Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Yanga Africans, Special Thread

    Report Post
    Page 68 of 78 FirstFirst ... 586667686970 ... LastLast
    Results 1,341 to 1,360 of 1551
    1. #1
      Gang Chomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th February 2008
      Location : hell
      Posts : 5,256
      Rep Power : 1771
      Likes Received
      1041
      Likes Given
      0

      Default Yanga Africans, Special Thread

      yanga ilianzishwa mnamo mwaka 1935 na inasemekana ndo klabu kongwe na yenye mafanikio zaidi hapa nchini. klabu hii ilianzishwa na wazalendo halisi wa nchi hii waliokuwa wakiji shughulisha na uchuuzi wa nazi na samaki na muda wao wa jioni ulipofika walikuwa wakijumuika pamoja kusakata kabumbu na hapo ndipo ilizaliwa yanga.

      kama hiyo haitoshi wazalendo hawa waliendelea kujikusanya kwa pamoja na kuanza mishemishe za kusaka uhuru wa nchi hii, na ndipo tarehe 9 disemba mwaka 1961 tanganyika ikapata uhuru, hivyo kama tutazungumzia uhuru wa taifa hili basi hatusiti kwa namna moja au nyingine kuitaja yanga, na kwa heshima yake inatakiwa unapoitaja yanga kama umekaa basi unatakiwa usimame.
      MAFANIKIO.
      yanga ndio timu iliyochukua ubingwa wa ligi ya bara mara nyingi zaidi, na ndio klabu inayofahamika zaidi kitaifa na kimataifa kwa sababu ndiyo klabu iliyopeperusha vizuri bendela ya taifa hili la tanzania nje ya mipaka.
      na kama hiyo haitoshi yanga ndiyo klabu yenye washabiki wengi zaidi ndani na nje ya nchi, ndani ya africa na dunia kwa ujumla.

      na pia yanga ndiyo klabu ya mwanzo hapa nchini au hata afrika mashariki kwa ujumla kwa kuwa na makao makuu sambamba na uwanja wa mazoezi ambao unajulikana kwa jina la Kaunda, jina la muasisi na mpigania uhuru mwengine wa taifa la zambia muheshimiwa keneth kaunda.
      mfumo huu wa kuwa na makao makuu pamoja na uwanja wa mazoezi ni wa timu kubwa barani ulaya na dunia kwa ujumla.

      yanga pia ndio timu ya kwanza kuwa na gazeti hapa nchini. gazeti hili linajulikana kama "Yanga imara". lilipotoka katika wiki ya kwanza liliuzwa takriban nakala 50,000 nchi nzima na baadhi ya nchi za jirani.
      mfumo wa kuwa na gazeti la klabu pia umeigwa na baadhi ya klabu hapa nchini lakini unaonekana kusua sua katika mauzo na hata ukisoma nakala ya gazeti lao utakuta limejaa matangazo ya waganga tu.

      yanga ndo timu pekee iliyowahi kuuza mchezaji nje ya nchi na kung'aa katika vilabu mbali mbali barani ulaya, mchezaji huyu alijulikana kama Nonda Shaaban al maarufu kama "papii".
      nonda ambaye aliwahi kutamba na mashujaa hawa wa jangwani amepata kuchezea vilabu kama val profesional ya south africa, FC zuurich ya uswis, stade rennes na AS monaco zote za ufaransa, AS roma ya italia akicheza pamoja na francesco totti, blackburn ya uingereza na sasa anakipiga katika klabu ya galatasaray yenye maskani yake katika uwanja wa ali sami yen nchini uturuki.

      na hapa ndipo tunapoitofautisha yanga na vilabu vingine vya soka hapa nchini ambavyo wachezaji wake huuzwa burundi, rwanda na uarabuni ambako hakuna soka la ushindani.

      pia yanga ndo timu ya kwanza hapa nchini kuongozwa na rais.
      pia yanga ndo timu ya kwanza kuwa na mfumo wa wanachama kuwa wana hisa wa klabu kama timu nyingi za ulaya, hivyo kumfanya kila mwanachama kuhusika kikamilifu katika mipango na malengo ya klabu, tofauti na majirani zetu ambao mfumo wao wa uongozi haueleweki na hata mishahara ya wachezaji wanalipwa kimkanda mkanda na inafika kipindi mchezaji anakaa miezi minne hajalipwa mshahara mwisho wanatimkia kucheza ligi za mchangani.

      MAFANIKIO NJE YA MIPAKA.
      Yanga kama yanga ndo timu pekee iliyowahi kuchukua kombe linalotambuliwa na shirikisho la soka barani afrika CAF na shirikisho la soka duniani FIFA. itakumbukwa tu yanga waliwafunga express ya uganda kwa goli 3-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la klabu bingwa afrika mashariki na kati na mechi ya fainali walitakiwa wakipige na SC villa.

      yanga waliwacharaza bila huruma SC Villa goli 2-1 katika uwanja wa nakivubo kwenye mechi ya fainali ya kombe lililokuwa na msisimko kipindi hicho la klabu bingwa afrika mashariki na kati na kupelekea serikali ya tanzania kutuma ndege mpaka katika uwanja wa ndege wa entebe kwenda kuwachukua waheshimiwa waliolitoa taifa kimasomaso yaani yanga.
      hivyo kuweka adabu kwa waganda ambao hawawezi kuisahau yanga maishani mwao.

      yanga katika mechi hiyo iliwakilishwa na:
      1) steven nemes
      2) mwanamtwa kihwelu
      3) keneth mkapa
      4) willy mtendamema
      5) issa athuman
      6) method mogella
      7) steven mussa
      8) hamis thobias gagarino
      9) said mwamba kizota
      10) mohamed husein chinga one
      11) edibily jonas lunyamila


      pia yanga walikuwa na bunduki nje kwenye benchi kama willy martin, rifat said, aboubakar salum "sure boy" david mwakalebela "MP" na wengine wengi ambao walikuwa ni miiba kwa waganda.

      katika mechi hiyo mnamo dakika ya 81 beki mahili wa villa na timu ya taifa ya uganda marehemu Paul Hasule alivua jezi na kutoka nje kwa kile ambacho mwenyewe alikiri kuwa ameshindwa kumkaba winga wa yanga edibily lunyamila, lakini alilazimishwa na kocha wake kumaliza mechi kutokana na aibu iliyokuwa inawakabili.

      kutokea hapo waganda walitekwa akili kutokana na kabumbu safi lililoonyeshwa na yanga na kupelekea daladala nyingi nchini humo kuandikwa majina kama "lunyamila trans" "kizota trans" au hata wengine walifuta majina ya salon zao na kuandika "gagarino hair salon" na mpaka leo hii waganda wakisikia timu kutoka tanzania inakwenda huko wanauliza "je ni yanga?".

      na baada ya ushindi huo mwanamuziki nguli wa afrika marehemu kabasele yampanya al maarufu kama peppe kalle alitunga wimbo wa kuisifia timu hiyo baada ya kuonyesha dhahili kiwango cha juu na kuvutia washabiki wengi wa soka kitu ambacho hakijawahi kufanywa na klabu yoyote nyingine hapa nchini.

      HISTORIA ISIYO SAHAULIKA.
      mwaka 1972 katika pambano la watani wa jadi lililokuwa lifanyike katika uwanja wa taifa, watanzania walishuhudia kituko cha mwaka pale kilabu ya simba ya dar es salaam ilipoishia chang'ombe na kugeuza basi na kurudi katika mtaa wa msimbazi na kufanya timu ya yanga ya tanzania kupewa ushindi baada ya mpinzani kufyata mkia na kutokomea vichakani.

      mnamo pia tarehe 13 mwezi novemba mwaka 1991 katika uwanja huo huo wa taifa timu ya yanga ya tanzania waliingia uwanjani na basi la sharuksi lililokuwa likimilikiwa na mfadhili wa yanga wa kipindi hicho marehemu abbas gulamali, timu ya soka ya simba ya dar es salaam iliweka mpira kwapani wakati wa mapumziko na kutokomea kusiko julikana.

      na kauli hii ya kuweka mpira kwapani iltolewa na mtangazaji aliyekuwa anatangaza soka redio tanzania siku hiyo ndugu Charles Hillary, na magazeti kama motomoto, mfanyakazi, uhuru na mzalendo ya kipindi hicho yalipambwa na kichwa kikubwa cha habari "mgonjwa atema dawa".

      na kuweka mpira huko kwapani kulifuatia vipigo mfululizo vya august 31, october 9 lakini hii iltanguliwa na kipigo cha Said Sued "Scud" cha mei 18.

      baadhi ya mashujaa waliowahi kukipiga yanga miongoni mwao ni rifat said, joseph katuba, peter manyika, anwar awadh, salum kabunda "ninja", godwin aswile "baba subi" au scania, said zimbwe, thomas kipese, joseph lazaro, omar husein, costantino kimanda, sanifu lazaro "tingisha" na wengine wengi.

      hili nililokupa hapo ni tone tu la maji, ila bahari ntakupa siku nyingine.
      na hii ndo yanga, klabu bora kabisa hapa nchini, isiyotishwa na kelele, adhabu wala faini yoyote.
      Last edited by Gang Chomba; 10th April 2011 at 01:42.


    2. #1341
      Mpeni sifa Yesu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd May 2010
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 472
      Rep Power : 555
      Likes Received
      18
      Likes Given
      1

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      kuna kipindi hadi kwenye tiketi za kuingilia kati ya simba na yanga, zilishawahi kuandikwa maandishi ya kuran, hadi watu walilalamika sana...hata hivyo, sisi tusio waislam huwa tunawavumilia kwa hilo, lakini laiti kama wakristo ndo wangefanya hivyo, ungesikia kelele na manung'uniko ya ajabu...nafikiri ni bora tuchague kuishi kwa kuvumiliana tu ili tz yetu iwe ya amani.
      Hakuna lisilowezekana kwa Mungu, anaponya, anaokoa. kwa ushauri na maombi, tuwasiliane ([email protected]). karibu kwa Yesu.

    3. #1342
      Wingu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2011
      Posts : 4,063
      Rep Power : 1239
      Likes Received
      257
      Likes Given
      41

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      Mkuu utaita askofu wakati waliopo wote wamevaa kanzu na karabaghashee.Akili ya kawaida ni kwamba jumuia inayoizunguka asilimia kubwa ni waislamu.Hata simba wanafanyaga hivyo hivyo na sio yanga tu
      mtu chake likes this.

    4. #1343
      Malipo kwamungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2012
      Posts : 291
      Rep Power : 425
      Likes Received
      44
      Likes Given
      72

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      Nafikiri waislam wanapalilia udini kuliko kitu kingine kila mahali lakini "YOUNG AFRICAN SPORTS CLUB" haina udini mimi niliwahi kuichezea timu hiyo
      Kwanini wenzetu waumini wakiislam wanaokuwa na nafasi sana kwenye shughuli za klabu? Wengi wao wanakuwa na shughuli binafsi si waajiliwa hivyo wanapatikana
      Pili wenzetu ushirikina ni sehemu ya maisha yao na dini yao
      tatu :Yanga ndipo harakati za kupigania uhuru zilikuwa zinafanyika kwa wakazi wa mzizima yote sasa [DARESALAAM]
      Mwl JK alikuwa anafika sana kwenda mtaa wa mafia hata bao alikuwa ana chezea pale mtaa wa Kongo chini ya mti mkubwa sijui kama bado upo ule mti
      Last edited by Malipo kwamungu; 27th July 2012 at 11:56.

    5. #1344
      Henge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 5,440
      Rep Power : 1678
      Likes Received
      920
      Likes Given
      1673

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      Kwani haujui kuwa yanga ni tasisi ya chama cha mapinduzi,
      naipenda yanga but ninapokumbuka ilikuwa tasisi ya ccm najihisi kuichukia!
      TUKIWAKAMATA MAFISADI NCHI ITAYUMBA by PINDA

    6. #1345
      ndomyana's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 2,080
      Rep Power : 0
      Likes Received
      211
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Henge View Post
      Kwani haujui kuwa yanga ni tasisi ya chama cha mapinduzi,
      naipenda yanga but ninapokumbuka ilikuwa tasisi ya ccm najihisi kuichukia!
      ccm ndo yanga make ilianza yanga mwaka1936 ikaja ccm 1977,. Acha kupotosha umma


    7. #1346
      mtu chake's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th August 2010
      Location : Kivu
      Posts : 2,173
      Rep Power : 1768
      Likes Received
      1021
      Likes Given
      1341

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      ...kwa kwaida waislamu huwa wana tabia ya kuombea marehemu na hizi club iwe Yanga au simba wanao utaratibu huo...

      katika uchaguzi wa yanga wagombea wakristo walikuwpo..na hata aliyeshinda nafasi ya makamu mwenyekiti ni mkristo anaitwa Frank Sanga...sawa mtoa mada@TELO..pia kulikuwa na mtu anaitwa Yono Steven Kavela...alikuwepo mwamli Joseph Chibura...sasa cjui ulikua unamaanisha nini ulipoleta mada hii@TELO...na wengine

      Kuhusu zile Tiketi ilikua mechi kati ya Simba na Yanga..kumbuka mechi yanga ilikua mwenyeji na ilikua ndio mechi ya kwanza kuchezwa uwanja mpya wa Taifa katika Kuzidhiti Mapato hasa Tiketi feki waliamua kuweka muhuri wenye maandishi ya Kiislamu Mpeni sifa Yesu...
      @@

    8. #1347
      JATELO1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2011
      Posts : 1,019
      Rep Power : 905
      Likes Received
      81
      Likes Given
      41

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      Quote By mtu chake View Post
      ...kwa kwaida waislamu huwa wana tabia ya kuombea marehemu na hizi club iwe Yanga au simba wanao utaratibu huo...

      katika uchaguzi wa yanga wagombea wakristo walikuwpo..na hata aliyeshinda nafasi ya makamu mwenyekiti ni mkristo anaitwa Frank Sanga...sawa mtoa mada@TELO..pia kulikuwa na mtu anaitwa Yono Steven Kavela...alikuwepo mwamli Joseph Chibura...sasa cjui ulikua unamaanisha nini ulipoleta mada hii@TELO...na wengine

      Kuhusu zile Tiketi ilikua mechi kati ya Simba na Yanga..kumbuka mechi yanga ilikua mwenyeji na ilikua ndio mechi ya kwanza kuchezwa uwanja mpya wa Taifa katika Kuzidhiti Mapato hasa Tiketi feki waliamua kuweka muhuri wenye maandishi ya Kiislamu Mpeni sifa Yesu...
      Hapo pekundu rudia kusoma mada yangu. Nauliza tu ni kwanini shughuli za Yanga F.C hasa kama uchaguzi wa viongozi unaohusisha wanachama wote itanguliwe na sala ya Kiislamu wakati kuna wana siyo wa Imani ya Kiislamu? Je YANGA F.C ni Taasisi ya Kidini ya Kiislamu? hapo ndiyo hoja yangu. Naamini sasa utakuwa umenielewa ukiunganisha na huo mfano wa wagombea uliotoa hapo kwenye post yako.

    9. #1348
      mtu chake's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th August 2010
      Location : Kivu
      Posts : 2,173
      Rep Power : 1768
      Likes Received
      1021
      Likes Given
      1341

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      ...hahahahahahahaha...naona umeamkia Yanga leo ..umegusia uchaguzi na kuanza kwa sala wakati ulisema hata wagombea wa yanga ni waislamu..sawa sawa..ulishawahi kuhudhuria uchaguzi wa simba?...mwaka juzi...uliyoongozwa na bwn Dalali...

      nimekusoma..nami nimemaliza
      @@

    10. #1349
      PAKA MAPEPE's Avatar
      Member Array
      Join Date : 20th July 2012
      Posts : 19
      Rep Power : 351
      Likes Received
      0
      Likes Given
      1

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      Mkuu sielewi Yanga ndio nini???

    11. #1350
      Opaque's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th October 2008
      Posts : 955
      Rep Power : 734
      Likes Received
      227
      Likes Given
      84

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      Quote By mtu chake View Post
      .... Tiketi feki waliamua kuweka muhuri wenye maandishi ya Kiislamu Mpeni sifa Yesu...
      Hapa duniani kuna maandishi ya kiisilamu? Au kiarabu ndio kiisilamu?



    12. #1351
      Anselm's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2010
      Location : Dar-es-salaam
      Posts : 1,476
      Rep Power : 731
      Likes Received
      183
      Likes Given
      138

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      Quote By PAKA MAPEPE View Post
      Mkuu sielewi Yanga ndio nini???
      Nimerudi sasa....UTAELEWA TU VUTA SUBIRA

    13. #1352
      Anselm's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2010
      Location : Dar-es-salaam
      Posts : 1,476
      Rep Power : 731
      Likes Received
      183
      Likes Given
      138

      Default Re: wapiga penalti wa yanga kama chelsea

      Quote By paty View Post
      ile penalt ya kiiza kama pirlo vileeeeeeeeeeeeee
      Ile penalt ya Kiiza ni noumarr

    14. #1353
      Henge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 5,440
      Rep Power : 1678
      Likes Received
      920
      Likes Given
      1673

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      Quote By Ukweli mtupu View Post
      ccm ndo yanga make ilianza yanga mwaka1936 ikaja ccm 1977,. Acha kupotosha umma
      unajua jezi za yanga miaka hiyo zilikuaje na mwaka gani zilibadilishwa kuwa za kijani kama ccm??
      mtu chake likes this.
      TUKIWAKAMATA MAFISADI NCHI ITAYUMBA by PINDA

    15. #1354
      mtu chake's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th August 2010
      Location : Kivu
      Posts : 2,173
      Rep Power : 1768
      Likes Received
      1021
      Likes Given
      1341

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      Quote By Opaque View Post
      Hapa duniani kuna maandishi ya kiisilamu? Au kiarabu ndio kiisilamu?
      ..hahahahahaha...ndio umekuja kusahihisha?...haya tupe maoni yako juu ya mada..kama huwezi baki jikoni upike wanaume tuko sebuleni tuna maongezi...
      @@

    16. #1355
      chief-mkwawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2011
      Posts : 3,529
      Rep Power : 1662
      Likes Received
      1045
      Likes Given
      0

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      nchi imejaa siasa na udini hadi kwenye michezo? This is too much guys mod bora muhamishe hii topic

    17. #1356
      zaratustra's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 635
      Rep Power : 634
      Likes Received
      85
      Likes Given
      116

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      Quote By paka mapepe View Post
      mkuu sielewi yanga ndio nini???
      paka mapepe!

    18. #1357
      paty's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th October 2010
      Location : never never land
      Posts : 1,041
      Rep Power : 982
      Likes Received
      273
      Likes Given
      66

      Default Re: wapiga penalti wa yanga kama chelsea

      Quote By Anselm View Post
      Ile penalt ya Kiiza ni noumarr
      ngoja tuwacheki hawa jamaa kkama leo watachomoka kwa azam, maana wana mdomo sana
      CHADEMA mwendo mdundo - T 2015 CDM

    19. #1358
      ndomyana's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 2,080
      Rep Power : 0
      Likes Received
      211
      Likes Given
      0

      Default Re: Yanga Africans, Special Thread

      Simba ndo mmeishiwa hela za kununua penat

    20. #1359
      Mandown's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th April 2012
      Location : japan
      Posts : 682
      Rep Power : 499
      Likes Received
      113
      Likes Given
      52

      Default Re: Yanga sports club ni taasisi ya kiislamu hapa tanzania?

      amakweli, maendeleo hatuwezi kuyapata kwasababu tunafikiria kwa MAKALIO

    21. #1360
      Kankwale's Avatar
      Member Array
      Join Date : 5th April 2012
      Posts : 83
      Rep Power : 379
      Likes Received
      13
      Likes Given
      8

      Default Yanga vs azam

      fainali ya kagame ni yanga na Azam.

    Page 68 of 78 FirstFirst ... 586667686970 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Yanga special thread
      By Pdidy in forum Sports
      Replies: 2
      Last Post: 23rd October 2012, 13:14
    2. Website ya Dar Young Africans-Yanga
      By Balantanda in forum Sports
      Replies: 60
      Last Post: 9th August 2012, 18:16
    3. Special Thread: Did You Know??
      By Qadhi in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 2
      Last Post: 6th January 2011, 16:31
    4. Replies: 2
      Last Post: 27th July 2010, 15:24

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...