujua kuwa uongozi wa kisiasa ungekuwa ulivyo, lakini tumeweza kupita katika misukosuko mingi ya kitaifa na tumeweza kufika leo tumeshuhudia mabadiliko makubwa na ushindi usiokadirika wa upinzani Tanzania na hivyo kusababisha malango yaliyofungwa kuachia. Huu ni ushindi wa hoja si vitisho.

      Kama kundi ambalo baadhi yetu tunajiita au tunaitwa wasomi, ni lazima tuwe tayari kutetea hoja zetu nakutumia ushawishi wa hoja kuweza kupata matokeo ya kisiasa. Ninachosema ni kuwa tuwakatae kwa hoja wale wote wenye kujaribu kutushawishi au kutoa kauli za matumizi ya nguvu kama "laiti ningekuwa sniper", "tuwapige risasi"n.k ili waone kama kuna watu wataunga mkono - na inasikitisha wapo wanaounga mkono.

      Kwa kufanya hivyo, tunaweka mtandao wetu tuupendao hatarini kwani kikiwa ni chombo kilichoandikishwa na licha ya watu kutumia majina mbadala endapo jambo fulani linatokea mtandao huu una wajibu wa kushirikiana na vyombo vya kiusalama kutekeleza amri halali ya mahakama kuweza kuwapata wahusika. Sasa tusichukulie kimzaha tunapotoa kauli zenye mfanano wa vitisho, kauli hizo hazilindwi na "uhuru wa maoni" kwani ni kama ilivyosema "kupiga kelele moto, kwenye ukumbi uliojaa".

      Hivyo, kwa wale ambao tumekasirishwa sana na matokeo, tujitoe zaidi kujipanga katika vyama tunavyovitaka au kushiriki kuunga mkono au kuwasaidia wagombea waliochakachuliwa matokeo yao. Mtu akitoa kauli yenye mwelekeo wa vitisho kwa viongozi wa umma - haijalishi kama ni wa chama tawala au upinzani - nawaomba tuflag comment hiyo na kuwataarifu ma MOD mara moja. Tusidhania MODs wanasoma kila sentensi ya kila thread ya kila mtu kila siku. Tuwe walinzi wa forum yetu sisi wenyewe kwani ninaamini katika siku zijazo tutahitaji chombo hiki kuendelea kuwepo.

      Tukumbuke kuwa ufisadi bado upo, mgongano ndani ya CCM upo na changamoto mbalimbali za kitaifa bado zipo. Hivyo, ni kwa maslahi yetu sisi wenyewe wanachama, wageni, na mashabiki kuulinda mtandao huu kutoka kwa watu ambao wengine naamini ni political operatives wa baadhi ya watu ambao kazi yao ni kupandikiza hoja za kichochezi ili JF itajwe (kama mnakumbuka Feb 2008) kuwa ni mtandao wa kighaidi au kichochezi. Maana ikifanyika hivyo wengi hutimka na kukaa pembeni huku wachache vichwa vyao vikiwekwa katika kamba za wanyongaji.

      Tujiwajibishe wenyewe, tuilinde forum yetu..

      Napendekeza.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    2. RukaaJuu Final

    3. #21
      KipimaPembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th August 2007
      Posts : 772
      Rep Power : 761
      Likes Received
      338
      Likes Given
      130

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Kwa wachangiaji wengi makini hapa JF hiki kilikuwa kipindi cha kupumzika kwa sababu kuna wengine wameigeuza forum kuwa battleground pengine kwa kujua au kutojua! Kwa kweli michango mingi humu ndani wakati wa kampeni na wakati wa matokeo ilikuwa terrible na unaweza kusema uhuru wa habari uliopitiliza kama ulioonekana humu unatia kichefu chefu. Watu tuna tofauti, lakini viwango vya ustaarabu havitofautiani sana.

      Vile vile kuna watu wameamua kutumia kipindi hiki cha uchaguzi kuchafua hali ya hewa na kuifanya social media kama Jamii Forums ionekane kama kitu kisichofaa! Pengine hawa walikuwa wengi sana kipindi hiki, na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwa-put off watu wengi wanaoiona jamii forums kama channel muhimu ya kupata habari na fikra huru zisizo-haririwa.

      Mimi nashauri members wapya sana wawe wanapewa nafasi ya kuona content tu bila kupewa ruhusa ya kuchangia. Member mpya akisajiliwa awe anapewa kama One month ya kukaa kama observer kabla ya kuruhusiwa ku-post kitu chochote kwenye forum. Nahisi kuna watu humu wakiona hoja zinazowashinda hukimbilia kujisajili kwa ID mpya na kuvuruga mijadala yenye hoja hizo. Hili linawezekana kutokana na urahisi wa kujisajili upya na kuanza kuchangia. At least masharti haya yanaweza kuwekwa katika baadhi ya majamvi tu, sehemu kama mapenzi na mahusiano watu waruhusiwe kujimwaga.

      Ni kweli mijadala mingi isiyokuwa na lugha za kistaarabu inavuruga sana forums na kufanya wale wanaoitegemea kuchukia na kutafuta alternative source.

      Siasa ni mchezo msafi, kwani siasa hutoa viongozi wanaotakiwa kuwaongoza watu. Si ajabu kuwa nchi yetu inaendelea kuzama katika lindi la umaskini, ikiwa tunaendelea kuichukulia siasa kama ni sehemu ya kutumia hila, fitna na uzandiki kiasi cha watanzania kuaminishwa kuwa siasa ni MCHEZO MCHAFU. Mchezo mchafu, hauwezi kutoa washindi wasafi. Taifa linatakiwa kuongozwa na watu wasafi. Lazima tuseme kuwa siasa zetu tunaziendesha vibaya ndo maana matokeo yake ni mabaya kwetu wote.

      Tunataka mabadiliko, lazima tutumie njia safi ili kujitenga na wanaotumia njia mbovu. Tunajua fitna na hila zitaendelea kuwepo na kwa kipindi fulani zitaonekana kushinda. Lakini dawa yake ni kuzikataa hila na fitna sehemu yoyote tunapopata nafasi ya kufanya hivyo, hatimaye ukweli utasimama. Kujaribu kumuondoa nyoka ndani ya nyumba kwa kuichoma moto inaweza isiwe uamzi wa busara sana!

    4. #22
      engmtolera's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st October 2010
      Posts : 3,610
      Rep Power : 1332
      Likes Received
      780
      Likes Given
      655

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      ulichokisema mwanakijiji ni cha ukweli hatupingi,ila utambue kuwa ni matokeo ya wizi na mwenendo mbaya wa uongozi wa hii tz ndio unawafanya watu kuwa na hasira hadi kutumia hoja zenye hasira ndani yake,kwani kumbuka,ni hatari sana kumfanya mwenzako ni mjinga na akatambuwa kuwa wa mfanya yeye ni mjinga kitakachotokea ni kile ambacho baadhi wanajamii forum wanakitoa sasa,ni kweli tunahitaji kubadilika ili tuiweke JF Katika mazingira salama

      MAPINDUZIIIIIIIIIIIII DAIMAAAAAAAAA

    5. #23
      Pelosi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 22nd July 2010
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 77
      Rep Power : 464
      Likes Received
      4
      Likes Given
      33

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      ahante MMKJJ, hili limekuja wakati muafaka na imezidi kunidhihirishia kuwa kimya kingi kina mshindo mkuu!

      Haya tusonge mbele tena kwa busara na maarifa, hii nguvu tuliyo nayo isiishie hapa bali haya yaliyokusudiwa kutukatisha tamaa yawe chachu ya mema na makubwa zaidi!

      JOY COMES WITH THE MORNING.... KUMEKUCHAAAAAAAAAAAA!!!

    6. #24
      Ngolinda's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 12th April 2010
      Location : Chile
      Posts : 114
      Rep Power : 489
      Likes Received
      23
      Likes Given
      35

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Naunga mkono hoja na pia nakupongeza MKJJ.
      A wise person does at once, what a fool does at last. Both do the same thing; only at different times.

    7. #25
      chanai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th October 2010
      Posts : 280
      Rep Power : 493
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      That's great.

    8. Miaka 50

    9. #26
      George Maige Nhigula Jr.'s Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2008
      Posts : 464
      Rep Power : 667
      Likes Received
      142
      Likes Given
      235

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Ndugu Wana JF,

      Naunga mkono hoja, mi nadhani ingewezekana kuwe na utaratibu kila Mwezi au kila wiki MOD awe anatoa list ya watu waliokiuka maadili ya uchangiaji tuwakanye na wale waliokuwa na mchango mkubwa itolewe list yao then tuwapongeze.

      Utaratibu huu utatusaidia kuweza kuwa objective na kuwa na self evaluation ya jinsi tunavyotoa michango yetu humu ndani.

      Nashukuru sana
      "We cannot walk alone, we must pledge once more to march into the future. Let us keep that promise and in the words of Scripture hold firmly, without wavering to the hope that we confess."

    10. #27
      Mp Kalix2's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th October 2010
      Posts : 513
      Rep Power : 540
      Likes Received
      106
      Likes Given
      50

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Quote By EXECUTIVE

      Utaratibu huu utatusaidia kuweza kuwa objective na kuwa na self evaluation ya jinsi tunavyotoa michango yetu humu ndani.
      Naunga hoja ya MMKJ 100%.

      Na pia hapo kwenye Red hakuna haja ya kumpa MOD kazi hiyo. Kazi hii ya kuchambua wote waliopitiwa/kuzidiwa na jazba na kutoa matusi na lugha za uchochezi inaweza kufanywa na sisi Members bila kupoteza muda wa MOD.

    11. #28
      Baba_Enock's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2008
      Location : Bunju "B"
      Posts : 5,818
      Rep Power : 1900
      Likes Received
      1162
      Likes Given
      977

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Napinga hoja!

      Mabadiliko ya Uongozi wa Siasa katika nchi yetu hautapatikana kupitia "Ballot Boxes"...PERIOD!

      Lazim itumike njia mubadala kurudisha heshima katika jamii
      Ad Majorem Dei Gloriam - "For the greater glory of God"

    12. #29
      Ferds's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th October 2010
      Posts : 878
      Rep Power : 610
      Likes Received
      27
      Likes Given
      153

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Ucmtishe ndugu Melo, hakuna mtu atakayeishi kwa tabu mimi naunga mkono hoja zote za wachangiaji wa maneno ya busara ya mwanakijiji, ukweli ni kuwa ktk forum hii tulijikita zaidi kiupnzani tukasahau kuwa hii ni part ya media, na ilitakiwa isiwe na bias sas sisi tukawa biased, anyway whatever happened in the electin months happened with reasons aliye na masikio na asikie na mwenye macho atazame.

      Tulio great thinkers tuendelee kutoa na kuchangia hoja, tupunguze jazba, kufungiwa ndugu notradamme tutafungiwa wengi tu kama hutuleti habari zenye ushahidi
      OLESAIDIMU likes this.

    13. #30
      Njowepo's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 26th February 2008
      Location : Santiago
      Posts : 7,624
      Rep Power : 22060
      Likes Received
      1001
      Likes Given
      793

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Am still pondering your message
      WB Tanzania lead economist Jacques Morisset said the GDP doubled in 10 years, but it has failed to produce any significant decline in poverty levels.

    14. #31
      Bigirita's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Under a mango tree
      Posts : 11,263
      Rep Power : 3043
      Likes Received
      3054
      Likes Given
      4137

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      MMKJ,
      asante kwa kuni-quote.
      Nilichosema nimekimaanisha. Unajua vema kwamba wewe na institution yako inaweza kutengeneza taswira ya mambo lakini inaweza kupenya kwenye vichwa vya watu wachache sana. "thanks" za jf zisikutie kiburi.
      We know you better.........support yako ya kifiki kwa wana-mageuzi wa nchi hii tunaijua vyema. Wewe si ndio ulikuwa muasisiwa CCJ katika dakika za mwisho za kueleka uchaguzi mkuu? kiliposambaratika ulikuja na hoja gani? CHEAP.

      Taarifa zako za Meremeta ulizoleta hapa zilikuwa zinamsaidia nani? ulijaribu kuonyesha kuwa Meremeta ni swala kubwa kuliko tunavyoweza kufikiri, point yako ni kwamba, it is a global issue, na inahusisha watu amabo kimsingi hatuwezi kuwafanya chochote. ILIKUWA NI REPORT YA KUTUKATIZA TAMAA SISI WATANZANIA tusiendelee kuhoji tena Meremeta.

      Naweza kuendelea lakini, haina maana. Kama unataka nipige IP ban!
      * LOVE COMES NATURALLY; HATE IS TAUGHT.....by nngu007 wa JF

    15. #32
      Chapakazi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th April 2009
      Location : Kathmandu
      Posts : 2,910
      Rep Power : 1096
      Likes Received
      256
      Likes Given
      272

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Huwezi kuibiwa alafu useme tujenge hoja zenye msingi! We are simply stating the facts and reflect our emotions. We speak the truth and we dare to speak openly! Hizo hoja za itikadi ya nguvu ni zipi?
      Change begins with YOU

    16. #33
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,512
      Rep Power : 46712
      Likes Received
      16401
      Likes Given
      8461

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Tayari wana mabadiliko tumefanya vizuri sana kwenye uchaguzi huu, hakuna mtu mwenye sababu ya kutembea kichwa kainamisha chini au kujaribu kujisikia vibaya; ukisukuma mlango ambao wao wanausukuma usifunguka na ukafanikiwa kuuachia, basi kumalizia ni juhudi kidogo tu. Malango yametikisika, na mlango umeachia.. sasa tusije tukajikuta tunapoteza muda wakati wao wanaubamiza tena dhidi yetu.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    17. #34
      Chapakazi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th April 2009
      Location : Kathmandu
      Posts : 2,910
      Rep Power : 1096
      Likes Received
      256
      Likes Given
      272

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Tayari wana mabadiliko tumefanya vizuri sana kwenye uchaguzi huu, hakuna mtu mwenye sababu ya kutembea kichwa kainamisha chini au kujaribu kujisikia vibaya; ukisukuma mlango ambao wao wanausukuma usifunguka na ukafanikiwa kuuachia, basi kumalizia ni juhudi kidogo tu. Malango yametikisika, na mlango umeachia.. sasa tusije tukajikuta tunapoteza muda wakati wao wanaubamiza tena dhidi yetu.
      wabunge 20 ndo success?
      Change begins with YOU

    18. #35
      chuwaalbert's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th September 2010
      Posts : 295
      Rep Power : 499
      Likes Received
      52
      Likes Given
      129

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Mzee, Mwana wa Kijiji, nakuunga mkono. Utamu wa mjadala ni kujadili HOJA ya mtu bila JAZBA, bali kuzingatia mantiki, mtiririko na ufinyu (weakness) katika hoja inayojadiliwa, bila kuwa na uharaka wa kutumia NGUVU za mwili kwa kutumia maneno. Napenda kuwaomba wachangiaji wenzangu kujenga hoja katika kupinga hoja! nakushukuruni.

    19. #36
      King of Kings's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2010
      Location : KWA MBAYUWAYU
      Posts : 3,765
      Rep Power : 1221
      Likes Received
      430
      Likes Given
      818

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Asante sana MwanaKijiji well said

    20. #37
      khoty's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Posts : 64
      Rep Power : 446
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      mwisho wako wa kufikiri, pole

    21. #38
      Fundi Mchundo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2007
      Posts : 4,351
      Rep Power : 2678
      Likes Received
      194
      Likes Given
      136

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Quote By Bigirita
      MMKJ,
      asante kwa kuni-quote.
      Nilichosema nimekimaanisha. Unajua vema kwamba wewe na institution yako inaweza kutengeneza taswira ya mambo lakini inaweza kupenya kwenye vichwa vya watu wachache sana. "thanks" za jf zisikutie kiburi.
      We know you better.........support yako ya kifiki kwa wana-mageuzi wa nchi hii tunaijua vyema. Wewe si ndio ulikuwa muasisiwa CCJ katika dakika za mwisho za kueleka uchaguzi mkuu? kiliposambaratika ulikuja na hoja gani? CHEAP.

      Taarifa zako za Meremeta ulizoleta hapa zilikuwa zinamsaidia nani? ulijaribu kuonyesha kuwa Meremeta ni swala kubwa kuliko tunavyoweza kufikiri, point yako ni kwamba, it is a global issue, na inahusisha watu amabo kimsingi hatuwezi kuwafanya chochote. ILIKUWA NI REPORT YA KUTUKATIZA TAMAA SISI WATANZANIA tusiendelee kuhoji tena Meremeta.

      Naweza kuendelea lakini, haina maana. Kama unataka nipige IP ban!
      Hivi tangu lini Mzee Mwanakijiji anatoa "ban"? Mkosoe tu kwa raha zako wala usiogope. Mbaya ni matusi na lugha za vitisho zitakazoweza kutuangamiza wote.

      Amandla.......
      Fundi Utumbo

    22. #39
      cabhatica's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th September 2010
      Location : SoWeTo
      Posts : 228
      Rep Power : 484
      Likes Received
      66
      Likes Given
      84

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      mzee MKJJ umenena.

      Uchaguzi huu ni wa mafanikio makubwa katika harakati za kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa watanzania. Tumepiga hatua. Ndio. Ingeweza kuwa ni hatua kubwa zaidi lakini kwa sababu tunazozijua za upigaji kura na utangazaji matokeo, mambo yako kama yalivyo. Hatujapoteza sana. Bado tunatembea kifua mbele. Nashauri hasira zetu tuzielekeze kwenye maeneo matatu yafuatayo:

      1. Vyama vya upinzani vilivyochukua majimbo na vilivyochukua Halmashauri za Wilaya/Manispaa etc wawaonyeshe watanzania kwa vitendo jinsi wanavyoitafsiri ilani za vyama vyao. Waonyeshe kuwa kuna tofauti kati ya uongozi wa sasa na utawala uliopita. Hii itajenga imani kwa umma na kuwa mifano ya mafanikio na mtaji kwenye kampeni za chaguzi zijazo.

      2. Wapenda mabadiliko tutumie nguvu ya hoja na ushawishi uliokwenda shule kuwaamsha watz ili wafuatilie kwa karibu utekelezaji wa serikali inayoingia madarakani ahadi zote zilizotolewa wakati wa kampeni. Hili lianze immediately baada ya kuapishwa kwa baraza la mawaziri.

      3. Wapiganaji waliofanikiwa kuingia bungeni kwa mara ya kwanza (hasa vijana) wasisinzie. Wawadhihirishie watanzania kuwa wanaweza ili kujenga imani kwa umma kuwa vijana wanahitaji kupewa nafasi zaidi. Wajue pia mjengoni kuna kanuni zake, hivyo kila mara wapate ushauri kwa wapiganaji wanaoitetea nchi ambao wana uzoefu wa shughuli za bunge ( Dr. Slaa et al)

      ROME WAS NOT BUILT IN A DAY!!!!!!!!!!

      TOGETHER WE CAN!
      Learn the Rules so you know how to break them properly!

    23. #40
      Zakumi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2008
      Location : Mtoni
      Posts : 3,975
      Rep Power : 1347
      Likes Received
      893
      Likes Given
      374

      Default Re: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

      Mwanakijiji:

      Heshima mkuu. Nilikuwa nasubiri kwa hamu posti zako. Kuna Mzee mmoja maarufu, jina kapuni, alipoandika barua wakati akiwa na hasira haikuipeleka moja kwa moja posta. Aliiweka kwenye droo ya meza na kesho yake aliisoma tena na kuandika barua nyingine. Kwa mtindo huu aliweza kuwa makini na kile alichoandika.

      Uchaguzi Tanzania ni kama mitihani ya shule ambayo kazi yake ni kuchagua watakaoendelea mbele. Lakini tukichukua kuwa uchaguzi au mitihani kuwa ni kigezo cha tathmini ya maendeleo, kuna mambo mengi ya kujifunza na vyama vya upinzani vina haki zote za kujisifu na kutumia matokeo ya uchaguzi kupanga mikakati ya baadaye.

      Nimetoka katika jimbo ambalo limechagua mbunge kutoka CCM. Na matokeo yalipotangazwa characterization ya kwanza ni kuwa jimbo letu ni la watu wasio soma na matusi mengine. Matusi haya yananifanya niwe na wasiwasi na mabadiliko yanayotakiwa na wanaJF.

      Kwa bahati nzuri namfahamu mbunge wa jimbo letu. Kwa miaka miwili alikuwa anajiandaa kwa uchaguzi huu. Na katika kipindi cha miaka hiyo miwili kulikuwa hakuna network ya chama chochote cha upinzani. Sasa watu wanapopiga kura kumchagua mtu wanayemfahamu kwanini waitwe wajinga.
      If we permit feathers to be freely borrowed, who is to tell the peacock from the crow?

    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Kizazi cha sasa na matumizi ya lugha
      By Ngomo in forum Jukwaa la Lugha
      Replies: 5
      Last Post: 6th February 2011, 13:53
    2. Palipo na demokrasia nguvu ya umma haina nafasi
      By GeniusBrain in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 29
      Last Post: 31st January 2011, 18:18
    3. Matumizi sahihi ya lugha
      By Dingswayo in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 3
      Last Post: 21st June 2010, 13:15
    4. Matumizi ya lugha.
      By Ekitarangwe in forum Jukwaa la Lugha
      Replies: 1
      Last Post: 22nd April 2009, 11:57

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...