Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

    Report Post
    Page 3 of 3 FirstFirst 123
    Results 41 to 50 of 50
    1. #1
      Bujibuji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2009
      Location : NYUMBANI PANONO
      Posts : 13,800
      Rep Power : 11185
      Likes Received
      6989
      Likes Given
      5168

      Default Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

      RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa bado Serikali ina dhamira ya kuileta moja ya timu za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania, 'La Liga' kuja Tanzania na amemtaka Balozi mpya wa Hispania nchini kusaidia kufanikisha mpango huo.

      Aidha, Kikwete ameipongeza Hispania kwa kufanikiwa kutetea ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya katika mashindano yaliyomalizika mwezi uliopita nchini Poland na Ukraine. Rais Kiwete alisema hayo jana Ikulu, jijini Dar es Salaam katika hafla ya utambulisho wa balozi mpya wa Hispania nchini, Luis Manuel Cuesta Civis.

      Kikwete alisema: “Wananchi wa Tanzania, ambako timu za Hispania, zina washabiki na wafuasi wengi, bado wanasubiri kwa hamu ziara ya moja ya timu kubwa za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania. Tunataka ije hapa, icheze mechi moja ama mbili na itembelee mbuga zetu maarufu za wanyama.”

      Aliongeza:“Kama utakavyokuja kuthibitisha mwenyewe, Watanzania ni watu wanaopenda michezo na hasa soka na ni wafuatiliaji wakubwa wa Ligi Kuu ya Hispania ambako timu zenye mvuto zaidi ni Real Madrid na Barcelona.”

      “Tunawapongeza sana kwa kuweka historia. Kwanza mlishinda Kombe la Mataifa ya Ulaya, kisha mkashinda Kombe la Dunia. Sasa mmeweza kutetea Kombe la Ulaya. Hili halijapata kutokea kwa nchi moja kushikilia vikombe vyote viwili vikubwa vya soka duniani kwa wakati mmoja ama nchi kutetea Kombe la Ulaya.”

      Wakati huohuo, serikali imesema imeridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wanamichezo walioshiriki michezo ya Olimpiki iliyomalizika Jumapili iliyopita, London, England.

      Pamoja na wanamichezo hao kurudi bila medali, lakini serikali imesema wanastahili pongezi kwa vile walijitahidi kushindana kadri walivyoweza. Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Leonard Thadeo wakati wa hafla ya chakula cha usiku kwa wanamichezo iliyofanyika muda mfupi baada ya kuwasili.

      "Mmetujengea heshima kubwa Olimpiki, miaka ya nyuma wanamichezo wetu waliokuwa wakituwakilisha baada ya mashindano wanazamia uko, lakini nyinyi hakufanya hivyo" alisema Thadeo.

      Mbali na kuwapongeza wanamichezo hao, pia Thadeo aliwakabidhi vyeti na medali za ushiriki kwenye michezo ya Olimpiki. Katika michezo hiyo, Tanzania iliwakilishwa na wanamichezo wa masumbwi, riadha na kuogelea, ambapo waliishia hatua ya makundi.

    2. Miaka 50

    3. #41
      Kapo Jr's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2011
      Posts : 374
      Rep Power : 494
      Likes Received
      37
      Likes Given
      0

      Default Re: Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

      Shame on mr dhaifu,he think to entertains tanzanians while they are tired with his admnistration-he cheated himself

    4. #42
      babacollins's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd December 2010
      Posts : 435
      Rep Power : 436
      Likes Received
      74
      Likes Given
      52

      Default Re: Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

      Quote By MAMMAMIA
      Ombi zuri lakini kwa mwaka huu haiwezekani tena kwani msimu wa La Liga ambao unaanza kesho tarehe 18/8 hadi tarehe 01/06/2013.

      Ikumbukwe kuwa muda pekee timu za ligi ya Spain na Ulaya kwa jumla zinakuwa na ratiba iliyobanana sana wakati msimu unaanza kwani mbali na mechi za ndani, kunakuwa na mashindano ya Ulaya. Wakati pekee timu zinapokuwa huru kidogo ni pale wanapomaliza msimu.

      Mhe. Raisi afuatilie ili ikiwezekana ziara hizo ziweze kufanyika baada ya msimu huu kumalizika.
      Huyu mkuu wa nchi king'ang'anizi! toka enzi za zidane!

    5. #43
      Inkoskaz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 6th November 2010
      Location : URT
      Posts : 4,396
      Rep Power : 7348
      Likes Received
      1060
      Likes Given
      1088

      Default Re: Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

      hizo mapesa ya kuteketea kuzilipa klabu hizo yangetumika kujenga academi za michezo kwa kanda kama tano hivi
      kanda ya ziwa-mpira,uogeleaji na makasia
      kanda ya nyanda za juu kusini -mpira na ngumi
      kanda ya kati na kaskazini -riadha
      kanda ya Pwani na Mashariki-Basketball,Mpira,bao,uogeleaji na makasia
      kanda ya kaskazini magharibi-shabaha nk
      Thinking is the hardest work there is,which is probably the reason why so few engage in it!!

    6. #44
      Nivea's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 5,680
      Rep Power : 0
      Likes Received
      3139
      Likes Given
      4053

      Default Re: Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

      Quote By ritz
      ttb wanahusika na nini?
      gooogle!!!!!!!!!!!!!!!

    7. #45
      giLESi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2011
      Posts : 777
      Rep Power : 535
      Likes Received
      217
      Likes Given
      235

      Default Re: Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

      Haya ni matumizi mabaya ya kodi zetu

    8. Study Abroad

    9. #46
      mandieta's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th February 2012
      Posts : 2,741
      Rep Power : 890
      Likes Received
      269
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By MAMMAMIA
      Ombi zuri lakini kwa mwaka huu haiwezekani tena kwani msimu wa La Liga ambao unaanza kesho tarehe 18/8 hadi tarehe 01/06/2013.

      Ikumbukwe kuwa muda pekee timu za ligi ya Spain na Ulaya kwa jumla zinakuwa na ratiba iliyobanana sana wakati msimu unaanza kwani mbali na mechi za ndani, kunakuwa na mashindano ya Ulaya. Wakati pekee timu zinapokuwa huru kidogo ni pale wanapomaliza msimu.

      Mhe. Raisi afuatilie ili ikiwezekana ziara hizo ziweze kufanyika baada ya msimu huu kumalizika.
      Nani atawalipia gharama ata kama ingekua ligi haijaanza?
      Yani walimu wanalialia yeye prezidar analeta ungesengese hapa!

    10. #47
      MAMMAMIA's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Location : Near You
      Posts : 3,794
      Rep Power : 3256
      Likes Received
      1496
      Likes Given
      1206

      Default Re: Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

      Quote By DUDU JEUSI
      Nani atawalipia gharama ata kama ingekua ligi haijaanza?
      Yani walimu wanalialia yeye prezidar analeta ungesengese hapa!
      Hilo la juu, neno; kwani sio gharama ya kuwaleta tu bali hata kuwalipa. Nakumbuka mwaka jana Barca ilikwenda nchi moja ya Kiarabu, mapesa waliyolipa ni bajeti yetu ya mwaka (nimetia chumvi kidogo), na sidhani kama watakuja kufanya kazi ya ukweni.

      Hilo la chini, umepitiliza kidogo. Kama kiongozi wa nchi, pamoja na mapungufu yake yote, anastahiki heshima.
      "JF - SAUTI YA WASIO NA SAUTI ............ na wapayukaji"

    11. #48
      Manyanza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Location : Look Behind You......
      Posts : 4,419
      Rep Power : 25469
      Likes Received
      1143
      Likes Given
      908

      Default Re: Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

      pamoja na matatizo tuliyonayo hapa nchini JK anafikiria kuileta Barca au Real? Huyu JK hata uwezo wa kufikiria umepungua toka Sheikh Yahya amekufa

    12. #49
      Tram Almasi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 26th February 2009
      Location : Marsabit
      Posts : 753
      Rep Power : 671
      Likes Received
      217
      Likes Given
      92

      Default Re: Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

      Quote By King Kong III
      Kweli jamaa ni Janga la Taifa!! Hizo fedha si wangeongeza mosquito nets,mashuka na vitanda kwenye hospital zetu? Kama lengo ni utalii kwani TTB wanafanya kazi gani?
      Talking of utalii,that could be a good move. The world knows about Real Madrid an Barcelona. But very few are familiar with our national parks,taking one of the teams to the parks,all the major media houses will be there hence the world will knw where Ngorongoro is and what they should expect. As a result, more and more tourists vising Tanzania!
      "YouR MoST UNhaPPy CuSToMers ArE YoUr GREateST SOurCE Of LEarNInG"- BiLL GaTEs

    13. #50
      Ngambo Ngali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th April 2009
      Posts : 2,568
      Rep Power : 1027
      Likes Received
      530
      Likes Given
      398

      Default Re: Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

      Quote By peri
      Mmetujengea heshima kubwa Olimpiki, miaka ya nyuma wanamichezo wetu waliokuwa wakituwakilisha ,baada ya mashindano wanazamia uko lakini nyinyi hakufanya hivyo" alisema Thadeo.

      Kweli kuna wachovu wa fikra nchi hii.
      Na huyu Thadeo, sijui Video analipwa kwa kutoa hii verbal diarrhoea. Hawa ndio wa kufukuzwa kazi
      Injustice anywhere is a threat to justice everywhere.

    14. FemaTV & Radio
    Page 3 of 3 FirstFirst 123

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...