Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

    Report Post
    Page 3 of 12 FirstFirst 12345 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 239
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22297

      Default Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Wanabodi,

      Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimekubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai yuko fit, japo he looks sick), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, them matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali, mkatae!.

      Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena, endapo and only if itamsimamisha Lowassa!.

      1. Uwezo wa Kupanga, Kusema, Kusimamia na Kutenda.
      Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kupanga wa kusema tuu, (Mkukuta, Mkumbita, Mkurabita, Mkuza, na sasa Dira 2025), lakini hawana uwezo wa kusimamia na kutenda!, mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na vitendo sifuri!. Edward Lowassa sio msemaji, bali ni mtendaji, yeye sio mtu wa maneno mingi, ni mtu wa vitendo virefu, he is an action oriented man!.

      Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Elimu, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile mising minne tulisahau capital!.

      Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo la siasa safi na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Elimu ni adui, lakini we never invested because we had no capital. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana na IMF, WB etc matokeo tunayajua!.

      Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, akafanya study tour ya tulioanza nao kwanini wao wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha nyuma sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!.

      Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu, tumeibiwa madini kwa sababu hatuna elimu ya madini, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu elimu ya gesi, kwa kifupi, hutujui lolote na tutaishia kuibiwa tena gesi yetu kwa kukosa elimu ya gesi!. EL ameshauri, lets invest kwenye elimu kwanza ili kuwa empower watu wetu kielimu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kilimo kwanza gesi etc!.

      Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

      Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayewa kusimama na Lowassa kwenye urais na bado akaambulia kura!, there is none, no one!.

      Mwenye masikio na asikie!.

      2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.

      Najua wapinzani wa dhana ya ukweli, watakuja na hoja za dhambi kubwa ya Lowassa ni Richmond!, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipa Simbion capacity charge ile ile ya dola 152 kama Richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanyaga moto, tumeruka maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.

      3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hana wa Kushindana Nae!.

      Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli CCM itamsimamisha, then, 2015, ni CCM tena, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yoyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulaini kama kumsukuma mlevi!.

      Mwisho.

      Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali huu ukweli mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa? au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa kutegemea katiba mpya ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

      Asante.

      Pasco.

      NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.
      Last edited by Pasco; 29th August 2012 at 07:26.
      MTENDAHAKI and MsemajiUkweli like this.

    2. Miaka 50

    3. #41
      Kashaijabutege's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 20th October 2010
      Location : Kabuteigi
      Posts : 1,918
      Rep Power : 823
      Likes Received
      371
      Likes Given
      241

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      LOWASSA ana roho ya paka, na ndiye amebeba robo ya "roho" ya CCM!
      Pasco and Henge like this.
      NAKUSHUKURU MUNGU KWA KUIADHIBU CCM MCHANA KWEUPE, BABA NINAKUOMBA UZIDI KUWAUMBUA, KWA KUYAWEKA WAZI MCHANA WANAYOYAFANYA USIKU. OMBI KWA MUNGU: MUNGU WEWE NI MWEZA WA YOTE, NA SIKU ZOTE UNAYASIKILIZA MAOMBI YA WAKUCHAO, NAKUOMBA UKAFUNGE NGUVU ZA GIZA ZINAZOINYEMELEA M4C; NA UVUNJE MIPANGO YOTE YA MASHETANI WALIOPO NDANI YA CHADEMA. AMINA

    4. #42
      Jibaba Bonge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2008
      Posts : 1,003
      Rep Power : 764
      Likes Received
      145
      Likes Given
      61

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Pasco, imekuwaje umekuwa rahisi kiasi hicho?!! Yaani two- series za kipindi cha Kipima Joto cha ITV kuhusu Lowasa zimetosha kukununua?! Are you cheap to such an extent?

      Achilia mbali hizo dakika 90 ulizomsikiliza; sisi tumeuona utendaji wake wa kazi, alishakuwa waziri kwa miaka mingi tu huko nyuma na akawa Waziri mkuu kwa miaka miwili na kitu hivi, na huo utendaji wake ndiyo ulimfikisha hapo alipo! Kama aliibeba mizigo ya watu asiikatae mapema wakati hiyo mizigo inaandaliwa? Angeonekana wa maana sana kama angekataa kubeba mizigo ya watu kwa maslahi ya watanzania.

      Hivi unayemsema ni huyu huyu Lowasa aliyeshindwa kuelezea uhalali wa mali zake alipoulizwa na Nyerere wakati anagombea kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya ccm mwaka 1995?
      Pasco likes this.

    5. #43
      Domhome's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th June 2010
      Location : Chimbo
      Posts : 703
      Rep Power : 592
      Likes Received
      182
      Likes Given
      142

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Quote By Mzalendo80
      Huyu Lowassa atatuumizia akili za kaka yetu Pasco.

      Lowassa, he will never be a President of this Republic hata akigombea na Jiwe ni uhakika kuwa Jiwe litashinda. Lowassa ni mmoja waliomo kwenye list of Shame, alitajwa na rais wetu Dr Slaa kuwa ni fisadi kama Kikwete alivyo, still no difference mwizi ni mwzi tu hata ukimpa manyoya ya kuku bado ataiba hata mavi ya kuku.

      Pasco you real need help ASAP
      .....Sidhani kama afya yake itamruhusu...anyway, hata kama atafika y2015 hataweza hata kuongea tena...atakuwa kitandani....binafsi natamani sote tufike hiyo y2015 ili tujioneee...lakini afya ya mwenzetu EL, inasua-sua!!

      Mark my words!

      Pasco likes this.
      “It’s now the moment for political baboons to see their backsides” - Time for politicians to look at themselves in the mirror! (Kenyan human right's activist)

    6. #44
      N-handsome's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd January 2008
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 1,859
      Rep Power : 950
      Likes Received
      91
      Likes Given
      478

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      He is good but ni babu jamani, alikuwa wapi siku zote kupigania masilahi ya nchi mpaka aje wakati keshaanza tetemeka?
      Pasco likes this.

    7. #45
      Cynic's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th January 2009
      Location : Around
      Posts : 2,157
      Rep Power : 968
      Likes Received
      317
      Likes Given
      186

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Pasco hapa sana sana ulichofanya ni kwamba umetutukana wtz
      Pasco likes this.
      '... Knowledge is good, but wisdom is even better ...'

    8. #46
      HOMOSAPIEN's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st March 2011
      Posts : 484
      Rep Power : 509
      Likes Received
      131
      Likes Given
      42

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Aje.aje,atajua kuwa waTZ tuko wengi sasa na tumeenda shule,kwanini majina yaleyale tu kwani hakuna wengine?kama ni hivyo wamfufue nyerere agombee tena,tumeshachoka na majina yaleyale kila siku,tuoneeni huruma sasa alaa!!!!!
      Pasco likes this.
      THE FUTURE ALWAYS START TOMORROW AND NOT TODAY

    9. #47
      chomete's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th December 2010
      Posts : 1,056
      Rep Power : 638
      Likes Received
      107
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      hivi pasco umepewa pesa, basi lowasa aje chadema tumpenchi sisi kitu ambacho atutaki ni ccm kuingoza hii nchi
      Pasco likes this.
      mura

    10. #48
      Henge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 5,440
      Rep Power : 1675
      Likes Received
      918
      Likes Given
      1673

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      pasco umeuzwa na umenunulika daaah SORRY BROTHER!
      Pasco likes this.
      TUKIWAKAMATA MAFISADI NCHI ITAYUMBA by PINDA

    11. #49
      Johnsecond's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2010
      Posts : 933
      Rep Power : 650
      Likes Received
      152
      Likes Given
      65

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Quote By Kivumah
      Quote: NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.

      ..Leo ndio nimekusoma itikadi yako Brother Pasco!!. Leka Tutigite
      i wish ningekuwa namjua huyu jamaa maana atakuwa anapata vihela hela aliowataja hapo wote ni very corrupt. Amini usiamini hao wote ni matajiri sana na wanajua kuhonga. Nimekuwa nikijiuliza huyu Pasco usimtaje zito kwa lolote anakurupuka tena kwa speed, mara JK constructive opinion sijui. Hutafika mbali
      Pasco likes this.

    12. #50
      Johnsecond's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2010
      Posts : 933
      Rep Power : 650
      Likes Received
      152
      Likes Given
      65

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Quote By Jibaba Bonge
      Pasco, imekuwaje umekuwa rahisi kiasi hicho?!! Yaani two- series za kipindi cha Kipima Joto cha ITV kuhusu Lowasa zimetosha kukununua?! Are you cheap to such an extent?

      Achilia mbali hizo dakika 90 ulizomsikiliza; sisi tumeuona utendaji wake wa kazi, alishakuwa waziri kwa miaka mingi tu huko nyuma na akawa Waziri mkuu kwa miaka miwili na kitu hivi, na huo utendaji wake ndiyo ulimfikisha hapo alipo! Kama aliibeba mizigo ya watu asiikatae mapema wakati hiyo mizigo inaandaliwa? Angeonekana wa maana sana kama angekataa kubeba mizigo ya watu kwa maslahi ya watanzania.

      Hivi unayemsema ni huyu huyu Lowasa aliyeshindwa kuelezea uhalali wa mali zake alipoulizwa na Nyerere wakati anagombea kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya ccm mwaka 1995?
      Ni lini Pasco amekuwa mgumu, he is always easy going
      Pasco likes this.

    13. #51
      Mwita Maranya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2008
      Location : Ikorongo Game Reserve
      Posts : 7,999
      Rep Power : 12012
      Likes Received
      5321
      Likes Given
      5154

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Quote By Pasco
      1. Uwezo wa Kupanga, Kusema, Kusimamia na Kutenda.
      Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kupanga wa kusema tuu, (Mkukuta, Mkumbita, Mkurabita, Mkuza, na sasa Dira 2025), lakini hawana uwezo wa kusimamia na kutenda!, mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na vitendo sifuri!. Edward Lowassa sio msemaji, bali ni mtendaji, yeye sio mtu wa maneno mingi, ni mtu wa vitendo virefu, he is an action oriented man!.
      Mambo mengine mtu unapoyaandika ama kuyazungumza unahitaji walau dakika mbili za kuyatafakari.
      Huyu lowasa wa monduli tunayemfahamu ndiye mtu wa vitendo ama ni mwingine?
      Pasco unaweza kutueleza hapa ni vitu gani tangible ambavyo Tanzania kama taifa tumenufaika na utumishi wa lowasa tangu akiwa AICC hadi akiwa naibu waziri na waziri katika wizara mbalimbali na hatimaye kuwa waziri mkuu?? sitaki uniambie porojo nataka unitajie vitu ambavyo alikaa chini akafikiria na kuvianzisha kisha akavisimamie utekelezaji wake.

      Usiniambie habari ya shule za kata kwani hilo ni wazo "aliloliiba" kutoka kwa watanzania wazalendo wa kweli. Pasco labda nikufahamishe kwamba sisi wilyani Serengeti tulipitisha uamuzi wa kujenga shule ya sekondari kila kata na kuanzia mwaka 1998/1999 tulikuwa tumejenga ama kuanza ujenzi wa shule za sekaondari katika kila kata. Nakumbuka shule nyingi za kata zilifunguliwa kati ya mwaka 1999-2000. Wakati huo lowasa wa monduli hajui kama atakuja kuwa waziri mkuu wa nji hii.

      Sasa pasco nikumbushe kingine alichofanya lowasa wa monduli zaidi ya kujilimbikizia mali kiasi kwamba alipogombea uraisi mwaka 1995 mwalimu Nyerere alipomhoji ni wapi alipopata huo utajiri wake alishindwa kumjibu na akatolewa katika kinyang'anyiro.
      Pasco likes this.
      Honesty is a very expensive GIFT. Do not expect it from cheap people.

    14. #52
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22297

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Quote By Mwita Maranya

      Mkuu Mwita Maranya, uwezo wa EL unafahamika, power yake kubwa ni pamoja na uwezo wa kufanya maamuzi magumu, la kujiuzulu likiwa ni mojawapo. Naomba nisiorodheshe aliyoyafanya maana nitaongezewa sana bahasha za kumpigia debe, ila ni kweli 1995 alienguliwa kwa kosa la utajiri, jee mpaka 2015, utajiri ni dhambi?.

    15. #53
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22297

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Quote By Henge
      pasco umeuzwa na umenunulika daaah SORRY BROTHER!
      Mkuu Henge, sijauzwa wala sijanunulika, ila mimi kama mwandishi wa kujitegemea, naandika habari niiuze ndio nipate kula yangu, sasa ikitokea mtu akanilipa kuandika na kuposti humu jf, huoni s/he made my job easier, hivyo sasa jf ndio ofisini kwangu, na ndio maana nashinda humu 24/7, kuna ubaya?.

    16. #54
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22297

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Quote By Cynic
      Pasco hapa sana sana ulichofanya ni kwamba umetutukana wtz
      Mkuu Cynic, nimewatukana kivipi?.

    17. #55
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22297

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Quote By Jibaba Bonge
      Pasco, imekuwaje umekuwa rahisi kiasi hicho?!! Yaani two- series za kipindi cha Kipima Joto cha ITV kuhusu Lowasa zimetosha kukununua?! Are you cheap to such an extent?

      Achilia mbali hizo dakika 90 ulizomsikiliza; sisi tumeuona utendaji wake wa kazi, alishakuwa waziri kwa miaka mingi tu huko nyuma na akawa Waziri mkuu kwa miaka miwili na kitu hivi, na huo utendaji wake ndiyo ulimfikisha hapo alipo! Kama aliibeba mizigo ya watu asiikatae mapema wakati hiyo mizigo inaandaliwa? Angeonekana wa maana sana kama angekataa kubeba mizigo ya watu kwa maslahi ya watanzania.

      Hivi unayemsema ni huyu huyu Lowasa aliyeshindwa kuelezea uhalali wa mali zake alipoulizwa na Nyerere wakati anagombea kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya ccm mwaka 1995?
      Mkuu Jibaba Bonge, kwanza nakiri udhaifu, mimi ni very cheap, kwa kifupi sina bei kabisa!, dakika 15 tuu zingetosha, hivyo hizo 90 ndio kabisa nimemconfirm huyu jamaa ndie the best we have so far, unless otherwise!.

      Kosa la EL ni kuwa na nidhamu ya hali ya juu, nidhamu ni kutenda kila unaloambiwa bila kuuliza chochote, na baada ya kukamilisha kazi ndipo una lodge complain, safari ya kuelekea 2015 imeanza, tutakafika darajani, ataitua mizigo yote ili atuvushe salama!.

    18. #56
      Karikenye's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 405
      Rep Power : 492
      Likes Received
      192
      Likes Given
      173

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Quote By Pasco
      Wanabodi,

      Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimekubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai yuko fit, japo he looks sick), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, them matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali, mkatae!.

      Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena, endapo and only if itamsimamisha Lowassa!.

      1. Uwezo wa Kupanga, Kusema, Kusimamia na Kutenda.
      Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kupanga wa kusema tuu, (Mkukuta, Mkumbita, Mkurabita, Mkuza, na sasa Dira 2025), lakini hawana uwezo wa kusimamia na kutenda!, mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na vitendo sifuri!. Edward Lowassa sio msemaji, bali ni mtendaji, yeye sio mtu wa maneno mingi, ni mtu wa vitendo virefu, he is an action oriented man!.

      Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Elimu, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile mising minne tulisahau capital!.

      Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo la siasa safi na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Elimu ni adui, lakini we never invested because we had no capital. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana na IMF, WB etc matokeo tunayajua!.

      Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, akafanya study tour ya tulioanza nao kwanini wao wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha nyuma sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!.

      Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu, tumeibiwa madini kwa sababu hatuna elimu ya madini, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu elimu ya gesi, kwa kifupi, hutujui lolote na tutaishia kuibiwa tena gesi yetu kwa kukosa elimu ya gesi!. EL ameshauri, lets invest kwenye elimu kwanza ili kuwa empower watu wetu kielimu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kilimo kwanza gesi etc!.

      Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

      Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayewa kusimama na Lowassa kwenye urais na bado akaambulia kura!, there is none, no one!.

      Mwenye masikio na asikie!.

      2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.

      Najua wapinzani wa dhana ya ukweli, watakuja na hoja za dhambi kubwa ya Lowassa ni Richmond!, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipa Simbion capacity charge ile ile ya dola 152 kama Richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanyaga moto, tumeruka maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.

      3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hana wa Kushindana Nae!.

      Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli CCM itamsimamisha, then, 2015, ni CCM tena, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yoyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulaini kama kumsukuma mlevi!.

      Mwisho.

      Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali huu ukweli mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa? au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa kutegemea katiba mpya ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

      Asante.

      Pasco.

      NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.
      Naona PASCO tatizo halisi la NYINYIEM siyo individuals ni tatizo la kimfumo ni tatizo la kitaasisi EL kama EL hata afanyaje hawezi kuubadili... aidha je, unajua alipoenda kwa TB Joshua Nigeria aliambiwa nini? Mtafute umuulize atakwambia.... IN short anajua HE IS NOT THE NEXT PRESIDA wa Tanzania.... na CCM wanajua wakimsimamisha... IMEKULA kwao! Na hawatamsimamisha take it from me! Sasa kinyume chake wakimsimamisha CDM ndio watachukua NCHI kama wananawa!

    19. #57
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22297

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Quote By ZeMarcopolo
      Tanzania ina watu zaidi ya milioni 40. zoezi la sensa linaweza kutuambia tuko mil 50!
      Kuwa obsessed na mtu mmoja katika nchi yenye watu wengi kiasi hicho ni tatizo.
      Mkuu Ze Marcopolo, sio obsession kwa sababu sababu pia nimeziweka, siku zote huwa nawaambia humu, kama na ninyi mnao watu wenu wowote ambao ni bora zaidi ya EL, watajeni waleteni!, kwa uono wangu, CCM has no one else better than EL akifuatiwa na Membe, who else?.

    20. #58
      Lambardi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th February 2008
      Location : KITAANI ZAIDI
      Posts : 4,532
      Rep Power : 1799
      Likes Received
      657
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      CCMabwepande wasipomsimamisha EL wajue wameliwa!!hata kubali ataisambaratisha kabisa na watajuta!

    21. #59
      Didia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2010
      Posts : 336
      Rep Power : 500
      Likes Received
      60
      Likes Given
      55

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Pasco nakumbuka miezi si mingi ulikuwa umemuasi kipenzi chako EL vipi amekununua tena? Tukumbuke hii

      "Yametimia!, CCM Imechokwa!, Chadema Njia Nyeupe 2015!-Jipangeni!

      Wanabodi,
      Mara tuu baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010, nilipandisha uzi wa "CCM Imechokwa!, Chadema Haijajipanga"!. Leo baada ya matokeo ya uchaguzi mdogo wa Arumeru, nimethibitisha kuwa ni kweli CCM Imechokwa, hivyo yale maneno yangu ya 2010, sasa yanatimia!. CCM sasa ni "sikio la kufa..." na kama ni tunda, basi ni "lakuvunda..."
      Katika mada hiyo, nilisema Chadema, haijajipanga!. Ushindi wa Arumeru, sio uthibitisho kuwa sasa Chadema ndio imejipanga, no!, ni uthibitisho tuu kuwa CCM imechokwa, Wananchi wameamka na sio watu wa kuswagwa na kupelekwa pelekwa tuu kama ling'ombe!.

      Ushindi huu wa Arumeru, ni uthibitisho kuwa Chadema mkiamua, mnaweza!. Ushindi huu, umewafungulia njia kuelekea 2015, yaani njia ni nyeupe!, kilichobakia ni kujipanga kwa kupanga mipango mkakati na kuunda kikosi kazi kitakachokabidhiwa malengo na kujadili utekelezaji with time frame, 2015, Ikulu ya Magogoni ni yenu!.

      Kwa wale mliokuwa mkinifuatilia kwa siku nyingi, nimekuwa nikimpigania EL ili awe mgombea wa CCM, kwa imani kuwa ndio most ambitious and the easiest to defeat, ili mgombea wa Chadema, amsukume kama kumsukuma mlevi! nikihofia CCM ikiwasimamisha watu makini kama Magufuli, Dr. Shein etc, itakuwa sio rahisi kuwashinda!.

      Kwa vile ushindi wa Arumeru ndio indicator ya 2015, na kwa vile CCM imechokwa!, hata ikimsimamisha nani, down the drain, atakwenda na maji, kwa sababu hiyo, sina tena sababu ya kushabikia CCM kuwasimamisha the weak kama Lowassa au Membe, let CCM iwasimamishe their strongest ever, down with it wata zama nayo!.

      Mimi sio mwana CCM bali imetokea Sioi kuwa ni rafiki yangu. Mimi ndiye nilikuwa MC wake wakati wa harusi yake, hivyo loyality is all "what friends are for", na nimesimama nae, mpaka mwisho na nimeanguka nae!. Pole Sioi, poleni wana CCM, huu ni ukweli mchungu kumeza!.

      Kufuatia chaguzi ndogo za Busanda na Biharamulo, nilijiaminisha kwa asilimia 100% kuwa Watanzania ni wale wale na CCM ni ile ile, na kuwa sio inachaguliwa kwa kupendwa, bali imekuwa ikichaguliwa kwa mazoea, maadam sasa imechokwa, hakuna namna ya kuiokoa, safari ya kuelekea kaburini imewadia, kilichobakia ni kusubiria tuu itakufa kifo gani!.

      Namalizia kwa kuipongeza sana Chadema, hongera sana Nasari, na pia naomba nimpongeze mwana jf mwenzetu, Mzee Mwanakijiji kwa "ule waraka".

      Naomba kuiweka ile mada ya msingi for reference.

      Asanteni.

      Pasco."

    22. #60
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,207
      Rep Power : 5042
      Likes Received
      2438
      Likes Given
      2230

      Default Re: Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then 2015, ni CCM Tena!.

      Quote By Pasco
      Mkuu Ze Marcopolo, sio obsession kwa sababu sababu pia nimeziweka, siku zote huwa nawaambia humu, kama na ninyi mnao watu wenu wowote ambao ni bora zaidi ya EL, watajeni waleteni!, kwa uono wangu, CCM has no one else better than EL akifuatiwa na Membe, who else?.
      Well, I think you have to reverse the order...
      "To greed, all nature is insufficient"

    Page 3 of 12 FirstFirst 12345 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...