Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Sitayatambua matokeo ya urais - Dk. Slaa

    Report Post
    Results 1 to 2 of 2
    1. EMT is offline
      EMT
      #1
      EMT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2010
      Location : Mahuta
      Posts : 9,181
      Rep Power : 68916
      Likes Received
      7560
      Likes Given
      6676

      Default Sitayatambua matokeo ya urais - Dk. Slaa

      Wednesday, 03 November 2010 05:18

      Na Mwananchi

      MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema, atayakataa matokeo ya urais yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa kumefanyika wizi mkubwa wa kura.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema, kama NEC inaitakia mema nchi hii, ifute matokeo yote ya urais na uchaguzi urudiwe upya.

      Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema wamekuwa wakifuatilia matokeo ya nchi nzima kwa umakini mkubwa na wamegundua kuna wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.

      "Kuna uchakachuaji mkubwa wa kura na kazi hiyo inafanywa na usalama wa taifa,"alisema Dk Slaa.

      Sitayatambua matokeo ya urais - Dk. Slaa


    2. #2
      remoteattacks's Avatar
      Member Array
      Join Date : 30th October 2010
      Posts : 25
      Rep Power : 443
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Sitayatambua matokeo ya urais - Dk. Slaa

      Nilitoa hii taarifa wengine walipuuza, wengine wakasema mie mzushi, ona sasa! Isome tena halafu sikiliza Dr. anasema nini?
      mhh hii ni balaa

      By pangamawe
      Poleni na harakati za kuikomboa nchi yetu!
      Leo napenda kuwajulisha mikakati michafu ya kupora na kuzuia maamuzi ya umma yanayofanywa na ccm kwa uratibu wa usalama wa taifa. Baada ya kubaini dalili za kuanguka vibaya katika uchaguzi wa mwaka huu idara ya usalama wa taifa imeandaa mikakati ya kuiba kura ili kuzuia chadema msiingie ikulu. Mikakati hii inaeleweka vizuri kwa tume ya taifa ya uchaguzi ambayo inashirikiana bega kwa bega na idara ya usalama wa taifa kumtengenezea jk ushindi bandia wa 80%. Wana hakika watanzania watagundua wizi huo na watakataa matokeo ndiyo maana kwanza waliwatumia viongozi wa dini waliotembelea makao makuu ya chadema wawasihi chadema wakubali matokeo yatakapotangazwa na juzi wamelitumia jeshi kutisha wananchi watakaoamua kupinga matokeo ya kupikwa yanayoandaliwa na nec/usalama wa taifa. Majid kikula ambaye ni government security officer ndiye mratibu wa zoezi la kuiba kura, ni mtaalamu aliyebobea katika kazi za aina hii aliratibu vizuri zoezi kama hilo mwaka 2005. Pia mwaka 2007 alitumwa kenya kwenda kumsaidia kibaki kupora ushindi wa odinga.

      Kikula anatumia muda wake mwingi hivi sasa ofisi za tume ya uchaguzi kwa ajili ya uratibu wa uvurugaji daftari la kudumu la wapiga kura akiifanya kazi hiyo kwa karibu na baadhi ya watendaji wa nec na maafisa kadhaa wa usalama wa taifa kutoka kurugenzi ya IT ya idara ya usalama (DITA) ambao wako ndani ya nec kwa zaidi ya miezi sita sasa, nitawapatia majina yao. Pia kuna vijana wataalamu wa IT waliochukuliwa kutoka maeneo mbalimbali wamepewa nyumba upanga mtaa wa undali shughuli kubwa wanayofanya ni kuandaa utaratibu wa ku-access remotely daftari la kudumu la wapiga kura. Hawa wanafanya kazi chini ya salva rweyemamu na mindi kasiga kutoka kurugenzi ya mawasiliano ikulu. Wapo vijana kadhaa leo nawapa majina ya wawili; maharage chande na edgar masatu wanafanya kazi kwa karibu na nzowa wa idara ya usalama ambaye ndiye aliyeratibu shambulio la kumwagiwa tindikali kubenea. Pia kuna kundi linalojumuisha wataalamu wa printing wa kiwanda cha uchapaji cha usalama wa taifa kilichopo MALINDI ambao hivi karibuni walikuwa mjini tanga kwa semina fupi ya jinsi ya kughushi kura kupitia fake ballot paper, timu hii inaongozwa na ndg SINYAU.

      Kwa hiyo utaona kwamba imeandaliwa mikakati mingi kuufanikisha uovu huo ili mmoja ukikwama basi mwingine utatumika ila wameamua ni lazima jk ashinde kwa 80%. Ndani ya idara ya usalama wa taifa maafisa wengi wamechoshwa na uongozi mbovu wa ccm hivyo wanataka mabadiliko ya uongozi idara imechukua hatua kadhaa kuhakikisha maafisa wote wa idara wanampigia kura jk, wote wameagizwa kuwasilisha vitambulisho vyao vya kupigia kura ili vinakiliwe namba ili atakayepigia upinzani afukuzwe kazi baada ya uchaguzi. Fuatilieni kwa karibu haya niliyowaeleza nimeyapata kwa nafasi yangu ndani ya tiss. Huyu KIKULA mfuatilieni kwa karibu ni hatari. HAKIKISHENI DUNIA NA WATANZANIA WOTE WANAJUA MAPEMA HILA HIZI. Jambo la kujiuliza maafisa usalama wa taifa wanafanya nini ndani ya tume ya uchaguzi wakati huu.

      Tafadhali ukipata ujumbe huu mtumie na mwingine ili kuchukua hatua makini kuilinda na kuikomboa nchi yetu.

    Similar Topics

    1. Matokeo ya Urais
      By Tanganyika in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 7
      Last Post: 4th November 2010, 11:52
    2. Matokeo ya urais bongo vipi?
      By Mauza uza in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 9
      Last Post: 3rd November 2010, 18:58
    3. Picha ya matokeo ya Urais kwa sasa
      By Mwanamayu in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 5
      Last Post: 3rd November 2010, 14:16
    4. Matokeo Ya Urais, kulikoni jamani?
      By Aristides in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 3
      Last Post: 2nd November 2010, 12:04
    5. ITV Tangazeni matokeo ya Urais mnavyoyapata
      By Mzee Mwanakijiji in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 7
      Last Post: 2nd November 2010, 08:36

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...