Kwa mara ya tatu kwa macho yangu nashuhudia penati za hatari, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2004 robo fainali ya EURO kati ya URENO na ENGLAND sikosei alikuwa SIMAO SAMBROSA alifunga penati ya hatari ya pili alifunga ROBEN VAN PERSIE RVP mwaka huu
nahisi ilikuwa mechi na WOLVES na ya tatu nimeiona jana ANDREA PIRLO "FUNDI" akifunga penati nyingine ya hatari dhidi ya ENGLAND hebu nikumbushe na wewe uliziona penati ngapi kama zile? 2 minutes
Ile ya Pirlo jana usiku ilikuwa noma. Yule mzee balaaa. Nyingine mbaya ilikuwa 1994 fainali kati ya Brazil na Italy- Roberto bagio alikosa penati muhimu mno
Ile ya Pirlo jana usiku ilikuwa noma. Yule mzee balaaa. Nyingine mbaya ilikuwa 1994 fainali kati ya Brazil na Italy- Roberto bagio alikosa penati muhimu mno
ile penalti ya jana ya pirlo mara ya mwisho ilipigwa 1976 nadhani na jamaa mmoja anaitwa antonini pananka...ni kama ile ya jana ila pirlo jana aliiboresha zaidi na sasa imebatizwa jina la ''falling leaf''.... mpira ulivyokuwa inaenda wavuni ni mithili ya
jani linavyodondoka toka kweny mti..(jinsi mpira ulivyokuwa unazunguka)....jamaa ni noma
hahahah.....mbele ya maestro kama pirlo hawezi fanya lolote ..labda angekuwa ameangalia movie moja inaitwa "Pinto detuvo a Pirlo un penalti a lo Panenka'' ....sasa wao wachezaji wa wingereza waligawiwa dvd za namna ya kumfunga buffon lakini ndo hivyo....
Kwa mara ya tatu kwa macho yangu nashuhudia penati za hatari, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2004 robo fainali ya EURO kati ya URENO na ENGLAND sikosei alikuwa SIMAO SAMBROSA alifunga penati ya hatari ya pili alifunga ROBEN VAN PERSIE RVP mwaka huu nahisi ilikuwa mechi na WOLVES na ya tatu nimeiona jana ANDREA PIRLO "FUNDI" akifunga penati nyingine ya hatari dhidi ya ENGLAND hebu nikumbushe na wewe uliziona penati ngapi kama zile? 2 minutes
yule alikuwa helder postiga arifu....alipiga penalty almaarufu panenka style dadadadadeki,.......decco alishangilia balaaa..wakati scolalri alidata maana ilikuwa penati za mwisho mwisho....
...kuwa na baba maskini ni mipango ya Mungu ila kuwa na baba mkwe maskini ni ujinga wako mwenyewe.....
ile penalti ya jana ya pirlo mara ya mwisho ilipigwa 1976 nadhani na jamaa mmoja anaitwa antonini pananka...ni kama ile ya jana ila pirlo jana aliiboresha zaidi na sasa imebatizwa jina la ''falling leaf''.... mpira ulivyokuwa inaenda wavuni ni mithili ya
jani linavyodondoka toka kweny mti..(jinsi mpira ulivyokuwa unazunguka)....jamaa ni noma
Anaitwa Antonin Panenka- ilikuwa fainali ya Euro 1976 kati ya Czech Republic na Ujerumani Magharibi. Ila kuna beki mjerumani anaitwa Andreas Brehme. Alinipigia penalti kali mno tarehe 8 Julai 1990 katika Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina katika uwanja wa Stadio Olimpico, Roma. Mechi ikielekea dakika ya 85, refa Mmexico akatoa penati ya kutatanisha ambapo Rudi Voller alionekana kufanyiwa faulo na Roberto Sensini. Kapteni Rothar Mathaus akamwita Brehme na kubusu mguu wake wa kulia na kumwambia 'Mguu huu, leo upeleke heshima Ujerumani'. Brehme akafunga penalti hiyo kwa ustadi mkubwa na kutoroka na Kombe ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu toka UEFA kushinda Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya timu isiyo ya Ulaya
penati kali kuliko zote duniani nilipiga mimi nikamfunga marehemu baba yangu!katoka zake kazini na suti yake katukuta tunapigiana penati kwa mpira wa chandimu eti akakaa golini adake penati yangu
nikaenda kupiga penati huku nazunguka ile style ya kupata kizunguzungu nilipoufikia mpira nikapiga DOCHI nikampiga tobo mdingi!eti mdingi mpira ushazama nyavuni akaruka upande wa kulia!watu walicheka sana!tatizo hatukurekodi video ningewawekea you tube!
Follow Us Here