Taifa Stars, Msumbiji waingiza Sh605milioni - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Sports & Entertainment Forum


Sports & Entertainment Forum Talk about Music, Sports, TV Shows, Movies, Entertainment & Much More


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 12th September 2007, 08:20 PM   #1
Taifa Stars, Msumbiji waingiza Sh605milioni
Bubu Ataka Kusema Bubu Ataka Kusema is offline 12th September 2007, 08:20 PM

Taifa Stars, Msumbiji waingiza Sh605milioni
Na Phillip Nkini
Kutoka Gazeti la Mwananchi

BAADA ya kusita kwa siku tatu kutangaza mapato ya mechi ya kufuzu ya fainali ya Mataifa ya Afrika baina ya Taifa Stars na Msumbiji, jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilitangaza kuwa Sh605milioni zilipatikana katika mechi hiyo iliyofanyika katika uwanja mpya wa kisasa jijini Dar es Salaam.

Stars ilipata kipigo cha 1-0 kutoka kwa Msumbiji katika mechi hiyo iliyochezwa Jumamosi jambo ambalo lilifanya timu zote mbili kushindwa kufuzu kwenda Ghana mwakani katika fainali za Mataifa ya Afrika ambazo zitafanyika Januari 20 hadi Februari 10.

Senegal, ndiyo imefuzu kutoka katika Kundi la Saba baada ya kuifunga Burkina Faso mabao 5-1.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Fedha wa TFF, Silas Mwakibinga alisema watazamaji 55,514 walijitokeza kuona mechi hiyo katika uwanja mpya wenye uwezo wa kubeba mashabiki 57,129.

Mwakibinga alisema Sh 605, 020,000 zilipatikana ambazo ni sawa na asilimia 94 ya uwezo wa uwanja huo katika kiingilio cha siku hiyo.

''Si kweli kuwa uwanja mpya unaingiza watu 60,000 kwani viti vilivyopo uwanjani ni 57,129 kwa hiyo idadi hiyo ndio ya tiketi zilizotengenezwa,'' alisema mkurugenzi huyo.

Alisema watazamaji 743 walikata tiketi za Sh 50,000 katika Jukwaa la VIP (A), 1,973 walikata tiketi za Sh 40,000 katika Jukwa la VIP (B) na wengine 2,242 walikata tiketi za Sh 30,000 za VIP (C).

Alisema jukwaa lenye rangi ya machungwa (orange straight) linalotazamana na VIP, waliingia watu 5,326 kwa kiingilio cha Sh 20,000 huku jukwaa kama hilo nyuma ya magoli wakiingia watu 7,300 kwa kiingilio cha Sh 10,000.

Alisema viti vya bluu mzunguko waliingia watazamaji 18,340 kwa kiingilio cha Sh 10,000 na jukwaa la kijani waliingia watu 19,590 kwa kiingilio cha Sh 3,000.

Mkurugenzi huyo alisema tiketi nyingine zote zilimazika isipokuwa za Sh 20,000 ambazo kama zingemalizika zote jumla zingepatikana Sh 644,530,000.

''Si kweli kwamba tiketi zote zilimalizika kwani tiketi za 20,000 hazikwisha," alifafanua.

Alisema mapato haya yalichelewa kutangazwa kutokana na kamati kukamilisha taratibu zake zote na walitaka kutangaza kitu cha uhakika zaidi.

Mwakibinga alisema udhibiti wa watu walioingia uwanjani ulikuwa wa kuridhisha na hakukuwa na matatizo.

Tangu kuchezwa kwa mechi hiyo kumekuwa na manung'uniko na uvumi kutoka kwa wadau wa soka ambao hawakuridhishwa na mapato ya Sh milioni 234 yaliyopatikana katika mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Uganda iliyofanyika Jumamosi ya wiki iliyopita.
__________________
~*~Life is Good~*~

 
Bubu Ataka Kusema's Avatar
Bubu Ataka Kusema
JF Premium Member
Points: 12,662,314, Level: 100 Points: 12,662,314, Level: 100 Points: 12,662,314, Level: 100
Activity: 69% Activity: 69% Activity: 69%
Join Date: Sun Feb 2007
Location: Mfaranyaki
Posts: 12,663
Thanks: 1,027
Thanked 1,188 Times in 690 Posts
Views: 236
Reply With Quote
  #2  
Old 12th September 2007, 09:05 PM
Kuntakinte's Avatar
Kuntakinte Kuntakinte is offline
Kuntakinte Contextualizing
JF Senior Expert Member
Points: 222,144, Level: 100 Points: 222,144, Level: 100 Points: 222,144, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Sat May 2007
Location: Matombo, Morogoro
Posts: 790
Thanks: 6
Thanked 3 Times in 2 Posts
Rep Power: 24
Kuntakinte will become famous soon enoughKuntakinte will become famous soon enoughKuntakinte will become famous soon enoughKuntakinte will become famous soon enoughKuntakinte will become famous soon enoughKuntakinte will become famous soon enoughKuntakinte will become famous soon enoughKuntakinte will become famous soon enough
Default

Ina maana pesa nyingine imekwenda wapi au wengine walikuwa na Complimentary
__________________
"Mwisho wa ubaya Aibu"
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
msumbiji, sh605milioni, stars, taifa, waingiza


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Taifa Stars Bora Itolewe (ifungwe) Samvulachole Sports & Entertainment Forum 56 10th December 2009 09:30 PM
Taifa Stars waanza kugombea pesa! kanda2 Sports & Entertainment Forum 5 1st July 2007 10:19 AM
Bajeti Mbadala 2007/08 John Mnyika Business & Economic Forum 30 21st June 2007 10:08 PM
Breaking News: Taifa Stars ''matajiri'' Saidi Yakubu Sports & Entertainment Forum 85 21st June 2007 12:32 PM
No Jet for Taifa Stars to Ouagadougou? Kichuguu Sports & Entertainment Forum 6 17th June 2007 12:33 PM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 01:38 PM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com