Tanesco Temeke hivi hamlijui tatizo la Low Voltage huku Kijichi Mgeni nani?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Hii imekua kero sasa kila ifikapo saa 1 na saa 2 usiku umeme hupungua nguvu kwa kiwango kikubwa mno na kusababisha baadhi ya nyumba kuzima kabisa kwa maana hata bulb hauwezi washa! na haurudi katika hali ya kawaida hadi saa 5/6 usiku.kitu ambacho kimesababisha tushindwe kufanya shughuli zetu nyingi muhimu ikiwa pamoja na kushindwa washa pump za maji,kutopata kutazama taarifa za habari saa mbili na saa nne kwa Tv,Nashindwa elewa ni kwanini Tanesco hawatatui tatizo hili wakati mbali ya sisi kununua umeme wao kila mwezi na wanatucharge 'service charge' pesa nyingi,Tanesco Temeke hamuoni kua hamtendi haki?au mpaka Magufuli avamie ofisi zenu ndio muamke?
Tunaomba yeyote humu Jf aliye karibu na ofisi hizo au jamaa ajaribu kulidokeza hilo wakati sie wakazi wa huku tukiangalia namna ya kuji organize kudai haki yetu...tafadhali Tanesco tunaomba haki itendeke haraka!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom