Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 25
    1. #1
      LUCIFER's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th August 2012
      Posts : 100
      Rep Power : 361
      Likes Received
      32
      Likes Given
      41

      Default Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Kuna habari kwamba Waziri Mkuu aliyejiuzuru nafasi hiyo kutokana na kashfa ya mkataba tata wa Richmond, Edward Lowasa anajiandaa kuwekeza katika klabu ya Yanga kupitia kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji, ambaye ni swahiba yake mkubwa kibiashara, kama moja ya njia za kumnusuru katika mipango yake ya kuelekea ikulu mwaka 2015.Jaribio la Lowassa kuingia Yanga lilianza kwa utawala wa mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Lloyd Nchunga,ambapo alidaiwa kwamba Lowasa aliomba kuingiza kiasi cha shilingi 800 milioni hasa wakati Manji ambaye alikuwa ndiye mfadhili mkuu wa klabu hiyo, alipogoma kutoa msaada kwa Yanga, lakini Lloyd Nchunga alikataa, linadaiwa kutomfurahisha Lowassa na watu wanaomuunga mkono akiwamo Manji na Rostam Aziz ambaye naye anaelezwa kuwa ni mpenzi wa Yanga.Itakumbukwa wakati wakisuguana na Manji baada ya mfadhili huyo kujiweka pembeni kama mfadhili wa klabu hiyo na baadaye kuonekana akijaribu kujiingiza kwa kutumia mgongo wa wazee wa klabu waliotaka kukabidhiwa timu, Nchunga alihoji wazee hao wangepata wapi fedha zakuendeshea klabu hiyo na akasema hawezi kukabidhi timu kwa watu ambao hajui itaishia mikononi mwa nani kwani huenda wazee hao wanataka kuikabidhi timu hiyo kwa wafanya biashara wa mihadarati.Ingawa hakuwa amemtaja mtu,lakini kauli hiyo ilionekana kuwaudhi wazee hao na kudai Nchunga amewatusi na kumtusi Manji hivyo watahakikisha anaondoka madarakani kwa njia yoyote na ndicho kilichotokea.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga, njama za kuondolewa kwa Nchunga zilitokana kushindwa kufuata matakwa ya matajiri wa klabu hiyo wanaodai wana mpango wa kuifanya Yanga kuwa tajiri, lakini liwe lengo la kujipatia vyeo nchini kutokana na historia ya kuhusika kwake na harakati za uhuru wa Tanzania tangu Tanganyika.Inadaiwa Lowassa anataka pia kuwa karibu na watu wenye sauti kwenye chama cha mapinduzi visiwani Zanzibar akiwemo mama Fatma karume ili kumsaidia kupata umaarufu na kujijenga visiwani, tayari kwa kuwania urais. Inafahamika kwamba viongozi wengi wa Baraza la mapinduzi Zanzibar wana mapenzi na timu ya Yanga kutokana na timu hiyo kuwa na urafiki na timu ya za Afrika Sports na Miembeni tangu wakati wa harakati za kuwania uhuru wa nchi hizi mbili na Lowassa ameliona hili.Inadaiwa kazi ya kumsafishia Lowassa njia ya kuingia kwenye enzi ya klabu hiyo, inafanywa na Yusuf Manji ambaye jukumu lake kubwa alilonalo ni kuhakikisha anaibadili Yanga kuwa kampuni, na kwa kutumia udhaifu wa wanachama na wapenzi wa Yanga kutotaka kujua kinachoendelea katika klabu yao, isipokuwa waifunge Simba tu ama kuchukua ubingwa,ndiyo sababu ambayo wenye fedha wameeleza kuwa ndiyo njia rahisi ya kumpachika Lowassa awe mmoja wa wadhamini wa klabu ya Yanga pamoja na kuwepo kwa madai ya muda mrefu kwamba Lowassa ni Simba damu.Lakini u-simba wake kwa mujibu wa vyanzo vya habari utafunikwa na fedha ambazo atazimwaga klabuni Yanga na ikiwa njia ambayo pia ilitumiwa na mtu mwengine aliyewahi kuingia kwenye uongozi waklabu hiyo, Seif Ahmed Magari ambaye licha ya wanaojua kwa asilimia mia moja niSimba, lakini alitumia udhaifu wa kutochimbua mambo kwa wanayanga na kwa kuwa yeye ni mfanyabiashara wa magari mwenye fedha, akajifanya anaongoza kutoa msaada kwa wanayanga, kumbe nia ilikuwa kuingia Yanga ili ahalalishe ujanjaujanja wake katika biashara zake.Miongoni mwa mambo ambayo yatafanywa Yanga ni pamoja na kuvunja jengo lililojengwa na Karume na Maalimu Nyerere nakulifanya la kisasa zaidi ambapo litajengwa kama lile la Quality Business Centre ambapo ndani yake kutakuwa na uwanja wa kisasa, maduka makubwa na kila aina ya starehe ambako kwa mawazo yao wanaamini watakuwa wamewamaliza wanachama ambao hamu yao ni kuiona Yanga inashinda na kuwa na vitega uchumi, lakini kwa wao lengo lao lilikuwa ni kumweka Lowassa kwenye kiti cha urais mwaka 2015.ANOTHER MOVIE….hayawale Mnaojiita WANAZI WA YANGA MUTIMU WA MAPESA MPO?SOURCE: AFRICA LEO, 8th of August, 2012.
      Last edited by LUCIFER; 14th August 2012 at 10:58.

    2. FemaTV & Radio

    3. #2
      Konaball's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th March 2009
      Posts : 532
      Rep Power : 626
      Likes Received
      41
      Likes Given
      6

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      mhh kama ndio hivyo YANGA itakuwa timu bora kati ukanda wa Africa Mashariki na Kati

    4. #3
      LUCIFER's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th August 2012
      Posts : 100
      Rep Power : 361
      Likes Received
      32
      Likes Given
      41

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Quote By Konaball
      mhh kama ndio hivyo YANGA itakuwa timu bora kati ukanda wa Africa Mashariki na Kati
      na wanachama wake wataongoza kwa Umaskini katika ukanda wa Africa Mashariki na Kati.

    5. #4
      Safari_ni_Safari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2007
      Location : Kibaruani
      Posts : 11,935
      Rep Power : 24142
      Likes Received
      4653
      Likes Given
      2637

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Mhh.......mmiliki wa YANGA (Bw Mkubwa Riziwani) si alishatoa tamko kule Bagamoyo kuwa Rais ajaye hatatoka kaskazini? Hii vipi tena?

      Soki Ozali Mwasi Yaka, Soki Ozali Mobali Koya Te


    6. #5
      Konaball's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th March 2009
      Posts : 532
      Rep Power : 626
      Likes Received
      41
      Likes Given
      6

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Quote By LUCIFER
      na wanachama wake wataongoza kwa Umaskini katika ukanda wa Africa Mashariki na Kati.
      wewe komandoo nini unategemea pesa za club

    7. Miaka 50

    8. #6
      Kaliua urambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st April 2009
      Posts : 437
      Rep Power : 601
      Likes Received
      76
      Likes Given
      24

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Huyu jamaa mbona simba damu kitambo
      Friend's of Zitto " Zitto ze presidential material" uwajibikaji na haki ZZK T2015

    9. #7
      LUCIFER's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th August 2012
      Posts : 100
      Rep Power : 361
      Likes Received
      32
      Likes Given
      41

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Quote By LUCIFER
      na wanachama wake wataongoza kwa Umaskini katika ukanda wa Africa Mashariki na Kati.
      Kwani wanaolipia zile ada za 22,elfu cjui 20 kwa mwaka elfu ni kina nan?si wanachama..mi si komandoo bro....ni FREELANCER ha ha ha

    10. #8
      LUCIFER's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th August 2012
      Posts : 100
      Rep Power : 361
      Likes Received
      32
      Likes Given
      41

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Quote By Konaball
      wewe komandoo nini unategemea pesa za club

      Kwani wanaolipia zile ada za 22,elfu cjui 20 elfu kwa mwaka ni kina nan?si wanachama..mi si komandoo bro....ni FREELANCER ha ha ha

    11. #9
      MKALIKENYA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 709
      Rep Power : 501
      Likes Received
      282
      Likes Given
      407

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Quote By LUCIFER
      na wanachama wake wataongoza kwa Umaskini katika ukanda wa Africa Mashariki na Kati.
      Wewe ndio mpuuzi kweli kwani wanachama wa YANGA wanataka wawe matajiri kupitia YANGA nyie ndio wale hamna shughuli za kufanya mnashinda pale jengo la SIMBA mnamsubiri KABURU aje awape nauli na hela ya kula.

    12. #10
      Anselm's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2010
      Location : Dar-es-salaam
      Posts : 1,471
      Rep Power : 726
      Likes Received
      181
      Likes Given
      138

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Wish I were one of the Mod,ningeweka button ya "USHUZI" habari kama hii(ya mleta thread) inafanania na ile kitu inayotoka mtu anapopumua kwa ile njia nyingine ile.
      Wewe kweli Lucifer unafikiria sisi Wanachama wa Yanga ni Mapoyoyo kama nyinyi,sisi hatuwezi kushangilia picha ya Mwenyekiti wetu amemshika bega Mchezaji fulani na tukaamini kuwa ameshamsajili.
      Huyo Lowasa kama anataka kutumia Club ya mpira kama daraja la kuingia Ikulu aende kule Msimbazi akaanze na issue ya Uwanja ambao Rage kila siku anawadanganyia,huku Jangwani hataamini kitakachotokea.

    13. #11
      Ndumbayeye's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2009
      Posts : 1,065
      Rep Power : 738
      Likes Received
      98
      Likes Given
      806

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      kama anaona dar young african itamlipa akiwekeza kuna tatizo gani hata kama ni simba... acheni mambo ya kizamani.
      I HAVE SPOKEN

    14. #12
      Yaya Toure's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th August 2012
      Posts : 1,214
      Rep Power : 651
      Likes Received
      266
      Likes Given
      117

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Huyu mzee ana damu ya kunguni kweli khaaaa...
      Ni hatari sana kwa afya yako kushabikia siasa za Tanzania....

    15. #13
      Ubungo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 1,151
      Rep Power : 589
      Likes Received
      204
      Likes Given
      185

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Yanga hainunuliki, washashindwa wengi labda na hawa wajaribu bahati yao. Akina Virani, Gulamali, Murtaza Dewji, Mengi nk

    16. #14
      Bujibuji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2009
      Location : NYUMBANI PANONO
      Posts : 13,819
      Rep Power : 11188
      Likes Received
      7012
      Likes Given
      5183

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Simba na Yanga zitakufa soon na itabaki Azam peke hake. Huoni Azam wame adopt rangi za Chadema?
      The Magnificent likes this.

    17. #15
      LUCIFER's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th August 2012
      Posts : 100
      Rep Power : 361
      Likes Received
      32
      Likes Given
      41

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Quote By Anselm
      Wish I were one of the Mod,ningeweka button ya "USHUZI" habari kama hii(ya mleta thread) inafanania na ile kitu inayotoka mtu anapopumua kwa ile njia nyingine ile.
      Wewe kweli Lucifer unafikiria sisi Wanachama wa Yanga ni Mapoyoyo kama nyinyi,sisi hatuwezi kushangilia picha ya Mwenyekiti wetu amemshika bega Mchezaji fulani na tukaamini kuwa ameshamsajili.
      Huyo Lowasa kama anataka kutumia Club ya mpira kama daraja la kuingia Ikulu aende kule Msimbazi akaanze na issue ya Uwanja ambao Rage kila siku anawadanganyia,huku Jangwani hataamini kitakachotokea.

      kwa kutumia udhaifu wa wanachama na wapenzi wa Yanga kutotaka kujua kinachoendelea katika klabu yao, isipokuwa waifunge Simba tu ama kuchukua ubingwa,ndiyo sababu ambayo wenye fedha wameeleza kuwa ndiyo njia rahisi ya kumpachika Lowassa awe mmoja wa wadhamini wa klabu ya Yanga .....Huyu bwana hapa ni USHAHIDI TOSHA......AU NI IBRAHIM AKILIMALI NINI?

    18. #16
      Ulimakafu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2011
      Location : Itabanya Balasi
      Posts : 10,936
      Rep Power : 2601
      Likes Received
      690
      Likes Given
      1615

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Bado gonjwa.
      LUCIFER likes this.

    19. #17
      yahoo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2011
      Location : Tanzania
      Posts : 626
      Rep Power : 393
      Likes Received
      107
      Likes Given
      23

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      ninavofaham mimi huyu jamaa simba damu,labda kama amegundua kama yanga inamvuto zaidi

    20. #18
      Makoye Matale's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2011
      Location : Uwandani, Kondeni
      Posts : 1,154
      Rep Power : 638
      Likes Received
      234
      Likes Given
      43

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Mwandishi wa uzi huu ameishiwa sera.

      Kwani lazima kila mtu aanzishe uzi wake? Kama huna point si afadhali uwe unasoma tu nyuzi za Great Thinkers' badala ya wewe kuweka hisia binafsi na za kinazi kama hizi? Hivi umelenga kuisambaratisha Yanga kwa maneno yako haya ya kipuuzi? Nakuhakikishia, UMENOA! Kajipange upya kama yule jamaa asiye kuwa na TemboCard Master Card katika tangazo la CRDB.

      Yanga Imara, Daima Mbele, Nyuma Mwiko. Die to hell all who hate Young Africans Sports Club.
      'Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa' Hos. 4:6

    21. #19
      dri ma's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th August 2012
      Posts : 103
      Rep Power : 362
      Likes Received
      8
      Likes Given
      1

      Default

      Quote By LUCIFER
      na wanachama wake wataongoza kwa Umaskini katika ukanda wa Africa Mashariki na Kati.
      kwli mbaaz ikikosa maua hucngizia jua kwan w nan kakwmbia wanachama wa yanga 2nataka utajir c 2nataka raha bwna

    22. #20
      LUCIFER's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th August 2012
      Posts : 100
      Rep Power : 361
      Likes Received
      32
      Likes Given
      41

      Default Re: Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

      Quote By dri ma
      kwli mbaaz ikikosa maua hucngizia jua kwan w nan kakwmbia wanachama wa yanga 2nataka utajir c 2nataka raha bwna
      aliyekwambia maskini ana raha nani?

    Page 1 of 2 12 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...