Mwanamema alimchanganya akili bwana Musa, hadi akiona unyasi anashtuka akifikiri ni NYOKA. Huyo alikuwa ni jabari la Muziki Marijan Shaaban (RIP). Nilifanikiwa kumuona huyu mzee LIVE pale Dar na kibendi mshenzi, machozi yalinitoka kwa furaha na majonzi. Sikuamini kuja siku moja kumuona live tena hata watu hawana time naye ila majonzi yalikuwa kumuona akiwa na kibendi mshenzi Kunduchi beach hotel..... Na hobby yangu kubwa ya muziki, milele nitamuenzi huyu mzee. Ule wimbo wa Mkuki Moyoni na Hanifa (Bamping style) zilinifanya nimuone kama nyota ya Tanzania baada ya sallum Abdallah...
__________________ .... hata kama akitambika uchi huyu mwakyembe, ukweli utabaki pale pale kuwa yeye nimiongoni mwa wale wabunge waliokula milioni 5 za rostam wakati wa kampeni (By: Game Theory)
Kelly na wengine wote mliochangia nawashukuru kwa kutupeleka miaka ile ambapo muziki ulikuwa muziki.
Nitashukuru sana kama kuna atakayeweza kuniwekea maneno ya wimbo uliowahi kuimbwa na Fresh Jumbe enzi hizo ( nadhani late 80s) akiwa na Mlimani Park unaitwa " "Conjesta" - wimbo huu unaimbwa siku hizi na In Afrika Band ( kina Roy, Bob Rudala, Biz man na wengineo ) na wanaupiga vizuri mno kama kopi.
ninakumbuka baadhi ya maneno kama ifuatavyo: Nimetembea, pande za dunia, mashariki na magharibi, Sijapata kumpata mwingine mwenye mapenzi ya kweli.... Na sasa kwako mpenzi, nimefikia ukingoni ....
nitashukuru sana kama mwenye maneno yote atuwekee hapa.
__________________ Do not dwell in the past, do not dream of the future, concentrate the mind on the present moment. -- Buddha
Kelly na wengine wote mliochangia nawashukuru kwa kutupeleka miaka ile ambapo muziki ulikuwa muziki.
Nitashukuru sana kama kuna atakayeweza kuniwekea maneno ya wimbo uliowahi kuimbwa na Fresh Jumbe enzi hizo ( nadhani late 80s) akiwa na Mlimani Park unaitwa " "Conjesta" - wimbo huu unaimbwa siku hizi na In Afrika Band ( kina Roy, Bob Rudala, Biz man na wengineo ) na wanaupiga vizuri mno kama kopi.
ninakumbuka baadhi ya maneno kama ifuatavyo: Nimetembea, pande za dunia, mashariki na magharibi, Sijapata kumpata mwingine mwenye mapenzi ya kweli.... Na sasa kwako mpenzi, nimefikia ukingoni ....
nitashukuru sana kama mwenye maneno yote atuwekee hapa.
Sitegemei kupenda mwingine tena zaidi yako wee Konjestaaaa...
Mtoto mwenye imani, ooh jesta nimeamua kukupenda wee pekee duniani
mtoto mwenye imani, ooh jesta nimeamua kukupenda wee pekee duniani.
Mapenzi mazito, sioni mwingine,wala sisikii la yeyote yule
"Sabah al Kheri Mpenzi"
I remember someone inquiring about this Old Taarab song found the Lyric by chanceon the Web:
An old Taarab/Swahili song by Culture Musical Club Zanzibar. (Lyrics)
-Sabah al kheir mpenzi waonaje hali yako
-sabah an nur Aziz hali yangu kama yako
-Wa'waonaje wazazi nyumbani utokeapo
-kawanusuru mwenyezi hofu yao juu yako
ebu nitoe majonzi unijuze shida yako
shida yangu sijiwezi dawa yangu sura yako
(mwenginewe hachomozi nakupenda peke yako)
(daima n'takuenzi silitupi pendo lako)
-usi'ingie simanzi sura yangu mali yako
-na kuikosa siwezi sikia langu tamko
-mwenginewe hachomozi nakupenda peke yako
-nimefanya uchunguzi nakiri maneno yako
naiyona waziwazi ishara ya pendo lako
-milele n'takuenzi natoa ahadi kwako
(mwenginewe hachomozi nakupenda peke yako)
(daima n'takuenzi silitupi pendo lako)
-kibaya sikivumbui ndani ya maungo yako
-na mimi simtambui mwenye sifa kama zako
-rangi yako ya samawi kama sufi ngozi yako
-na kuzikosa haiwi cheko na bashasha zako
wallahi sijichukuwi mgonjwa kwa raha zako
-ukaidi siujui mimi mar'dhia kwako
(mwenginewe hachomozi nakupenda peke yako)
(daima n'takuenzi silitupi pendo lako)