Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

    Report Post
    Page 7 of 8 FirstFirst ... 5678 LastLast
    Results 121 to 140 of 144
    1. #1
      Wa Ndima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th August 2010
      Posts : 1,381
      Rep Power : 730
      Likes Received
      223
      Likes Given
      645

      Default Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Leo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala, alisema Dk Slaa katika uchumi ni mbumbumbu na inaonekana anazungumza asichokijua na kudanganya wananchi.

      Dk Kamala alisema ahadi hiyo ni ya uongo kwani Sh 5,000 ni gharama ya usafirishaji wa mfuko kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa njia ya reli na tani moja ya saruji ya mifuko 20 ni Sh 100,000 hivyo gharama kwa mfuko kuwa Sh 5,000 sawa na bei anayowaahidi Watanzania. Alisema gharama za uzalishaji si chini ya Sh 7,000 kwa mfuko na kabla ya kuongeza gharama nyingine, mfuko wa saruji unapofika Mwanza gharama inakuwa zaidi ya Sh 12,000, hivyo kwa bei yake kuwa kubwa.

      Dk Kamala alisema hoja hiyo ni ndoto ambayo hata viongozi wa nchi tajiri duniani hawatarajii kuiota mbali na kuitekeleza na huko ni kudanganya wananchi. Akizungumzia hoja ya makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwamba yanaumiza Watanzania, alisema Dk. Slaa anapotosha kwani msingi mkuu wa makubaliano hayo ni ushirikiano huo kujengwa hatua kwa hatua kulingana na ridhaa ya wananchi. “Serikali imekuwa ikizingatia msingi huu kikamilifu kwa kushirikisha wananchi, likiwamo Bunge ambalo Dk Slaa amekuwamo kwa miaka mingi, mfumo huu unaziwezesha nchi wanachama kupata fursa ya kujipanga vema katika utekelezaji na kuitumia ngazi moja kuwa msingi wa kupanda ngazi inayofuata ya utangamano,“ alisema Kamala.

      Kuhusu mfumo wa kodi katika jumuiya, alisema si kweli kwamba aliuanzisha yeye, kwa kuwa yalianza kabla hajawa waziri na haiwezekani ushuru ufutwe bila kujadiliana na kukubaliana nchi wanachama, hivyo akasema Dk.Slaa hawezi kufuta ushuru huo kwani ni lazima ajadiliane na viongozi wa EAC.

      Kuhusu viwango vya VAT alisema Dk. Slaa ameonesha hajui kuwa kodi hiyo si ya Afrika Mashariki na kiasi cha VAT anacholipa mlaji kinategemea bei ya bidhaa katika soko, huku akitolea mfano wa maji ya kunywa ya ujazo wa nusu lita, ambayo Tanzania yanauzwa Sh 500 na Kenya Sh 800 ingawa Mkenya analipa VAT ya asilimia 16 na Mtanzania asilimia 18; Mkenya analipa kiasi kikubwa kuliko Mtanzania.

      Alisema kabla Dk. Slaa kusema Tanzania imeliwa, kwa kuwa na kiwango cha juu cha VAT Afrika Mashariki, alitakiwa kuelewa kwamba VAT si kodi ya Afrika Mashariki na katika uchumi, huwezi kulinganisha viwango vya VAT kabla ya kuangalia mfumuko wa bei kwenye nchi unazotaka kulinganisha, na kabla haujakokotoa, lazima uangalie viwango vya thamani ya kubadilisha fedha na gharama ya maisha.

      Alimtaka Dk. Slaa kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwadhalilisha akiwaita mbumbumbu, kielimu na katika kufanya biashara, huku akitaka kura zao, jambo ambalo si kweli, kwani miaka mingi Tanzania imekuwa kitovu cha elimu katika kanda hii huku viongozi wake wengi wakisoma Tanzania.

      Sasa kama CCM Imeshindwa si ikae pembeni?


    2. FemaTV & Radio

    3. #121
      Elli's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 17th March 2008
      Location : Kijito-Upele
      Posts : 8,513
      Rep Power : 0
      Likes Received
      2102
      Likes Given
      1839

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Masikini wee, nilimuona alivyokuwa akijing'ata ng'ata sijui na yeye alilazimishwa kwenda kuyasema yale, vitu vingine kama maigizo flani hivi

    4. #122
      genekai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th February 2010
      Location : Loitering!
      Posts : 7,493
      Rep Power : 2077
      Likes Received
      1056
      Likes Given
      1568

      Default Re: Anavyosema Kamala

      Huyo hana data achaneni naye, angekuwa jimboni anapiga kampeni asingeyasema haya. Ni kwakuwa hana kazi ndo maana anajikeep busy kwa kubwabwaja tu. Hivi alishahama kwenye nyumba ya serikali au anasubiri kufukuzwa?
      The future of this country is being jeopardized by the intellectual slavery of our top leaders

    5. #123
      Chesty's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2009
      Posts : 1,037
      Rep Power : 701
      Likes Received
      155
      Likes Given
      18

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By Ami
      Mfano uliotumia si sahihi.China ni nchi ya kisoshalist na sisi ujamaa umetushinda.HIzo subsidies hatuzitaki,ni mzigo wa bure kwa serikali.
      Kila mtu abebe mzigo wake.Slaa wa kwake na Kikwete wa kwake.Mwenye pesa ya kujengea nyumba abebe mfuko wake wa saruji.
      Wewe na Kamala chungu chenu kimoja. Subsidy inatumika sana nchi za kibepari. Wakulima wao wanapewa subsidy kubwa sana ndo maana nchi zetu tunawalalamikia kila siku.

    6. #124
      Ernesto Sheka's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 102
      Rep Power : 454
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By Ndugu
      Kweli kabisa
      "Dk Kamala alisema ahadi hiyo ni ya uongo kwani Sh 5,000 ni gharama ya usafirishaji wa mfuko kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa njia ya reli na tani moja ya saruji ya mifuko 20 ni Sh 100,000 hivyo gharama kwa mfuko kuwa Sh 5,000 sawa na bei anayowaahidi Watanzania. Alisema gharama za uzalishaji si chini ya Sh 7,000 kwa mfuko na kabla ya kuongeza gharama nyingine, mfuko wa saruji unapofika Mwanza gharama inakuwa zaidi ya Sh 12,000, hivyo kwa bei yake kuwa kubwa."
      Ushabiki kweli mbaya?Hamuoni kitu hapo?

    7. #125
      Ernesto Sheka's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 102
      Rep Power : 454
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By Ernesto Sheka
      "Dk Kamala alisema ahadi hiyo ni ya uongo kwani Sh 5,000 ni gharama ya usafirishaji wa mfuko kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa njia ya reli na tani moja ya saruji ya mifuko 20 ni Sh 100,000 hivyo gharama kwa mfuko kuwa Sh 5,000 sawa na bei anayowaahidi Watanzania. Alisema gharama za uzalishaji si chini ya Sh 7,000 kwa mfuko na kabla ya kuongeza gharama nyingine, mfuko wa saruji unapofika Mwanza gharama inakuwa zaidi ya Sh 12,000, hivyo kwa bei yake kuwa kubwa."
      Ushabiki kweli mbaya?Hamuoni kitu hapo?
      Takwimu hazidanganyi.Likiwachoma hawataki kuliona.Wanaharakati uchwara waje wampinge Dr.Kamala na tuwaone sasa.

    8. Study Abroad

    9. #126
      Ernesto Sheka's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 102
      Rep Power : 454
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By kisu
      Kama Kiwete akiulizwa kwa nini watanzania masikini na hajui kwa nini ndio utegemee nini toka Chama cha Majambazi???
      Kikwete knows why we are poor.Do you remember who asked him that question?International journalist right?
      Ulitaka aseme watanzania wengi ni wavivu na bado wana ota kuhusu ujamaa?

    10. #127
      Ernesto Sheka's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 102
      Rep Power : 454
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By Chesty
      Wewe na Kamala chungu chenu kimoja. Subsidy inatumika sana nchi za kibepari. Wakulima wao wanapewa subsidy kubwa sana ndo maana nchi zetu tunawalalamikia kila siku.
      Vipi kuhusu international regulations kwa local subsidies?Hivi unafahamu unachoongea kweli?

    11. #128
      Mndamba Namba 1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 19th October 2010
      Posts : 103
      Rep Power : 455
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Kamara hana lolote yeye ndo mbumbumbu, unajua kilichomponza kule Nkenge mpaka akapigwa chini na mwanamama Nshunga?wananchi wa Nkenge walimwambia mheshimiwa nyani wanakula mazo yetu yeye akawajibu kwa kuwaambia kuleni hao nyani ili wapungue,"waganda kyaka"wakamsubiri kwenye kura za maoni wakamfundisha adabu,kesho yake aliondoka na ndege ya Auric air ya saa kumi na mbili yeye,karamagi.Lucy msafiri na Masilingi.hana lolote anataka apewe nafasi ya ubunge wa upendeleo.

    12. #129
      M-mbabe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th October 2009
      Location : here n' there
      Posts : 1,297
      Rep Power : 745
      Likes Received
      326
      Likes Given
      352

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By Kibunango
      Si mbumbumbu kwenye uchumi tu, hata katika maisha yake binafsi amejionyesha ni mbumbumbu... Utatembeaje na mke wa mtu bila kujua?
      Haya ndugu, kwa kutumia hiihii lugha yako ya majitaka...je na huyo wa KWENU anayetembea na vyangudoa utamwitaje?
      If you're not ready to die for it, put the word 'freedom' out of your vocabulary (Malcolm X)

    13. #130
      hashycool's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2010
      Location : network search....
      Posts : 4,957
      Rep Power : 1456
      Likes Received
      559
      Likes Given
      141

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By Kibunango
      Si mbumbumbu kwenye uchumi tu, hata katika maisha yake binafsi amejionyesha ni mbumbumbu... Utatembeaje na mke wa mtu bila kujua?
      Stupidity doesn't count as a handicap, park elsewhere.
      hivi vrusi vya H.I.V na wewe nani mchokozi?

    14. #131
      Kashishi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th April 2010
      Posts : 230
      Rep Power : 508
      Likes Received
      50
      Likes Given
      29

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By Rafikikabisa
      Huyu kamala siyo mbumbumbu tu bali pia limbukeni alipopata uwazili akawadharau hata wapiga kura wake kiasi kwamba alikuwa akiwaambia kuwa yuko bussy na rais kwa hiyo hawezi kuwasaidia.

      Sana sana ni kuwaambia alivyokuwa UK na USA akifikiria hayo ndiyo matatizo ya wananchi wake. Nafikiri kafulia sasa anaangalia kama atapata kacheo angalau aweze kupata mkate wa kila siku, vinginevyo uzee utamwijia hivi karibuni maana hata vyeti vyake kishule havikubaliki.
      Lakini si unaona kwa ulimbukeni wa kuwa dharau mpaka wapiga kura wake sasa wameamua kumpiga chini kwenye kura za maoni. Hivi sasa hata future yake mwenyewe imekuwa kitendawili. Mwache aendelee kumsaidia JK kupiga jalamba wakati Dr wetu anaelekea House No.1 Magogoni Street (aka Ikulu:-)

    15. #132
      Ngolinda's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 12th April 2010
      Location : Chile
      Posts : 114
      Rep Power : 488
      Likes Received
      23
      Likes Given
      35

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By Mnyalu wa Kweli
      Hivi tulitegemea nini sisi watanzania kwa kuongozwa na viongozi wenye mawazo mfu kama ya huyu Dr Kamala? Naililia Tanzania ya Nyerere na Sokoine.
      Tatizo ni pale tunapoiacha siasa na uongozi mikononi mwa wapuuzi ama kwa kuogopa misukosuko ya siasa ama kutoona umuhimu, na kuruhusu wasio na upeo walio katika siasa wafanye maamuzi kwa niaba yetu. Ni wakati wa wale wenye uwezo wa kiakili, kimaadili na wazalendo kujitoa muhanga kwa maslahi ya taifa.
      A wise person does at once, what a fool does at last. Both do the same thing; only at different times.

    16. #133
      Ernesto Sheka's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 102
      Rep Power : 454
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Anavyosema Kamala

      Quote By genekai
      Huyo hana data achaneni naye, angekuwa jimboni anapiga kampeni asingeyasema haya. Ni kwakuwa hana kazi ndo maana anajikeep busy kwa kubwabwaja tu. Hivi alishahama kwenye nyumba ya serikali au anasubiri kufukuzwa?
      "...anajikeep busy kwa kubwabwaja tu." = Upofu + Ushabiki.

    17. #134
      chamajani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd September 2010
      Location : Baharini Kina kirefu
      Posts : 492
      Rep Power : 537
      Likes Received
      0
      Likes Given
      9

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By Kagemro
      kweli Kamala ni mjinga na sijui kama anasoma.jamani huyu waziri hajui kwamba EAC ni hiari,leo katiba ya kenya wakenya wamejiondoa katika jumuhia hiyo simply they are not ready prepared.mwambieni atafute gazeti East africa asome,viongozi kama hawa hawafai.
      Hilo gazeti la East African umelisoma mwenyewe au umesomewa? Usije kuwa wee ndo mjinga maradufu!

    18. #135
      chamajani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd September 2010
      Location : Baharini Kina kirefu
      Posts : 492
      Rep Power : 537
      Likes Received
      0
      Likes Given
      9

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By Ernesto Sheka
      Vipi kuhusu international regulations kwa local subsidies?Hivi unafahamu unachoongea kweli?
      Kama ni mbumbumbu wa uchumi wa ndani, vipi kwenye International Regulations si ndio zero kabisa.

    19. Pax
      #136
      Pax's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd May 2009
      Posts : 234
      Rep Power : 557
      Likes Received
      54
      Likes Given
      0

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Huyu Kamala ana matatizo kichwani. Ushirikiano wa EAC kama hauna faida kwa wananchi hauna maana. Kushusha bei ya saruji inawezekana sana tu, kama wao wameshindwa wawaachie wanaoweza, ebo!

    20. #137
      Magulumangu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th January 2010
      Posts : 2,987
      Rep Power : 1073
      Likes Received
      370
      Likes Given
      419

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Quote By M-mbabe
      Haya ndugu, kwa kutumia hiihii lugha yako ya majitaka...je na huyo wa KWENU anayetembea na vyangudoa utamwitaje?

      Hivi Babu seya aliwekwa ndani kwa ajili ya nani vile?alikula vya mkulu eeehhhh? kesho kutwa mzee lao kwishineyi
      The Goal is The Love Of a Lifetime, And a Lifetime Of Love Together.....

    21. #138
      Ernesto Sheka's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 102
      Rep Power : 454
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Anavyosema Kamala

      Quote By genekai
      Huyo hana data achaneni naye, angekuwa jimboni anapiga kampeni asingeyasema haya. Ni kwakuwa hana kazi ndo maana anajikeep busy kwa kubwabwaja tu. Hivi alishahama kwenye nyumba ya serikali au anasubiri kufukuzwa?
      "..kubwabwaja.."
      Kweli mchambuzi.

    22. #139
      Father of All's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 3,093
      Rep Power : 1043
      Likes Received
      1828
      Likes Given
      3343

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Hili lenyewe liligushi cheti na halijioni kuwa ni zuzu na mbumbumbu mzungu wa reli! Kweli nyani haoni nonihino lake!

    23. #140
      Santo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th December 2011
      Posts : 308
      Rep Power : 436
      Likes Received
      50
      Likes Given
      2

      Default Re: Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

      Umetumwa wewe, jipange upya

    24. Miaka 50
    Page 7 of 8 FirstFirst ... 5678 LastLast

    Similar Topics

    1. Who is Deodorus Kamala?
      By Tuko in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 16
      Last Post: 29th October 2010, 18:51
    2. Replies: 6
      Last Post: 28th October 2010, 11:29
    3. Kamala: Slaa muongo, aombe radhi
      By Safari_ni_Safari in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 5
      Last Post: 26th October 2010, 09:59
    4. Replies: 38
      Last Post: 20th October 2010, 20:58
    5. [Good Job] We need more Dr Diodorus Kamala's
      By Alpha in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 19
      Last Post: 2nd September 2008, 15:44

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...