Habari zenu wana jamii forums na wapenzi wa jukwaa hili la Michezo. Kwa wale tunaofuatilia ligi kuu ya uingereza,kumekuwa na matukio mawili yanayohusishwa na ubaguzi wa rangi,yakiwakabili JT(John Terry) na LS(Luis Suarez).Baada ya LS kutuhumiwa kumtolea maneno ya kibaguzi Patrice Evra,alipatikana na hatia na kuadhibiwa kwa kukosa mechi nane.Kinachoshangaza ni kwamba kesi ya JT dhidi ya Antony Ferdinand hata haikusikilizwa,na FA wakatoa tamko kwamba kesi hiyo itasikilizwa baada ya ligi kumalizika mwezi wa 6.Nikajiuliza kwa nini kesi ya LS nayo wasingesema itasikilizwa mwezi wa 6?. Chelsea wakakutana na timu ya QPR kwa mara nyingine katika kombe la FA,wachezaji wa QPR wakapanga kutokumshika JT mkono.FA waliamua kuondoa utaratibu wa kupeana mikono katika mechi ile,kumnusuru JT.Wikiendi hii tutashuhudia mechi ya mzunguko wa pili ya ligi kati ya Chelsea na QPR na FA wameshatangaza tena kwamba hakutakuwa na ule utaratibu wa kushikana mikono kabla ya mechi.Najiuliza mbona Man U na Liverpool walipokutana tena FA hawakuondoa huu utaratibu wa kushikana mikono kabla ya mechi ile?Je hii ni kwa sababu LS si mwingereza? Kwa nini kesi ya John Terry(mwingereza) dhidi ya Anthony Ferdinand(Mwingereza) isikilizwe baada ya ligi kuisha wakati kesi ya Luis Suarez(Uruguay) dhidi ya Patrice Evra(Ufaransa) isikilizwe wakati ule ule?kwa nini huku waruhusu utaratibu wa kushikana mikono huku wazuie tena mara zote mbili? Je hii haidhihirishi kwamba FA wamezichukulia kesi hizi tofauti kwa sababu ya racism?yaani FA pia ni wabaguzi au ndio mcheza kwao hutuzwa? Karibuni tujadili ila tuweke usabiki wa timu pembeni!

Reply With Quote


Follow Us Here