Nilipata kumsikia mtu akisema hangependa aitwe "mswahili". Nikapatwa na maswali mengi kichwani kwani mtu huyu alikua mzawa, mweusi na anaishi DSM. Kabla sijamtaka undani kwa kauli yake hii, nilidhani uswahili ni title ya mtu mwenye ngozi nyeusi na anayeishi au anayetoka kwenye jamii ya watu wa mwambao. Baada ya kuongea na huyu mtu, niligundua kuwa hata mzungu na watu wa bara wanaweza kuwa waswahili!
Kinachomfanya mtu awe mswahili kumbe ni "hulka" - kubwa mbili zikiwa (1) kuongea zaidi ya matendo na (2) kujifanya kujua kila kitu.
Kwa mtizamo huu, Tanzania tuna waswahili kibao, Tutafika kweli?

Reply With Quote
Follow Us Here