Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Pendekezo: JamiiForums iandae ajenda yake ya Uchaguzi Mkuu

    Report Post
    Results 1 to 7 of 7
    1. #1
      Sheba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 199
      Rep Power : 553
      Likes Received
      83
      Likes Given
      34

      Default Pendekezo: JamiiForums iandae ajenda yake ya Uchaguzi Mkuu

      Waungwana,

      Imekuwa ni ada sasa kwa wanasiasa na hasa katika Bunge letu tukufu kusisitiza aidha umuhimu wa kujipanga au kusema kuwa sasa wanajipanga au wamejipanga. Tatizo kubwa ni kuwa, toka msisitizo wa kujipanga umeanza hakuna anayezungumzia kujipangua.

      Lakini, kwa tuliopitia JKT hata wale wachambuzi wa mpira tunafahamu kuwa wakati fulani kikosi kinalazimika kujipangua ikiwa ni mbinu ya kujipanga upya, hususan pale ambapo mpango wa kwanza umejikuta umekwama. Ni maoni yangu kuwa, dhana hii inaweza pia kuwa na mantiki katika siasa na utawala.

      Ndani ya Jukwaa hili tumejipanga kila kukicha kulaumu, kudhihaki na kukosoa bila mafanikio, je si wakati wa Jukwaa hili kujipangua kwa kujitokeza na vipaumbele vya Agenda ya Jamii Forum ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 na kuinadi kwa wagombea na vyama kuisimamia na kuiweka katika ilani zao? Hatutakuwa tumetenda haki zaidi sisi wasomi kwa taifa letu?

      Kama hivyo ndivyo, uchaguzi mkuu na chaguzi za ndani ya vyama vinabisha hodi mbele yetu.................. ni maeneo gani kumi ya vipaumbele tunadhani yanatakiwa kupanguliwa au tunapaswa kama taifa kujipangua? Maeneo haya yanaweza kuandaliwa kama Agenda ya Jamii Forum ya Uchaguzi Mkuu 2010 na kushawishi wagombea na vyama kubeba agenda hizo katika ilani zao.

      Tusipofanya hivyo, ipo hatari ya Jukwaa letu hili tukufu kutumika kujadili watu na kuchafuana badala ya 'issues' za msingi na haja za wananchi wetu.

      Napendekeza Mwanakijiji na moderator waratibu mchakato huu kwa kuanzia.


      Nawasilisha waungwana!
      Argue Dont Shout,shouting will make it worse.......if you are forced to be really nasty, don't shout;use ridicule instead. Ridicule is argument; and it requires knowledge!-Mwl.Nyerere 1969

    2. Miaka 50

    3. #2
      Kakati's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th April 2009
      Posts : 119
      Rep Power : 538
      Likes Received
      11
      Likes Given
      13

      Default Re: Kujipanga ni Kujipangua..? Pendekezo la Agenda ya Jamii Forum ya Uchaguzi Mkuu 20

      Sheba,

      Nadhani ingekuwa bora kama ungesema hayo unayoyafikiria.
      Development is unfortunately not about obeying law but refusing any traces of the unjust part of it.

    4. #3
      Kiby's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2009
      Posts : 3,500
      Rep Power : 1189
      Likes Received
      599
      Likes Given
      33

      Default Re: Kujipanga ni Kujipangua..? Pendekezo la Agenda ya Jamii Forum ya Uchaguzi Mkuu 20

      Mkuu mi nadhani maoni yako ni mazuri ila kwa upande wangu, wanaotakiwa kujipangua ni chama tawala kwasababu hapa kwetu kinaonekana kuwa chama dola. Ilani zake zilizoandaliwa na wasomi hazitekelezeki, na sababu haijulikani kama ni waalimu wa chuo kikuu wanaandaa mtihani halafu wasahihishaji ni waalimu wa shule za msingi, ama ni sababu ya wadanganyika wengi kuwa hawajitambui na hivyo kuwafanya watawala kutumia uzoefu tu kuburuza nchi.

      Hivyo wapinzani wajipange kutetea

      (1) katiba inayoendana na mfumo wa vyama vingi.
      (2) Tume huru ya uchaguzi
      (3)Uundwaji wa mfumo uliyo wazi wa kulinda mali za serikali zisetumike kukampenia chama chochote.
      (3)Watumishi wa serikali mfano wa wakuu wa mikoa, wilaya kutojihusisha na harakati zozote za chama cha siasa. Na kama watafanya hivyo basi wapoteze mamlaka yao kikatiba na kubakia kuwa wapembe wa mkuu fulani wa chama cha siasa.

      Kila mwenye kutimiza vigezo vya kupiga kura awe ameandikishwa kabla ya siku ya uchaguzi.

      NB. Kama masuala muhimu hayazingatiwi ni afadhali uchaguzi kuahirishwa hata kwa baazi ya miaka kuliko kuwa wabeba muhuri wa kuihalalisha ccm kutawala milele.

    5. #4
      Sheba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 199
      Rep Power : 553
      Likes Received
      83
      Likes Given
      34

      Default Re: Kujipanga ni Kujipangua..? Pendekezo la Agenda ya Jamii Forum ya Uchaguzi Mkuu 20

      Quote By Kiby
      Mkuu mi nadhani maoni yako ni mazuri ila kwa upande wangu, wanaotakiwa kujipangua ni chama tawala kwasababu hapa kwetu kinaonekana kuwa chama dola. Ilani zake zilizoandaliwa na wasomi hazitekelezeki, na sababu haijulikani kama ni waalimu wa chuo kikuu wanaandaa mtihani halafu wasahihishaji ni waalimu wa shule za msingi, ama ni sababu ya wadanganyika wengi kuwa hawajitambui na hivyo kuwafanya watawala kutumia uzoefu tu kuburuza nchi.
      Hivyo wapinzani wajipange kutetea
      (1) katiba inayoendana na mfumo wa vyama vingi.
      (2) Tume huru ya uchaguzi
      (3)Uundwaji wa mfumo uliyo wazi wa kulinda mali za serikali zisetumike kukampenia chama chochote.
      (3)Watumishi wa serikali mfano wa wakuu wa mikoa, wilaya kutojihusisha na harakati zozote za chama cha siasa. Na kama watafanya hivyo basi wapoteze mamlaka yao kikatiba na kubakia kuwa wapembe wa mkuu fulani wa chama cha siasa.
      (1)Kila mwenye kutimiza vigezo vya kupiga kura awe ameandikishwa kabla ya siku ya uchaguzi.
      NB. Kama masuala muhimu hayazingatiwi ni afadhali uchaguzi kuahirishwa hata kwa baazi ya miaka kuliko kuwa wabeba muhuri wa kuihalalisha ccm kutawala milele.
      Kiby,Asante kwa maoni yako. Nakubaliana kimsingi na hoja ulizotoa hapo chini. Wasiwasi wangu ni kuwa agenda nzima ya JF ya Uchaguzi Mkuu 2010 itakosa maana ikiwa itajikita kuunga upinzania dhidi ya Chama tawala. Maono yangu katika hili ni kuwa na agenda mtambuka na za kitaifa......... kama ambavyo umeziainisha vizuri. Kwa vyovyote vile wadau humu ndani wataleta agenda nyingine zinazohitaji kuzingatiwa. Mwishoni tunaweza kujikuta na agenda mia. lakini zingine zikiwa zinashahabiana na zingine si za msingi. Tukifika hapo tunaweza kuzipunguza na kuzioanisha na kisha na kuwa vipaumbele kumi. Tukifika hapo, sasa tunaanza kuzinadi na kushawishi vyama kuvibeba. Unaonaje? Hatutakuwa tumesaidia taifa badala ya lawama tu?
      Argue Dont Shout,shouting will make it worse.......if you are forced to be really nasty, don't shout;use ridicule instead. Ridicule is argument; and it requires knowledge!-Mwl.Nyerere 1969

    6. #5
      Regia Mtema's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 21st November 2009
      Posts : 2,988
      Rep Power : 1111
      Likes Received
      763
      Likes Given
      397

      Default Re: Pendekezo: JamiiForums iandae ajenda yake ya Uchaguzi Mkuu

      Naunga mkono hoja.Ni vema JF tukaandaa agenda ya uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.Tuchangie kwa pamoja agenda hizo.This is a very good idea.
      Kilombero For Change(K4C)-Mfuko wa Maendeleo Kilombero

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      Kinyamana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2008
      Posts : 772
      Rep Power : 720
      Likes Received
      107
      Likes Given
      291

      Default Re: Pendekezo: JamiiForums iandae ajenda yake ya Uchaguzi Mkuu

      Mkuu Sheba,nadhani ingependeza kama ungeanza kwa kuonyesha njia! Hoja yako ina mshiko lakini wewe mtoa hoja ungeleta agenda ambazo unafikiri zingefaa kuwa-adopted na JF kama ajenda za uchaguzi mkuu na wengine nasi tukaumiza kichwa kuleta dondoo zetu.

    9. #7
      Kaa la Moto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th April 2008
      Location : Bristol
      Posts : 6,829
      Rep Power : 1944
      Likes Received
      431
      Likes Given
      4199

      Default Re: Pendekezo: JamiiForums iandae ajenda yake ya Uchaguzi Mkuu

      Agenda namba moja kuwe na mabadiliko ya Katiba ya nchi hii ambayo ndio msingi wa matatizo mengi sana. Na ijadiliwe na watanzania wote si wanasiasa wachache tu. Tunahitaji kukubaliana kuhusu hili.
      wakati Cuf wanataka kuchukua nchi mwaka 2000 CCM walikuja na single ya kusema Cuf ni waislamu na kwa sasa wanadai sisi Chadema ni chama cha wakristo sasa CCM nacho ni cha watu gani? Watu wakajibu mashetaaaaaniiiiii.!---Wana Kigoma.

      ....Pamoja na kansa ya uongozi wa CCM watu wataendelea kukichagua,au watu wanaweza wakachoka na kusema potelea mbali wakachagua chama KINGINE....Julius. Kambarage. NYERERE"

    Similar Topics

    1. Replies: 62
      Last Post: 17th June 2011, 09:10
    2. Replies: 1
      Last Post: 22nd November 2010, 14:49
    3. JamiiForums kuwa na waangalizi katika uchaguzi mkuu
      By Kaa la Moto in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 19
      Last Post: 23rd October 2010, 15:37
    4. Zitto Kabwe Na Ajenda Yake Moja
      By Sumaku in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 41
      Last Post: 14th July 2009, 13:12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...