Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

    Report Post
    Page 3 of 5 FirstFirst 12345 LastLast
    Results 41 to 60 of 87
    1. #1
      Mchokonozi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th November 2009
      Posts : 15
      Rep Power : 487
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Unhappy Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Waungwana, mtaniwia radhi kwa kutoonekana ukumbini kwa muda mrefu. Nimekuwa nikisoma alama za nyakati ili niweze kuja hapa na mada iliyosheheni hoja za nguvu, si nguvu za hoja.

      Naanza kwa hili la Mke Mdogo wa Mkuu wa Kaya – nadhani wote mnamtambua, sihitaji kumtaja jina lake – ambaye hivi karibuni ameanza kampeni za wazi wazi, ikionekana dhahiri kwamba si kwamba anajinadi ili kuweza kupata umaarufu wa haraka haraka, lakini lengo lake haswa likiwa kuupata Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Tawala.

      Habari za ndani kutoka kwa wadau walio karibu naye zinadai kwamba mwanamama huyu machachari na mkorodi, ambaye inasemekana kwamba “haambiliki” hata kwa Mkuu wa Kaya mwenyewe, amepania naye kuukwaa Ubunge huo ili naye aingie “mjengoni” mwaka 2010, lakini kisichojulikana ni kwa malengo gani haswa yanayomsukuma kufanya hivyo. Licha ya kwamba mwanamama huyu ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kifedha – jambo ambalo amelidhihirisha wazi wazi – haieleweki ni kipi haswa anachokifuata “mjengoni” humo.

      Duru za kisiasa zinasema harakati za mwanamama huyu zinaweza kuleta athari hasi kwa Mkuu wa Kaya, kwani zitasomeka kuwa harakati za kuigeuza hali ya kisiasa nchini hapa kuwa ya “kisultani”, kwani, minong’ono inasikikika kwamba mwana wa Mkuu wa Kaya, ambaye ni Mjumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Bagamoyo, naye pia yumo mbioni kujiandaa kugombea kuingia “mjengoni”, ingawa hajatangaza rasmi nia yake hiyo.

      Mwanamama huyu alianza kishindo cha kampeni zake siku chache zilizopita baada ya kumwaga kitita cha fedha taslim shilingi milioni 10, ambazo alihakikisha zinaonekana kwenye taarifa ya habari ya kituo cha luninga cha Channel Ten, ambacho ndicho kimekuwa karibu naye kwa wakati wote huu. Kitita hicho kilimwagwa kama “msaada” kwa timu ya soka ya wanawake, Twiga Stars, RK akitambulishwa kama “mdau wa soka ya wanawake”, na kutambulishwa kwamba amekuwa akiichangia timu hiyo mara kwa mara. Jambo la kushangaza ni kwamba, ni zaidi ya mara moja timu hiyo imekuwa ikitembeza bakuli kwa wafadhili mbalimbali, lakini haikuwahi kusikika hata mara moja kwa mwanamama huyo – ambaye anaishi nchini Oman – kujitokeza kuisaidia, licha ya uwezo wake mkubwa wa kifedha.

      Jitihada za mwanamama huyu kujinadi wazi wazi hazikuishia hapo, kwani, ni Jumapili ya wiki iliyoisha, alijitokeza kufadhili kinyanganyiro cha kuwasaka walimbwende wanaoshiriki kupitia shindano la Miss Inter College, ambao washindi wake watapata nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye shindano la Miss Tanzania 2010. Safari hii, dau la mwanamama huyu limeongezeka kufikia Shilingi milioni 12, akijinadi kupitia kampuni ya RBS Oil and Technology.

      Tathmini yangu ni kama ifuatavyo.

      Iwapo mwanamama huyu ataachwa kuendelea kufanya ayatakayo, huenda kambi ya Mkuu wa Kaya ikapata athari hasi, kwani harakati hizi zitaweza kuwa “mtaji wa kisiasa” (political capital) kwa kambi ya upinzani, wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010, jambo ambalo linaweza kuathiri vibaya matokeo ya kura zitakazovunwa na Mkuu wa Kaya
      Duru za kisiasa zimezidi kudodosa na kusema kwamba, harakati za mwanamama huyu zinaweza kutafsiriwa kuwa ukandamizaji kwa wanawake kutokana na nafasi kubwa aliyonayo kama Mke Mdogo wa Mkuu wa Kaya, nafasi ambayo anaweza kuitumia ipasavyo kwani hakuna atakayeweza kumpinga wakati wa kinyang’anyiro hicho cha Ubunge kupitia Viti Maalum. Kampeni ya kusaka umaarufu kwa kutoa michango lukuki inasadikiwa kuwa ni kutaka kumwiga Mke wa Rais, ambaye tayari amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya wanawake na watoto, japokuwa Mke huyo hajaonesha nia ya kutaka kugombea nafasi ya kuingia “mjengoni”

      Wadau wa masuala ya kisiasa wamemshauri Mkuu wa Kaya kumwita mwanamama huyo na kumkalisha, kasha kumpa karipio kali na amri ya kusitisha mara moja harakati zake hizo, kwani harakati hizo za kuutaka umaarufu zinaelekea kumwaga “mtama” na kuweka wazi mambo ya ndani ya “familia” yasiyopaswa kujulikana, jambo ambalo litaweza kuiweka kambi ya Mkuu wa Kaya kwenye wakati mgumu mara tu kipenga cha kampeni za Uchaguzi Mkuu kitakapopulizwa rasmi.

      “Sio kwamba Mkuu wa Kaya anapendwa sana na wananchi wake, la hasha; sio kwamba wananchi wake wote watafurahi akirejea ulingoni, la hasha; itakuwa ni aibu akishindwa kurejea kwa sababu ya kukuru-kakara za mke wake mdogo”, alishauri mdau mmoja wa kisiasa.

      Nimepewa ujumbe niufikishe kwa Mkuu wa Kaya. Natumai utafika.

      >>> Mchokonozi, Shujaa wa Kuchokonoa!

    2. Miaka 50

    3. #41
      Nyambala's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th October 2007
      Location : Tahiti
      Posts : 4,402
      Rep Power : 1517
      Likes Received
      1019
      Likes Given
      938

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      "Aliwataja walioahidi kutoa fedha hizo kuwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba aliyeahidi Sh. Milioni 20"

      Du kweli Tanzania siku hizi nchi ya kibepari, Makamba ana biashara gani ya kuchangia kutoa Mil20? Katibu mkuu wa CCM siku hizi inaonyesha si mchezo! Just about 20 yrs ago zaidi ya heshima vyeo hivi ilikuwa ni umasikini tu! Sana sana ni nyumba bure, gari bure na utaambulia tuzawadi wakati wa kustaafu.

    4. #42
      Pengo's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 15th October 2009
      Posts : 581
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Tatizo la wadanganyika wengi ni wivu, chuki, fitina, uroho, upumbavu, ujinga n.k.

      Kwani mtu kuwa na pesa zake na kuutaka ubunge ni kosa? Mbona Mzee Ndesa ni bilionea na bado ni mbunge? Mbona mama Lwakatare ni bilionea na bado ni mbunge? Wakili Mkono na wengine wengi ni mamilionea wa kutupwa na bado wanang'ang'ania ubunge sembuse huyo al hadoud? Chuki zenu zinawapeleka pabaya na hasa pale mnapozionyesha hadharani kuhusu mtu fulani au jamii fulani au kikundi fulani.Leo mnalilia maximo mwingine wakati pesa za kumlipa zinatoka ikulu,kwanini msiamue kuchangia wenyewe na kumlipa ili hizo za ikulu zinunue madawati?

      Amejitokeza mwanamama shupavu wa kuchangia taifa lake katika michezo mnaanza ooh ushuzi, kajamba mtakufa bure na vijiba vya roho.Acheni ujinga fanyeni kazi na si kufuatilia mambo ya watu,taifa masikini kwa mtaji huo lazima mtaendelea kuwa masikini wa kutupwa na kutawaliwa kila siku. Najua hapo angekuwa anatoa misaada yule ambaye si miongoni mwa mliyetumwa kuwatenga katika mipango yenu basi mngeanza kumsifia yule anafaa sana.

      Upumbavu huo hautoisha hadi mbadili yaliyomo katika vifua vyenu. Nimekumbuka mhanga mmoja alisema "La kama mngeyajua yaliyomo vifuati mwao wala msingewafanya hao kuwa marafiki na vipenzi vyenu", sasa chuki zao zimeanza kujionyesha hadharani.

      Ukichukia chukia kwasababu huniongezei siku za kuishi hapa duniani,muda wangu ukifika nitajifia na si kuendekeza ujinga na upuuzi wa aina hiyo.

      Mungu ibariki Tanzania.

    5. #43
      Gembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2007
      Location : kamnyonge
      Posts : 2,586
      Rep Power : 1516
      Likes Received
      64
      Likes Given
      54

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Kwani kuna ubaya gani?Mwaache agombee sababu kila mtu yuko huru kugombea na kam hammtaki msimpe kura zenu..
      As long as I am leader, Our position is not going to change from that of our forefathers. I do not want the responsibility for selling the rights of our children yet unborn

    6. #44
      Brooklyn's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th March 2009
      Posts : 1,313
      Rep Power : 781
      Likes Received
      166
      Likes Given
      41

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Nimemuona huyu mrembo nami nikashtuka na kuwaza mbona ameamua kujitokeza kwenye public??

      Niliwahi kudokezwa na mtu ambaye yuko 'connected' kwamba huyu mama ndo bi mdogo.

      Kwa update tu, jana amemwaga Tsh. 10 million kwa kituo cha watoto yatima kigamboni kinachomilikiwa na Mwanamitindo Khadija Mwanamboka.

      TV station zote hapa mjini zilirusha tukio hilo kwenye taarifa zao za habari kwa kina na nafasi kabisa!!
      Ukipewa kazi ya kurina asali, mikono yako ikatapakaa asali, je utaisugua mikono kwenye vumbi ili kujisafisha au utailamba?

    7. #45
      MANI's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 22nd February 2010
      Location : CHINI YA MBUYU
      Posts : 1,914
      Rep Power : 953
      Likes Received
      568
      Likes Given
      629

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Wanasiasa wetu wapo kwa ajili yao na sio wewe Masanilo au Mtanzania yoyote kwa hiyo dispensari unayoiwaza wewe wao hawana shida nayo after all nani atakutangaza kwenye hayo.

    8. FemaTV & Radio

    9. #46
      roselyne1's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 1,374
      Rep Power : 0
      Likes Received
      75
      Likes Given
      3

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      huyu na mama salma nani mrembo??mie kura yangu inaenda kwa mama salma teh teh!

    10. #47
      Kakalende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2006
      Posts : 2,911
      Rep Power : 1228
      Likes Received
      381
      Likes Given
      371

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Sina shida na misaada anayotoa kwani wako wengine wanafanya hivyo kipindi hiki; isipokuwa amezidi sana kwenye vyomobo vya habari na sana sana imetusaidia kum-scrutinise kwa karibu. Kama kweli anataka ubunge, basi agombee kwenye jimbo mojawapo!

      Lakini hili lakuwa 'nyumba ndogo' ya mkuu wa kaya limetoka wapi?
      Volunteers are not paid -- not because they are worthless, but because they're priceless!

    11. #48
      Majala Kimolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2007
      Posts : 316
      Rep Power : 666
      Likes Received
      26
      Likes Given
      31

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Quote By Pengo
      Tatizo la wadanganyika wengi ni wivu, chuki, fitina, uroho, upumbavu, ujinga n.k.

      Kwani mtu kuwa na pesa zake na kuutaka ubunge ni kosa? Mbona Mzee Ndesa ni bilionea na bado ni mbunge? Mbona mama Lwakatare ni bilionea na bado ni mbunge? Wakili Mkono na wengine wengi ni mamilionea wa kutupwa na bado wanang'ang'ania ubunge sembuse huyo al hadoud? Chuki zenu zinawapeleka pabaya na hasa pale mnapozionyesha hadharani kuhusu mtu fulani au jamii fulani au kikundi fulani.Leo mnalilia maximo mwingine wakati pesa za kumlipa zinatoka ikulu,kwanini msiamue kuchangia wenyewe na kumlipa ili hizo za ikulu zinunue madawati?

      Amejitokeza mwanamama shupavu wa kuchangia taifa lake katika michezo mnaanza ooh ushuzi, kajamba mtakufa bure na vijiba vya roho.Acheni ujinga fanyeni kazi na si kufuatilia mambo ya watu,taifa masikini kwa mtaji huo lazima mtaendelea kuwa masikini wa kutupwa na kutawaliwa kila siku. Najua hapo angekuwa anatoa misaada yule ambaye si miongoni mwa mliyetumwa kuwatenga katika mipango yenu basi mngeanza kumsifia yule anafaa sana.

      Upumbavu huo hautoisha hadi mbadili yaliyomo katika vifua vyenu. Nimekumbuka mhanga mmoja alisema "La kama mngeyajua yaliyomo vifuati mwao wala msingewafanya hao kuwa marafiki na vipenzi vyenu", sasa chuki zao zimeanza kujionyesha hadharani.

      Ukichukia chukia kwasababu huniongezei siku za kuishi hapa duniani,muda wangu ukifika nitajifia na si kuendekeza ujinga na upuuzi wa aina hiyo.

      Mungu ibariki Tanzania.
      Hongera kwa mpasho bibi, sadaka yatolewa bila mkono wa kushoto kujua lipi limetolewa kwa mkono wa kulia. Hofu imetolewa hakuna haja ya kutoa matusi. Hukmu yake inahitaji muda, vuta subira uone mambo kama yatatimia.
      Vipi la nyumba ndogo weye hujalipata! Yaonesha una hasira na wenye wivu, ndo mapenzi basi

    12. #49
      Baba_Enock's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2008
      Location : Bunju "B"
      Posts : 5,817
      Rep Power : 1899
      Likes Received
      1161
      Likes Given
      977

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Aliwataja walioahidi kutoa fedha hizo kuwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba aliyeahidi Sh. Milioni 20, Superdol Sh. Milioni 3, Scandinavia Sh. Milioni 2, hoteli ya Paradise Sh. Milioni 2, familia ya Kapinga Sh. Milioni 1.5 na Mkurugenzi wa Masoko na Udhamini wa Vodacom Sh. 300,000
      Hapo penye red panawiana kwa karibu saaana!
      Ad Majorem Dei Gloriam - "For the greater glory of God"

    13. #50
      Congo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th March 2008
      Posts : 454
      Rep Power : 661
      Likes Received
      49
      Likes Given
      39

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Waungwana, ingawa jina la huyu mama Rahma Al kharoos al kharoos kwa sasa linaonekana kuwa kubwa lakini utafiti wangu mdogo kwenye google haukunionyesha umuhimu wowote ambao anaonekana kuwa nao huyu mama.

      Pamoja na kuwa kampuni yake
      RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED inaonekana kutaka kujenga kiwanda cha kusafishia mafuta (kama ilivowahi kuripotiwa na gazeti la East Afrcan huko nyuma) na kujenga bomba la mafuta lakini kampuni hii haina website wala address. Wala haina kampuni mama huko inakotoka.

      Nashindwa kabisa kuelewa inakuwaje kampuni hii ifiche details zake kiasi hiki. Huyu mama anaonekana kwenye likendly tu na profile yake ni kidogo sana hapo. Nadhani kuna usanii wa namna fulani ndani ya hili suala.

    14. #51
      Zogwale's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 10th July 2008
      Posts : 5,979
      Rep Power : 2634
      Likes Received
      1200
      Likes Given
      501

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Quote By Brooklyn
      Nimemuona huyu mrembo nami nikashtuka na kuwaza mbona ameamua kujitokeza kwenye public??

      Niliwahi kudokezwa na mtu ambaye yuko 'connected' kwamba huyu mama ndo bi mdogo.

      Kwa update tu, jana amemwaga Tsh. 10 million kwa kituo cha watoto yatima kigamboni kinachomilikiwa na Mwanamitindo Khadija Mwanamboka.

      TV station zote hapa mjini zilirusha tukio hilo kwenye taarifa zao za habari kwa kina na nafasi kabisa!!
      Mkuu hata ITV ilirusha tukio hilo? Ni saa ngapi hiyo? Sijaona hata chembe!!! Ningeshangaaaaa mnooooo! Lo! Labda kama unamanisha Chanel 10, Star Tv na TBC1 ambazo sifuatilii taarifa zao labda iwe bahati mbaya!

      "Kama unaingia Ikulu kwa njia ya rushwa, je ni biashara gani iko huko ya kuwezesha kulipa fadhila ya rushwa hiyo???"

    15. #52
      Ben Saanane's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th January 2007
      Posts : 6,725
      Rep Power : 32786
      Likes Received
      4994
      Likes Given
      6456

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Duh,kazi ipo....hii nchi.
      Wametuonyesha Jeuri ya ukaburu,tuwaonyeshe jeuri ya Umkhontho we sizwe kupitia Red Brigade.Tukiwaonyesha woga wetu, itakua silaha imara zaidi kwao kutumaliza-Ben Saanane

    16. #53
      Mayolela's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2009
      Posts : 385
      Rep Power : 569
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Tutaona mengi mwaka huu,from no where?

    17. #54
      Keil's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd July 2007
      Posts : 2,381
      Rep Power : 1090
      Likes Received
      756
      Likes Given
      292

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Kaazi kweli kweli!

      Baba Rais, then Mama ndani ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) hii haina tofauti na UWT, mama mdogo anataka Ubunge, Ridhiwan ameteka UVCCM na Khalfani amewekwa ndani ya Chipukizi. Yaani hapo zinaandaliwa generations 3 ziende kwa kupokezana vijiti mpaka mwisho.

      Kikwete anaweka familia kila kona. Tusubiri kuona teuzi za ajabu ajabu za wabunge wa kuteuliwa.

    18. #55
      Lambardi's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 7th February 2008
      Location : KITAANI ZAIDI
      Posts : 4,517
      Rep Power : 0
      Likes Received
      654
      Likes Given
      0

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Ubungeeee.....mwaka huu tutaona mengi sana sanaa.....na badooo

    19. #56
      Chimunguru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2009
      Posts : 7,794
      Rep Power : 2148
      Likes Received
      1221
      Likes Given
      543

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Haluuu, nilikuwa najiuliza sana huyu mwanamke ametokea wapi ghafla namna hii?? na anatafuta nini kwa kumwaga pesa namna hii?? kumbe ni small house!! da sasa waTZ hizi nyumba zetu ndogo tunaziendekeza mno KHAAAAAAAAAAAAAAAAA! kumbe mkuu wa kaya ana balaa namna hii haya wadanganyika sasa mpira kwenu hapo kuna KIONGOZI kweli?

    20. #57
      FirstLady1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th July 2009
      Location : Mama Mwenye Nyumba
      Posts : 14,962
      Rep Power : 3700
      Likes Received
      3576
      Likes Given
      5759

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Quote By Chimunguru
      Haluuu, nilikuwa najiuliza sana huyu mwanamke ametokea wapi ghafla namna hii?? na anatafuta nini kwa kumwaga pesa namna hii?? kumbe ni small house!! da sasa waTZ hizi nyumba zetu ndogo tunaziendekeza mno KHAAAAAAAAAAAAAAAAA! kumbe mkuu wa kaya ana balaa namna hii haya wadanganyika sasa mpira kwenu hapo kuna KIONGOZI kweli?
      Hii ni hatari kama kuna ukweli ndani yake nazidi kumvulia kofia
      No one is in charge of your happiness except you...
      God time is the best..

    21. #58
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6152
      Likes Given
      22273

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Quote By Brooklyn
      Niliwahi kudokezwa na mtu ambaye yuko 'connected' kwamba huyu mama ndo bi mdogo.
      Wa JF wenzangu, naomba tujitahidi kutenganisha, tetesi na habari ambazo ni too personal na kutochanganya privacy za watu na puclic rights.

      Huyo mama ni Mtanzania kama walivyo watanzania wengine, anazo haki zake kikatiba kugombea nafasi yoyote kupitia chama chochote na wala isiwe issue, kama ilivyo kwa Riz, lazima atachukua fomu ya ubunge 2010 ili 2015 aukwae uwaziri na 2025 apande ghorofani.

      Ila pia Mkuu wa nchi ni publi figure paid by taxpayers money, hivyo taxpayers wana right ya kuijua his public as well as his private life/conduct kwa sababu analipwa kwa jasho lao.

      Hivyo mimi nauliza hivi, kama hii issue ya 'jumba dogo' ni kweli, Watanzania tunahaki ya kupatiwa taarifa rasmi, mbona Mzee Mwinyi it was rasmi Bi Khadija na Mama Sitti, na ikakubalika the official one ni Mama Sitti. Hivyo hata kama Mama Salma ndio official 1st Lady, tunahaki ya kumtambua ma-mdogo ambae ni 2nd Lady.

    22. #59
      MwanaHaki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th October 2006
      Posts : 1,413
      Rep Power : 1003
      Likes Received
      156
      Likes Given
      91

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Quote By Fundi Mchundo
      Mnamuonea huyu dada. Kumbe alianza zamani kuchangia soka la wakina mama!

      Amandla....

      Lete ushahidi kama kweli alianza kuchangia zamani...

      ./Mwana wa Haki

      P.S. No research, no right to speak!
      Speaking Openly, without fear!

    23. #60
      MwanaHaki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th October 2006
      Posts : 1,413
      Rep Power : 1003
      Likes Received
      156
      Likes Given
      91

      Default Re: Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

      Quote By Pasco
      Wa JF wenzangu, naomba tujitahidi kutenganisha, tetesi na habari ambazo ni too personal na kutochanganya privacy za watu na puclic rights.

      Huyo mama ni Mtanzania kama walivyo watanzania wengine, anazo haki zake kikatiba kugombea nafasi yoyote kupitia chama chochote na wala isiwe issue, kama ilivyo kwa Riz, lazima atachukua fomu ya ubunge 2010 ili 2015 aukwae uwaziri na 2025 apande ghorofani.

      Ila pia Mkuu wa nchi ni publi figure paid by taxpayers money, hivyo taxpayers wana right ya kuijua his public as well as his private life/conduct kwa sababu analipwa kwa jasho lao.

      Hivyo mimi nauliza hivi, kama hii issue ya 'jumba dogo' ni kweli, Watanzania tunahaki ya kupatiwa taarifa rasmi, mbona Mzee Mwinyi it was rasmi Bi Khadija na Mama Sitti, na ikakubalika the official one ni Mama Sitti. Hivyo hata kama Mama Salma ndio official 1st Lady, tunahaki ya kumtambua ma-mdogo ambae ni 2nd Lady.

      Pasco,

      How can there be objectivity and transparency when the Head of State AND the Spouse (First, or Second Lady) are also at the VERTICE?

      Are we a MONARCHY or a DEMOCRACY?

      Answer that, please.

      Privacy MY ASS!

      ./Mwana wa Haki
      Speaking Openly, without fear!

    Page 3 of 5 FirstFirst 12345 LastLast

    Similar Topics

    1. Mtangazaji wa CTN Rahma Aziz
      By Mwana Mpotevu in forum Celebrities Forum
      Replies: 26
      Last Post: 24th December 2011, 17:25
    2. Huyu Kasiga ni dada yake Rahma Kharoos Kasiga wa Jakaya?
      By mpayukaji in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 3
      Last Post: 7th December 2011, 10:23
    3. RIP Rahma Swai - Miss Mtwara 2011/12
      By Stany in forum Celebrities Forum
      Replies: 64
      Last Post: 1st November 2011, 19:11
    4. Replies: 7
      Last Post: 21st October 2010, 20:03

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...