Mtoto wa miaka 15, amzalisha mama kwa njia ya upasuaji. - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Sports & Entertainment Forum


Sports & Entertainment Forum Talk about Music, Sports, TV Shows, Movies, Entertainment & Much More


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 4th July 2007, 08:55 AM   #1
Mtoto wa miaka 15, amzalisha mama kwa njia ya upasuaji.
Kuntakinte Kuntakinte is offline 4th July 2007, 08:55 AM

Mwandishi Wetu

HabariLeo; Wednesday,July 04, 2007 @00:01


Si jambo la kawaida kusikia mtoto mwenye umri wa miaka 15 duniani kufanya jambo kubwa linalowashangaza watu wengi kwa kuwa umri kama huo kwa watoto wa Afrika hususani Tanzania huwa kidato cha kwanza na wengine huwa bado kumaliza hata shule ya msingi.

Lakini hivi karibuni kwenye mji wa Manaparai ulioko Kusini mwa Jimbo la Tamil Nadu, nchini India;mvulana Dhileepan Raj(15), mtoto wa madaktari wawili amefanikiwa kumzalisha mama mmoja mwenye umri wa miaka 20, kwa njia ya upasuaji katika hospitali inayomilikiwa na wazazi wake ya Mathi Surgical and Maternity Hospital kwenye Jimbo hilo.

Tukio hilo lilifanyika chini ya uangalizi wa wazazi wake ambao walikuwa wakirekodi tukio zima kwa njia ya video na kuwa kitendo hicho ni cha kustaajabisha na cha kwanza kutokea duniani kufanywa na mtoto mwenye umri kama huo.

Kutokea kwa tukio hilo nchini humo kumekuja baada ya baba wa mtoto huyo Dk. K. Murugesan kutaka siku moja mwanae aweke rekodi ya tukio la kitabibu ili jina lake liingizwe kwenye kitabu cha rekodi duniani kiitwacho Guinness Book of Records, tukio ambalo amelitimiza kwa kuweka rekodi ya jina lake kwenye kitabu hicho.

Rekodi kama hiyo ya upasuaji haijawahi kuwekwa wala kutokea duniani kwa mtu mwenye umri kama huo na kuwa bado tukio hilo linawashangaza wengi ambao wanajiuliza Dhileepan alipata ujuzi huo wapi na chuo gani kwa kuwa mtoto kama yeye kwa kawaida huwa hajamaliza masomo ya sekondari na kuhitimu chuo,ili aweze kupata uzoefu wa kufanya upasuaji kama huo.

“Dk.Murugesan mwezi uliopita alionyesha mkanda aliourekodi wakati mtoto wake akifanya upasuaji huo kwenye hospitali yao huko Munaparai nchini India,” anasema Dk. Venkatesh Prasad Katibu wa Chama cha Madaktari nchini India (IMA), na kuongeza kuwa kwenye mkanda huo , Dk. Murugesan anaonekana akimchoma ganzi mgonjwa huyo kabla ya mwanae kuanza kazi ya upasuaji.

“Tulipata mshtuko tulipoona tukio hilo lililokuwa likirekodiwa kwenye mkanda, anasema Dk. Prasad wakati akizungumza na vyombo vya habari, na kusema kuwa IMA wamemuambia Dk. Murugesan kuwa kitendo hicho ni kinyume na maadili na pia ni kitendo cha ukiukwaji wa sheria”.

Hata hivyo kuna madai kuwa Polisi nchini humo wamewakamata wazazi wa mtoto huyo ambaye anadaiwa kufanya upasuaji huo, kwa lengo la kutaka jina lake liingie kwenye kitabu cha rekodi cha dunia.

Habari kutoka vyanzo mbalimbali zinasema kukamatwa kwa Dk. Murugesan na mkewe kumekuja baada ya Chama cha Madaktari nchini humo kuonyesha mkanda wa video unaoonyesha Dhileepan Raj akifanya upasuaji huo , na kusema Afisa mmoja wa wilaya ya Tiruchirappalli kwenye mji wa Tamil Nadu, Ashish Vachani alitoa taarifa hizo za kukamatwa kwa shirika la habari la Associated Press (AP).

Hata hivyo Msemaji wa kitabu hicho cha rekodi za Dunia, Amarilis Espinoza, aliliambia Shirika hilo la habari kwa njia ya barua pepe kuwa kitabu hicho hakiwezi kuidhinisha na kuweka kwenye rekodi jina la mtoto huyo, kwa kuwa kufanya hivyo kutachochea ukiukwaji wa maadili na kuzorotesha huduma za kitabibu kwa kufanya vitendo vya mzaa kwa maisha ya watu.

Hata hivyo wachunguzi wa mambo wanasema kuwa Dk.Murugesan, anaweza kuwekewa pingamizi la kutotoa huduma hiyo na pia kufunguliwa mashitaka kwa kuruhusu mwanae kufanya upasuaji ambao kwa kitabibu hakuwa amepitia chuo cha udaktari , bali kwa mujibu wa baba yake alikuwa amemfundisha mwanae huyu kufanya kazi hiyo kwa muda wa miaka mitatu!.

Dk. Prasad anasema kitendo hicho kilichofanywa na Dk. Murugesan kwa kumruhusu mwanae kufanya jambo kama hilo sio kizuri kwa kuwa ni kinyume kabisa na maadili ya kitabibu, jambo ambalo baba wa Dhileepan anasema sio mara ya kwanza kwa mwanae huyo kufanya upasuaji na kuwa amekuwa akimfundisha mwanae huyo kwa muda wa miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo Dk. Murugesan alikiambia chama hicho kuwa nia yake ilikuwa ni kuona siku moja jina la mwanae (Dhileepan) liko kwenye kitabu cha rekodi duniani.

Habari za mtoto huyo kufanya upasuaji huo ambao ulifanyika mapema mwezi Mei mwaka huu, zilisambaa ambapo Katibu wa Afya wa Serikali, V.K Subbaraj alisema uchunguzi wa jambo hilo unafanywa ili kubaini tukio hilo na Dk. Murugesan kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa kitendo kilichofanywa ni cha ukiukwaji wa sheria.

Vyanzo mbalimbali vya habari vinasema kuwa lengo la familia hiyo ilikuwa ni kuona tu jina la mtoto wao linawekwa kwenye rekodi ya kitabu cha dunia, na kuwa baadhi ya madaktari wa serikali walio kwenye chama hicho cha IMA, ambao waliona mkanda huo wa video ukirekodi tukio hilo wamesema kitendo hicho ni kinyume na maadili ya taaluma yao.


Habari zaidi kuhusu kukamatwa kwa wazazi hao wa Dheileepan hazijapatikana, ili kujua nini kitatokea kwa madaktari hao, licha ya kuwa baadhi ya madaktari nchini humo wanasema huenda Dk.Murugesan akanyang’anywa leseni ya kufanyia kazi kwa kitendo chake cha kumruhusu mwanae asiye na leseni wala mafunzo yanayotambulika kutoka chuo cha utabibu kufanya upasuaji huo.



Makala hii imetayarishwa na Mwandishi Wetu kwa msaada wa intaneti.

 
Kuntakinte's Avatar
Kuntakinte
JF Senior Expert Member
Points: 222,144, Level: 100 Points: 222,144, Level: 100 Points: 222,144, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
Join Date: Sat May 2007
Location: Matombo, Morogoro
Posts: 790
Thanks: 6
Thanked 3 Times in 2 Posts
Views: 725
Reply With Quote
  #2  
Old 4th July 2007, 10:20 AM
Amossy Samson Itozya Amossy Samson Itozya is offline
Amossy Samson Itozya has no status.
Junior Member
Points: 88,223, Level: 100 Points: 88,223, Level: 100 Points: 88,223, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Tue Mar 2006
Posts: 2
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0
Amossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enough
Default

where are going now?
Reply With Quote
  #3  
Old 4th July 2007, 10:21 AM
Amossy Samson Itozya Amossy Samson Itozya is offline
Amossy Samson Itozya has no status.
Junior Member
Points: 88,223, Level: 100 Points: 88,223, Level: 100 Points: 88,223, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Tue Mar 2006
Posts: 2
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0
Amossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enoughAmossy Samson Itozya will become famous soon enough
Default

where are we going now?
Reply With Quote
  #4  
Old 4th July 2007, 01:10 PM
Masatu Masatu is offline
Masatu Is Magumashi
JF Senior Expert Member
Points: 733,039, Level: 100 Points: 733,039, Level: 100 Points: 733,039, Level: 100
Activity: 4% Activity: 4% Activity: 4%
 
Join Date: Mon Jan 2007
Location: Mbagala, Jeshini
Posts: 3,741
Thanks: 0
Thanked 88 Times in 66 Posts
Rep Power: 0
Masatu is infamous around these parts
Default

What this doc has done is unethical
Reply With Quote
  #5  
Old 4th July 2007, 06:11 PM
Chuma Chuma is offline
Chuma has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 290,413, Level: 100 Points: 290,413, Level: 100 Points: 290,413, Level: 100
Activity: 2% Activity: 2% Activity: 2%
 
Join Date: Mon Dec 2006
Posts: 1,283
Thanks: 15
Thanked 38 Times in 23 Posts
Rep Power: 26
Chuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enough
Default

doc has go no problem..unless u put forward all unethical issues..
Reply With Quote
  #6  
Old 4th July 2007, 07:04 PM
Chuma Chuma is offline
Chuma has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 290,413, Level: 100 Points: 290,413, Level: 100 Points: 290,413, Level: 100
Activity: 2% Activity: 2% Activity: 2%
 
Join Date: Mon Dec 2006
Posts: 1,283
Thanks: 15
Thanked 38 Times in 23 Posts
Rep Power: 26
Chuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enoughChuma will become famous soon enough
Default

sorry Masatu labda sikukupata..kuhusu Dr(Docta).. kweli unethical..na ikiruhusiwa namna hii..itakuwa hatari...
Reply With Quote
  #7  
Old 5th July 2007, 09:46 AM
Kakalende's Avatar
Kakalende Kakalende is offline
Kakalende just around
JF Senior Expert Member
Points: 431,887, Level: 100 Points: 431,887, Level: 100 Points: 431,887, Level: 100
Activity: 2% Activity: 2% Activity: 2%
 
Join Date: Fri Dec 2006
Location: Itoma
Posts: 1,143
Thanks: 26
Thanked 33 Times in 17 Posts
Rep Power: 26
Kakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enoughKakalende will become famous soon enough
Default

Huyu mtoto genius, Doctors are born and not made!
Reply With Quote
  #8  
Old 24th October 2007, 09:29 PM
Shukurani's Avatar
Shukurani Shukurani is offline
Shukurani has no status.
Senior Member
Points: 107,360, Level: 100 Points: 107,360, Level: 100 Points: 107,360, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Tue Oct 2007
Posts: 238
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 23
Shukurani will become famous soon enoughShukurani will become famous soon enoughShukurani will become famous soon enoughShukurani will become famous soon enoughShukurani will become famous soon enoughShukurani will become famous soon enoughShukurani will become famous soon enoughShukurani will become famous soon enough
Default

Huu ni uchizi,
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
15, amzalisha, mama, miaka, mtoto, njia, upasuaji


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Ni wakati wa kuacha woga! Invisible Habari na Hoja mchanganyiko 6 4th June 2009 10:01 PM
Utekelezaji wa kutangaza mali za viongozi wa umma malisak Jukwaa la Siasa 457 5th January 2009 05:53 AM
Idd Azzan: Nyani Mtoto Na Mama Yake maggid Habari na Hoja mchanganyiko 0 24th April 2007 06:43 AM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 12:19 PM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com