Boban wa pili kushoto.
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ jana alikuwa kivutio kwa mashabiki, wasindikizaji na hata baadhi ya wasafiri waliomuona wakati wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuelekea Sudan. Uvaaji wa Boban, ndio uliowavutia watu kumtizama, kutokana na kuvaa kama mtu asiyesafiri.
Boban alikuwa amevaa fulana, suruali ya kimichezo ‘trakisuti’ na kandambili, hivyo kusababisha watu kuvutika kumuangalia, huku baadhi yao wakibaki kujiuliza kuhusu vituko vya nyota huyo ambaye mashabiki humuita Balotteli wa Bongo.


Bajeti ya maskini tajiri haiwezi 
Reply With Quote



" 
Follow Us Here